Crashwise, naona unachofanya hapa ni kuangalia "huyu mwenzetu" na huyu "sio mwenzetu!" Ingekuwa ni mtu unayetaka kusimamia unachokisema, ungeanza kuangalia wapi tumetokea! Kwanza labda nikuambie jambo moja! Huyo anayejiita Chademakwanza mie nilikuwa namuheshimu sana... na haikuwahi kutokea hata siku kum-quote popote ama kumtolea lugha chafu! Ile kuingia tu, kani-quote post ambayo sikumkashifu yeyote akaanza kwa lugha chafu:Akaona hiyo haitoshi, akaja na nyingine:Akaona bado tu, akani-quote tena: Come one, halafu unaona alichokifanya huyo jamaa ni sawa? Au kwavile ni CHADEMA mwenzako? Ndo maana nasema CHADEMA na CCM wote ni sawa tu... huku kulindana na kuteteana kwenye ujinga mnakofanya kwenye mitandao kwa mambo yaliyo dhahiri, ndiyo mtakayokuwa mnafanya hata hapo baadae! Ni bora ungekaa kimyaa kuliko kuona alichofanya mwenzako ni sawa na hakitakiwi kukemewa lakini alichofanya asiye mwenzako katika kujibu wa kile alichifanya mwenzako ndicho kinapaswa kuhojiwa! Sasa tofauti yenu hapo ipo iko wapi?