J Mnyika, Aunguruma Channel TEN, Athibitisha maridhiano yameisaidia Sana CHADEMA, Sasa Inayatambua Matokeo, Inalitambua Bunge na Kumtambua Mbunge Wake

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,558
113,746
Wanabodi

Kupitia kipindi changu kipya cha KMT, kinachorushwa hewani na kituo cha Television cha Channel Ten, kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku na marudio siku za Jumatano Saa 9:30 alasiri, Katibu Mkuu wa Chadema, JJ. Mnyika, ameunguruma na amezungumza mengi.

Kwa wale ambao bundle sio issue, kipindi chenyewe ni hiki
View: https://youtu.be/owBvx8H2H68?si=2kaPHEBJkcQoObcS

Ila pia mimi ni Mtanzania mzalendo, naijua hali ya uchumi ya Watanzania wengi kuhusiana na bundle, wengi bundle ni issue hivyo hawawezi kutazama kipindi chote, hivyo nimewadondolea baadhi ya dondoo zake muhimu.

1. JJ. Mnyika ametoa maoni ya jumla ya Chadema, wametaka miswada yote iondolewe kwanza, serikali ilete kwanza marekebisho madogo ya katiba, minimum reforms, katiba ifanyiwe mabadiliko kwanza ndipo miswada hiyo iletwe.
View: https://youtu.be/CRLiQjOQpro?si=6xgfm7aBX7Lvo0wQ

2. JJ Mnyika amethibitisha jinsi maridhiano na CCM yalivyo isaidia Chadema, ambapo mwanzo waligoma kuutambua uchaguzi na kuyatambua matokeo, lakini kupitia maridhiano sasa Chadema inautambua uchaguzi, inayatambua matokeo ya uchaguzi, inamtambua mshindi halali wa uchaguzi huo, inalitambua Bunge na kumtambua Mbunge wake mmoja tuu, Aida Kenani.
View: https://youtu.be/x5yFws4dc1U?si=Vi0dqREdT7AIhtme

3. Kufuatia Chadema kumtambua rasmi Mhe. Aida Khenani kama mbunge wake rasmi, JJ. Mnyika ameomba Mhe. Aida apewe muda wa kutosha kuchangia, na maoni yake yazingatiwe kama maoni ya kambi rasmi ya upinzani
View: https://youtu.be/r-SmiYZUOXc?si=HOrGl7qHppPYeF5v

4. Pia JJ Mnyika amejitahidi kujibu hoja mbalimbali za mwandishi Pasco Mayalla, zikiwemo hoja kuhusu wale wabunge wake 19, likiwemo jibu la swali ”Kwanini Chadema mpaka leo haijaripoti polisi kuhusu jinai ya kughushi ya wabunge hao 19?”
View: https://youtu.be/-M8HnYQgtAc?si=mBlAuAvub0JcokXp

5. JJ Mnyika, amesema Chadema ina uthibitisho wa uhusika wa mamlaka za nchi katika jinai ya kughushi uteuzi wa wabunge 19, serikali ikihusika na jinai, jeshi la polisi halifanyi uchunguzi!. Hata shambulio la Lissu, mamlaka ilihusika ndio maana mpaka leo hakuna uchunguzi wowote wa kijinai
View: https://youtu.be/CH1amKvbsQc?si=4_QhuIr4MXrYpv5J

6. Pia JJ Mnyika amethibitisha Chadema iliwatimua wabunge wake 19, kihalali kabisa kwa mujibu wa katiba ya Chadema, na Mahakama imethibitisha,

View: https://youtu.be/aJWb6Vkdx_s?si=E0oxq3R74CsGySah

Kipindi kilichopita nilizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salim Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema.
Wale ambao hamkukiona na bundle sio issue, mnaweza kukiangalia hapa

Vipindi vijavyo, kwa Chadema, nitamtafuta Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe,kwa ACT Wazalendo ,nitamtafuta Zitto na OMO, na kwa CCM Makonda atatosha.

Usikose!.
Paskali
 
Wanabodi

Kupitia kipindi changu kipya cha KMT, kinachorushwa hewani na Channel Ten, Katibu Mkuu wa Chadema, JJ. Mnyika, Kuunguruma Kuanzia Saa 3:00 Usiku.

Katika kipindi hicho, JJ. Mnyika atathibitisha jinsi maridhiano na CCM yalivyo isaidia Chadema, ambapo mwanzo waligoma kuutambua
uchaguzi na kuyatambua matokeo, lakini kupitia maridhiano sasa Chadema inautambua uchaguzi, inayatambua matokeo ya uchaguzi, na kumtambua Mbunge wake mmoja tuu, Aida Kenani.

Pia JJ Mnyika atajibu hoja mbalimbali za Mwandishi Pascal Mayalla, zikiwemo hoja kuhusu wabunge wake 19,
Kwanini Chadema mpaka leo haijaripoti polisi kuhusu jinai ya kughushi ya wabunge hao 19.

Jiunge nami hiyo saa 3:00 nitakuleta live kupitia hapa if na kupitia mitandao ya kijamii.

Kipindi kilichopita nilizungumza na Salim Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema

Vipindi vijavyo, nitamtafuta Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Usikose!.
Paskali
Tuombe Mungu kama kitakuwepo
 
kwahiyo Mmeamua kutufanya wapumbafu ?Kama ni hivyo siyo CCM wala CHADEMA wa kukaa madarakani ila bado mzungu ana mandatory ya kututawala direct coz nyote hamjielewi.
 
Wanabodi

Kupitia kipindi changu kipya cha KMT, kinachorushwa hewani na Channel Ten, Katibu Mkuu wa Chadema, JJ. Mnyika, Kuunguruma Kuanzia Saa 3:00 Usiku.

Katika kipindi hicho, JJ. Mnyika atathibitisha jinsi maridhiano na CCM yalivyo isaidia Chadema, ambapo mwanzo waligoma kuutambua
uchaguzi na kuyatambua matokeo, lakini kupitia maridhiano sasa Chadema inautambua uchaguzi, inayatambua matokeo ya uchaguzi, na kumtambua Mbunge wake mmoja tuu, Aida Kenani.

Pia JJ Mnyika atajibu hoja mbalimbali za Mwandishi Pascal Mayalla, zikiwemo hoja kuhusu wabunge wake 19,
Kwanini Chadema mpaka leo haijaripoti polisi kuhusu jinai ya kughushi ya wabunge hao 19.

Jiunge nami hiyo saa 3:00 nitakuleta live kupitia hapa if na kupitia mitandao ya kijamii.

Kipindi kilichopita nilizungumza na Salim Mwalimu na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Chadema

Vipindi vijavyo, nitamtafuta Tundu Lissu na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.

Usikose!.
Paskali
Safii sana japo hakuwatendea haki wafuasi wao kuwajulisha kua walishatema ndoano kitambo!
 
Paskali tunakuheshimu sana ujue! Sasa live gani iliyokwisha kurekodiwa na baadhi ya maswali amekujibu na watazamaji watarajiwa umeshatujibu?
 
Back
Top Bottom