Mnisamehe ila sitawasahau waarabu wa ISIL

Mnisamehe ila sitawasahau waarabu wa ISIL

Jana kuna mateka mwingine katupwa kutoka ghorofani huku kazibwa macho na kufungwa miguu na mikono.
Walivyoona hajafa, wakammalizia kwa kumponda kwa mawe mpaka kufa kutimiza sheria ya kadhi.
Kisa: Kisa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Sos: bbctv.

kama ni ukweli kabisa huyo muhanga alikua ni msodoma namuunga mkono kadhi ila kama ni fitina zao tu damu yake naiwe juu yao
 
mkuu umesema kweli kabisa. dah kama tukio hili la kuchinjwa lingetokea znz ingekua ni balaa.

Unajua hawa wakiristo wa dunia ya leo wanaishi na waislam kama wake wenza hawaoni maxuri ya uislam na waislam wala hawaoni machafu ya wakiristo wao wpo kuangalia muislam kafanya nini wiki mbili nyuma huko katavi kuna mwanaume mkiristo kamchinja mwanaume mkiristo mwenzie halafu kamkata kichwa na sehemu za siri halafu kazichemsha ktk masufuria mawili kichwa sufuria lake na sehem za siri sufuria lake lakini hakuna mtu alie sema mkiristo amchinja mtu na kumkatakata na kumchemsha....mungu mkubwa mauwaji yale yangefanywa na muislam au yangefanyika znz pasinge tosha mpaka mrithi wa Nchimbi angekwenda inyonga katavi....
 
Daaaaaa kwa hiyo kwa mtazamo wako ni sawa ISIS, Boko Haram na Al shababu kufanya wanaofanya??!!?? Unadhani wanaowaua ni akina kama sio waislamu wenzao???
Siyo sawa kumuua binadamu mwenziyo lakini kwanini haya makundi yanakuwepo??Ireland walikuwa wakatili ajabu mtu anaenda posta kipindi kama chajioni au asubuhi daladala inavyojaa analipua lote na hawakuitwa magaidi sijui kwakuwa walikuwa wazungu leo hii!Inashangaza sana!Na hii ni vita ambayo haiwezi kuisha kama watu wananyimwa haki zao!
 
Uojini mwenzenu faizer alikimbilia seminary school Leo anawezakumsahihisha hats pdidy nendakwawenzangu pale kariakoo al-.....loh shida sijuikamabadoipo ileshule rhaman unganisha utapatajinakamili,,,nenda vyuoni angalia wanaodesa wanatokeawapi. Fanya svhoolmqppingyaouineshule wakizopotia,,,,ntarudibaadae mshukuruni faizer f ndio anawatoa aibuhumundani elsemngekuwa mnacheza najukwaa lawakubwaatuu kushangilia pichazile,,,congs ff
 
Huyo rubani aliyeshikwa unasema alikuwa kazini, hivi ni kazi ipi? Kuiendesha ndege ya kivita akizurura tu?

huyu faizafoxy siku zote vile viovu wewe unachangia, mfano ufisadi, siasa, kuanguka kwa uchumi wa tz, wauza sembe, we unawapa big up, mie naona we si mtanzania na huna uzalendo na nchi hii,
 
Hukijui unacho kizungumza ww...unalopoka sana

yawezekana mkuu kweli sikijui.ila uoga wa kuyakakosoa haya makundi kwa kuogopa kushambuliwa hicho ndio nakijua.Hawa wahuni wanaichafua imani yenu hamuwakemei
 
yawezekana mkuu kweli sikijui.ila uoga wa kuyakakosoa haya makundi kwa kuogopa kushambuliwa hicho ndio nakijua.Hawa wahuni wanaichafua imani yenu hamuwakemei

Kwani ndugu hapa hatuyakosoi au we mwenzetu untaka tuyakosoe vipi labda.
 
Elewa kuwa hao waarabu nao ni watu sio malaika,na wana uwezo wa kushawishika kama watu wowote na wakatumika kama proxy.
ukifuatilia mwanzilishi wa isis,al baghdad alikua ni mateka wa wamarekani baada ya vile vita vya algaida in irag na occupied force,yaani marekani.
marekani wana system ya kuwaturn ama kuwabadili wafungwa wao wa al gaida ili watoke jail kwa makubaliano ya kufanya kazi chafu za marekani ama ku inftraite maadui zao.
hicho ndo walifanya marekani kumgeuza baghdad afanye kazi zao,na hii ilikua ni baada ya serikali ya irag chini ya malik kuwa imeegemea sana iran.
ikaonekana marekani wamepoteza matrilion kumtoa saddamu then irag imeangukia kwa iran.
ndo wakamwachia baghdad afanye kazi maalumu.
kumbuka mwaka 2012 hapakuwepo na kitu kinaitwa isis.
imezuka ghafla na kwa kasi ya ajabu sana,hasa baada ya mkutano wa putin na bandar bush,alipokua akimshikiniza putin aachane na assad,na baada ya putin kukataa,ndo hasa kivumbi cha isis kilianza,waliamua kutumia njia ndefu kumng'oa assad,kwa kuanza na kuikamata baghdad kwani assad anapata silaha zote toka iran na russia kupitia irag.
baada ya kushindikana ndo isis ika degenerate na sasa wanataka kutwanga kotekote,si saud,jordan,lebanon etc kasoro tu israel.

