Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Mnyika's refusal of talking about his private life dissapoints Clouds FM

Sasa mbona ni kama unamponda tu? Kujua kuongea kitu kwa wakati muafaka si ndiyo ingekuwa pale! Halafu siyo kweli kuwa kukataa kuongelea mapenzi inamaanisha umakini wa mtu. Huyo Bush mwenyewe alikuwa anapiga story na Oprah. Mnyika nani bwaaaaanaaaaaaa?
Hebu fikiria ongea ya Diva na lafudhi yake! Unamfananisha Oprah na Bush! Swaga za Diva ni kuwahoji akina Diamond bwana! Si mtu kama Mnyika!
 
it was like this, una GF?

Simple answe: haya ni maisha binafsi na sio ya uma. Maisha yangu, kaka, dada na mke au kama hivo ni yangu sio ya uma.

Clouds FM inakata simu,

Poa tu kata.

Sasa hapa ana kosa gani jamani? Radhia umesema hiyo ni private life yake, sasa kama ni private kwanini iulizwe kwenye media ambayo ni public? Si ungeenda tu kumuuliza yeye mwenyewe binafsi angekujibu badala ya kumhoji kupitia Clouds Fm? Kwani ilikuwaje tukio zima na limetokeaje?

Naomba utusimulie zaidi mwenzangu

Asha
 
Binafsi nimependa majibu ya Mnyika J.J!!Kwan lazma kila kitu tutangaze kwa umma?
 
Hebu fikiria ongea ya Diva na lafudhi yake! Unamfananisha Oprah na Bush! Swaga za Diva ni kuwahoji akina Diamond bwana! Si mtu kama Mnyika!

kwanini alikubali mwaliko? Jamaa mshamba kinoma yaani.
 
it was like this, una GF?

Simple answe: haya ni maisha binafsi na sio ya uma. Maisha yangu, kaka, dada na mke au kama hivo ni yangu sio ya uma.

Clouds FM inakata simu,

Poa tu kata.
he was very right
Ukiendekeza mbwa atakufuata hadi msikitini
 
Mapenzi si jambo la publicity.
Kama hataki yanini wamuone adui?

Kafanya maamuzi yake kama Mnyika.si sahihi kupinga fikra zake.
 
Watu wametukana kishenzi kwenye FB account yake. Hii issue itampotezea mashabiki sana.
 
naitwa JMK.Rais wa JMT.dunia yangu,chaguo langu......,....,..! Unashindwa kukaa na kutafakari mambo mahimu.nchi inamatatizo kibao,unabaki unarekodi mambo hovyohovyo tu.
 
..."refusal to talk about" would have been a more grammatically correct phrase. Thank you
 
"Private live" siyo sawasawa na "public life". Well, akianza na una girlfriend akasema "ndiyo" na swali la pili likiwa "huwa unakutana naye mara ngapi kwa wiki" ataweza kukataa au hilo la pili ni more private kuliko hilo la kwanza? Private life inaweza kuzungumzwa kama imefanywa subject na mtu mwenyewe au matukio fulani lakini huwezi tu from nowhere kuuliza "una mchumba" inamhusu nini muulizaji?

Kama angekuwa smati wenzao huwa wanauliza "hypothetical questions"...
 
Lakini kipindi chenyewe ni cha mapenzi. Kama ulivyoyapanga hapo, maswali yake huwa yanakuwaga hivyohivyo. Kukipa nguvu kipindi, hata watu kama kina Zitto walishawahi kuhojiwa.
 
..."refusal to talk about" would have been a more grammatically correct phrase. Thank you

Toa umaimuna wako hapo. Kuna 'refuses to talk about' na ' refusal of taking about'. Only wrongly written is the word 'dissapoint'
 
Kipindi kinazungumzia mapenzi, jamaa anakataa kukubali kama ana mchumba au hana. Hivi kuna tatizo gani hapo? Mbona mwenzake Zitto huwa anakubali?

kwani Zito ni mwenza wa Mnyika????

hiyo ni tungo tata na ashakum si matusi nnavyofahamu Zito hana u-wenza na Mnyika kwa maana zote za neno mwenza ikiwemo ambayo pengine ndiyo unayoikusudia ya kuwa wote ni wanasiasa.

Nadhani Zito is a liberal katika mambo ya mapenzi wakati Mnyika ni conservative..yote ni mitazamo na yote ni sahihi kama ni wewe ni objective great thinker lakini kama wewe ni subjective great thinker..utachukua upande kama ambavyo Radhia Sweety umefanya.

Muhimu ni kutambua si kila kifanywacho na wengi au akina fulani ndiyo sheria na kwamba wote lazima tupite njia hiyo. Mfano, binafsi napingana na utamaduni wa kumfanya mke wa Rais kuwa first lady...najiuliza why first lady, sisi tumepiga kura kuchagua rais na siyo kuchagua first lady, kama yeye ni first lady basi na iwe nyumbani kwake na kwa mumewe, hii habari ya mke wa rais naye ni kama kiji-rais inatoka wapi? Najua utaniambia mbona wenzetu wanafanya na pengine ukanipigia mfano wa marekani, nami ntakuuliza mbona wenzetu wengine hawafanyi mfano Waingereza, Waarabu nk.

Ni mitazamo tu..so big up Mnyika...simamia kile unachokiamini...achana na wapuuzi wanoitazama dunia mfano mtu mwenye chongo!!!
 
Watu wametukana kishenzi kwenye FB account yake. Hii issue itampotezea mashabiki sana.

waliotukana kishenzi pasi na shaka watakuwa ni washenzi...sidhani kama Mnyika anahitaji kujali sana kupoteza mashabiki washenzi.

mashabiki waungwana tupo na tutaendelea kumpa support
 
waliotukana kishenzi pasi na shaka watakuwa ni washenzi...sidhani kama Mnyika anahitaji kujali sana kupoteza mashabiki washenzi.

mashabiki waungwana tupo na tutaendelea kumpa support

Utakuwa Mnyika wewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom