Haya turudi kwenye mada sasa... kama ndo utachukulia kila siku huwa naiponda CHADEMA, shauri yako!! If you're serious, tafuteni watu wenye ushawishi na uwezo wakaongoze kanda ambazo CHADEMA haina nguvu na katu, domicile ya mtu isiwe ndiyo kigezo cha kumfanya awe kiongozi wa kanda husika!! IKiwa pale Ufipa kuna watu walio na nguvu ya ushawishi, wapelekeni huko wakajenge uelewa vinginevyo kila siku mtaishia kulalamika kwamba mmeibiwa kura wakati hakuna jitihada ambazo zilifanyika katika kupata hizo kura! Kilal siku mtaendelea kulalamika kwamba watu wa kusini hawajasoma kumbe ni wenyewe ndio mmeshindwa kuwashawishi!! Zamani sana, kama sikosei mwaka 2009, niliwahi kusema hapa hapa jamvini kwamba CHADEMA wana nafasi kubwa sana ya ku-excel maeno kama ya Kusini, Singida, na Rukwa coz' yale maeneo yamesahaulika mno, na kila dongo utakalopiga dhidi ya CCM, lazima litatua mahala pake!! Lakini kama ilivyo kawaida, mkaanza kashifa... mlitaka eti niseme CHADEMA ina nguvu kila mahali!!Nimesha muomba chemba...Tusonge mbele
Hivyo basi, wale akina Mnyika hakuna wanachofanya pale Ufipa katika kipindi lala salama kama hiki ingawaje ni kweli pia timing imeshakuwa ngumu tofauti na pale tuliposhauri kwa mara ya kwanza! Yule Mnyika na watu wengine kama yeye, hakuna cha maana wanachofanya pale Ufipa zaidi ya kusubiria viongozi wa serikali waharibu kisha waitishe press conference na kutishia kuandamana! Yapo mambo ya msingi zaidi ya kufanya kuliko hayo ya kila siku kuitisha press conference! Yule Profesa Safari yule... are you guys serious? Mtu mwenyewe hata kuongea ni taabu tupu halafu mnampa kanda yenye changamoto kama ya Mashariki!! Tangu lini Profesa Safari amebobea kwenye siasa za majukwaani hata apewe jukumu zito kama hilo?! Au ilikuwa ni lazima apate nafasi??