Ni-prove kwani natafuta nini? Ningekuwa nimewahi kujinasibisha na CHADEMA basi labda ningetakiwa ku-prove ili kuonesha kwamba bado nipo kundini! Halafu unajua nini ndugu yangu... tatizo lenu huwa mnapenda zile posts zinazowa-favor nyinyi peke yake; siku nyingine mkipewa za uso, ndipo zinapoanza kashfa! Umeleta suala la Jukwaa la Elimu coz' kwa inavyoelekea matokeo ya mwaka jana yalikuathiri ama wewe moja kwa moja au mtu wako wa karibu na kwavile niliponda kwa nguvu zote mfumo uliotumika katika matokeo yale, pale ndo ukaniona mwenzako! Lakini ninapokuja na posts kama hizi:Wewe ndiyo unatakiwa uprove kwamba upo neutral na sio kazi yangu mimi tena, utetezi ni juu yako maana mimi ni mshtaki wako mkuu.
Mkuu rudi tu jukwaa la elimu kule ndio huwa unakuwa kichwa kwa kushusha nondo za maana lakini hili jukwaa la siasa hapana, usilaghai watu upo neutral kitu ambachovsi kweli hata kidogo.
Lastly, hiyo 50,000 mtumie Ludovick kwa Mpesa coz ndiyo price tag yake, kwangu sina shida naz😵VER
Tobaaaa! Hapo mtaita kila majina... kwa sababu mnataka kuyasikia yale tu mnayotaka kuyasikia! Sie wengine hatuna sababu ya kumfurahisha yeyote humu jamvini, na katika siasa za Tanzania, ni mara kibao nimeshasema kwamba kwangu mimi CCM na upinzani ni wale wale tu:WANACHONIKERA CHADEMA, iwe kwa viongozi wao wakuu, wa kati na hata wafuasi wa kawaida, ni hivi vilio vya kuhujumiwa ama kugawanywa na CCM!! Kwanini mkubali kugawanywa au kuhujumiwa?
Leo akija mtu kwangu, kisha akanifitinisha na ndugu yangu; nami nikazichukua fitina hizo....je, mpumbavu hapo ni nani? Yule mfitini au mimi niliyekubali kufitinishwa?! Kwani CHADEMA ni chama cha watoto wadogo wenye uwezo mdogo wa utambuzi?! Hivi tatizo ni CCM au ni nyinyi wenyewe ambao miongoni mwenu kuna waganga njaa?!
Mathalani, kama kweli Ludovick alipewa TZS 50,000/- ili atengeneze ile video, sasa wa kulaumiwa hapo ni Nchemba au nyinyi wenyewe!! Ikiwa "wanaorubuniwa na CCM" ni watu wazima tena wenye nyadhifa basi tatizo kuu ni chama chenu wenyewe na sio CCM....yaani, you're so cheap hadi mnakera!!
Wanaume wazima kila siku mnalia lia kwamba CCM wanawagawanya, mara CCM wanawahujumu; STUPID! Kwani nyinyi hamjui hao CCM wanapatikana wapi? Nanyi si muwagawanye tu, ala! Mtabaki kulia lia hivi hivi kila cku....
I'll always insist, No Any Political Ground Has Clean Players, NONE....wherever you go!! We call it politics of survival. The more cheap players u've in your team, the more the chance to be defeated!
Kwangu mimi hakuna tofauti! Wabunge wa CCM na wa CHADEMA; wote ni wale wale tu; CCM au CHADEMA wote hawa ni one and the same, mmoja ni HEROIN na mwingine ni COCAINE....wote ni illegal drugs! Mmoja huku ataitwa chang'aa na kule ataitwa Gongo; lakini kumbe ni wale wale tu!! Tofauti kubwa ni kwamba huyu yupo jikoni anajipakulia apendavyo na mwingine yupo on transit kuingia jikoni ili akafanye kama mwenzake!
Hata hivyo, wapo wachache sana ambao wanaweza kuonekana kwamba ni bora lakini wengi zaidi katika hao wachache zaidi wataonekana ni bora kwavile tu ni wazuri katika ku-manipulate akili za Watanzania!! Hao ndio wale ambao hapa wamekuwa wakionekana ndo kama Wakombozi wa Kweli wa nchi hii; kumbe miongoni mwao kuna Nabii Mussa na upande wa pili kukiwa na Joshua; wote hawa wakiwa na lengo la kutufikisha kwenye Nchi ya Ahadi; nchi inayotiririka maziwa na asali! Thanks god, mimi si miongoni mwa wale wanaoweza kudanganywa kirahisi!-- Posted on October 31, 2013