msuyaeric
JF-Expert Member
- Dec 18, 2014
- 862
- 1,249
Na, Kalamu ya Jenerali, Mbalali
Katika zama ambapo kilimo kilionekana kama kazi ya kizamani isiyo na tija, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekuja na mtazamo mpya, ambao umegeuza kilimo kuwa fursa muhimu ya kibiashara. Sauti za wakulima ambazo kwa muda mrefu zilisikika kama kilio kisicho na majibu, sasa zinasikika na hatua zenye matokeo zinachukuliwa.
Takwimu hazidanganyi. Ukuaji wa sekta ya kilimo umeongezeka kutoka asilimia 2.6 mwaka 2021 hadi asilimia 4.2 mwaka 2023. Na kwa mwendo huu, serikali inalenga kufikia asilimia 5 mwaka 2026 na hatimaye asilimia 10 ifikapo 2030.
Aidha, thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo nje ya nchi imeongezeka kutoka Dola bilioni 1.2 mwaka 2019/2020 hadi Dola bilioni 3.54 mwaka 2023/2024. Hili ni ongezeko la zaidi ya mara mbili katika kipindi kifupi hatua inayoonyesha Tanzania inatambulika si kwa utalii pekee, bali pia kwa ubora wa mazao yake ya kilimo duniani.
Uzalishaji wa mazao ya chakula umeongezeka kwa kiwango kikubwa kutoka tani milioni 17.14 mwaka 2021/2022 hadi tani milioni 22.80 mwaka 2023/2024. Sasa Watanzania hawazungumzii tu kuhusu usalama wa chakula, bali pia nafasi ya kuisambaza Afrika Mashariki na hata nje ya bara. Ndoto ya Tanzania kuwa food basket wa ukanda huu si hadithi tena ni mwelekeo wenye uhalisia.
Kwa upande wa mahindi, Tanzania sasa ni mzalishaji wa pili kwa ukubwa barani Afrika. Kutoka Tani milioni 6.4 mwaka 2021 hadi tani milioni 12.26 mwaka 2023/2024. Wakulima hawahitaji tena kusubiri miujiza ya mvua au huruma ya madalali, sasa wana uhakika wa pembejeo, elimu ya ugani, na masoko ya uhakika.
Mafanikio haya yamewezekana kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu, ikiwa ni pamoja na;
Kwa mara ya kwanza, wakulima tunajiona si wanyonge tena bali washirika halisi wa maendeleo ya taifa. Hili ni taifa la kazi, si maneno. Na kazi hiyo inaongozwa na Rais mchapakazi, msikivu, na mwenye maono.

- Kuimarisha huduma za ugani,
- Kuwezesha upatikanaji wa pembejeo bora kwa wakati,
- Kuanzisha skimu za kisasa za umwagiliaji,
- Kuweka mifumo ya masoko na bei shindani,
- Na kufufua taasisi kama bodi za mazao ili kuwa bega kwa bega na mkulima.