Kwakusema hayo mkuu
NasDaz ningeomba uangalie wazo hili na labda tujikite kutokana na hapa tulipo, Uboreshaji wa kanda hizi na nguvu yake kuelekea uchaguzi mkuu. Na Vilevile tukumbuke hapa ilipo leo Chadema kwenye kanda hizi za kusini sipo ilipokuwa hapo awali, kiuhakika imesonga mbele ingawaje si kwa kiwango kile kilichotegemewa ama kulinganisha na Kanda zingine.
BACK TANGANYIKA
Mkuu wangu, kwanza ahsante kwa kunielewa! Sasa tukija hili suala la nguvu za chama huku kule, labda nikujuze jambo moja! Tofauti na watu kama akina
Crashwise ambao inaonekana anaishi Arusha huku akiwa hana mafungamano yoyote na sehemu kama Kusini, mimi binafsi ni mtu wa Kusini; mkoa wa Lindi! Issue ya CHADEMA kule Lindi niliileta kwa mara ya kwanza mwaka 2009. Kuna ndugu yangu wa damu alikuja Dar es salaam... yeye alikuwa ni kiongozi wa CUF kule! Nakumbuka kabla sijakaa sawa, swali langu la kwanza kumuuliza ni nguvu ya CHADEMA kule alikotoka! Jibu ambalo alinipa ni kwamba Kusini CHADEMA haipo kabisa! Nikaona dogo ananipiga changa... nikamuuliza in other way round na kutaka kufahamu, pale kijijini kwetu (ambacho ni moja ya vijiji vikubwa sana kwa Mkoa wa Lindi) kuna wenyeviti wa vitongoji wangapi kutoka CHADEMA; akanijibu mwenyekiti wa kitongoji atoke wapi wakati hata ofisi ya kusingiziwa' iwe barazani kwa mtu au sebuleni, hawana!! Kiukweli, mie sikuridhishwa sana na majibu yake coz' nikaona bado ananindanganya! Kuona hivyo, nikaanza kuongea na watu wengine wa kule! Huo wakati nikawa kama chizi, napiga simu huku na kule na namba zingine nikiomba kutoka kwa watu mbali mbali.... nikaona sehemu pekee kwa wakati huo ambako angalau CHADEMA ilikuwepo ni Nachingwea! And remember, wengine niliokuwa naongea nao wala siwafahamu... ni kwavile tu niliomba namba zao!
Baada ya kujiridhisha na hiyo hali, nikaja na hiyo mada hapa jamvini!! Kama kuna siku ambayo nilitukanwa hapa jamvini, basi ni hiyo siku na wale wanaojiita wao ni makamanda!!! Wengine hoja ya ikawa ni kwanini basi kama ninajifanya nina uchungu na CHADEMA mimi niineze hiyi CHADEMA huko kusini as if nimeawaambia nami ni mwanasiasa!
Hivyo basi, kwa kukupa hiyo historia mimi huwa naongea kitu ambacho nina ushahidi nacho! Wapo watu ambao wanaongea kutokana na ushabiki... mimi sio mwana-CHADEMA haidhuru hata kama kuna wengine wananiita CCM na wengine kuniita ACT... kwahiyo kitu ambacho nitasema mimi ni tofauti na kile ambacho kitasemwa na mwana-CHADEMA!
Crashwise alinitolea ushahidi wa picha kwenye mikutano, bado nasisitiza, Dr. Slaa kujaza kwenye mikutano wala sio kigezo cha kuwa na ufuasi... Dr. Slaa Mungu kampa kariba hiyo; popote atakapoenda, watu watataka kumsikiliza! Lakini kubwa zaidi, watu wanapokusanyika kwenye mikutano wanakuwa wametawaliwa na emotions... unaweza ku-recruit hata wananchama 5000 kwenye mkutano mmoja lakini royal members hapo wakabaki less than 100! Sie ambao tumesomea masuala ya customer services tunafahamu kwamba it's very simple to recruit 10 or more customers than retaining only one!! Mikutano ya CHADEMA kule ambako haijapata mizizi ya kutosha inatumika kama njia ya ku-recruit customers lakini hakuna strategies za ku-maintain wanachama ambao walisukumwa na mob psychology! Unaenda kijijii unapiga mkutano wa hadhara, unapata bonge la umati na wanachama, baada ya hapo unatoka bila kuacha strategies za namna gani wale waliopatikana watakuwa retained. Hivyo basi, ingawaje ni kweli hata huko kusini "nguvu" ya CHADEMA iliyonayo leo hii ni tofauti na ilivyokuwa maiaka 5 iliyopita, lakini bado sana! Wakati ule Nilisema wazi ni namna gani sehemu iliyosahaulika kama ile ingeweza kuwa mtaji mkubwa kisiasa coz' kila dongo utakalorusha kwa serikali, linatua mahala pake! Na hii ikaja kuthibitika kwenye uchaguzi wa mwaka 2010! CUF ingawaje walikuwa na wanachama Lindi, lakini hawakuwa na nguvu kivile lakini kambi ya siku 6 tu ambayo Lipumba aliifanya, CUF wakafanikiwa kupata wabunge wawili! Wakati Lipumba aliweka kambi ya siku 6 Lindi peke yake, Dr. Slaa alitumia saa chache kwa Lindi na Mtwara kwa pamoja... watu wa Kusini walipoipa CHADEMA za uso, kama kawaida ya baadhi ya mashabiki wa CHADEMA wa JF, tukatukanwa sana watu wa kusini kwamba hatujasoma ndo maana tunaichagua CCM na kwahiyo tutaendelea kuwa masikini miaka yote!