Nashukuru sana kwa habari za ndani ambazo sikuzijua, lkn swali langu linabaki pale pale kuwa waarabu bado hajitambui au hawana ushirikiano au hawana interijensia kujua adui yao ni nani hasa. kwa maelezo yako marekani anacheza na akili za waarabu huku akijifanya rafiki wa nchi furani lkn mission ikikamilika anabadirika, waarabu wanapaswa kupata somo toka iraq, libya na nk. tuache IS bado kuna maeneo mengine ambayo waislamu wanauana wao kwa wao, me nijuavyowaislamu ni ndugu ni dhambi kumuua mwislamu mwenzako, sasa mbona hawalitambui?
 
Kwa uelewa wangu niliokuwa nao asilimia kubwa ya waarabu wanaojiunga na hayo makundi ni wale wenye uraia wa ulaya ata hao isis wengi wao utasikia wanatoka uk na kwenda kujiunga.Sasa we fikiri muarabu umelelewa huko utakuwa unajua utalishwa sumu gani alafu hii ni mipango inapangwa ikapangika mfano angalia nani alimuua mfalme faisal na alitoka wapi na kwa maslahi yepi.Ivi uwe na watu kama panya road uwape siraha na mishahara minono uwaambie waanzishe mapinduzi kwa muavuli wowote ule uwe wa kidini ya kiislam au kikristo matokeo yake unajua ni nini ? Jibu lake ndo hayo yanayotokea uarabuni.
 
Unajua kuna vitu vingine vinachekesha sana duniani hapa,, Sasa unategemea huyu rubani hawa ISIL watamfanya nini??
huyu rubani alikuwa akipita juu angani na kuwashushia mabomu hawa ISIL, na kuua wafuasi wa ISIL na wao wamemkamata, je unategemea watamfanya nini??? DUNIANI NI SEHEMU SALAMA TU KAMA UNAFIKI UTAACHWA,,, TUKIENDELEA KUWA WANAFIKI DUNIA HAIWEZI KUWA SALAMA.......
 
Kwa mtazamo wangu wote hao ni mchezo wa kuigizwa unaochezwa na mabwana wakubwa kupiga vita Uislam, walishasema siku nyingi, baada ya ukomunisti sasa ni Uislam. Lakini wapi, Uislam si ideology uislam ni mfumo pekee wa kuishi duniani.

Hakuna atakae utazama Uislam kwa mafundisho yake ambae ataukana Uislam kuwa ni mfumo bora na wa pekee wa kuishi duniani.

Kama mafundisho ni bora hao mashaitwan kwa nini wanasema watu wengine ni makafiri? Ndo maana kiongozi wenu alioa mtoto! Uzinzi mtupu! l
 
Exactly how I feel right now!

Rebels and weapon from western.JPG

Waliwapa Silaha 'Wahuni' ili wamkomoe Assad ! :A S-frusty2:
 
Cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyelaani mauaji ya kimbari yaliyofanywa na USA na NATO yakishirikisha silaha nzito nzito kuwaua wa Iraq wa Syria na wengineo.

Mtoto anaona wazee wake wameuliwa mbele yake halafu akikuwa unategemea atampenda aliowaua wazee wake?

Unyama wa kuuwana kwa mamilioni uliofanywa kwa kuuwana Wakristo kwa Wakristo vita ya kwanza na ya pili ya Dunia sijasikia mtu akiushutumu Ukristo kuwa ndiyo uliofanya mauaji hayo.

Mauaji ya kutisha yaliofanyika Ireland ya kuuwana Wakristo kwa Wakristo sijasikia mtu akilalamikia Ukristo.

Mauaji waliouna Rwanda Wakristo kwa Wakristo ki unyama kabisa sijasikia mtu anaulaumu Ukristo.

Mauaji yanayofanywa leo hii na anti balaka ya kusafisha kabisa kila Muislam anaekutwa sijasikia ukilaumiwa Ukristo.

Leo mtu anakuja na daku zake halafu anaulaumu Uislam kwa mambo ambao hatuyajui na nna wasiwasi mkubwa sana kuwa wanayoyafanya hayo ni hao hao adui za Uislam ili kuupaka matope Uislam.

So true
 
Nashukuru sana kwa habari za ndani ambazo sikuzijua, lkn swali langu linabaki pale pale kuwa waarabu bado hajitambui au hawana ushirikiano au hawana interijensia kujua adui yao ni nani hasa. kwa maelezo yako marekani anacheza na akili za waarabu huku akijifanya rafiki wa nchi furani lkn mission ikikamilika anabadirika, waarabu wanapaswa kupata somo toka iraq, libya na nk. tuache IS bado kuna maeneo mengine ambayo waislamu wanauana wao kwa wao, me nijuavyowaislamu ni ndugu ni dhambi kumuua mwislamu mwenzako, sasa mbona hawalitambui?

..........ukisha vunja ushirikiano wataelewana vipi !? Arab League of Nations haina maana tena na 'OPEC' ilikufa zamaaani !
Leo hii bei ya mafuta imeanguka Duniani kwakuwa mafuta yanauzwa na 'wahuni' na si Serikali !
 
Cha kushangaza hakuna hata mmoja aliyelaani mauaji ya kimbari yaliyofanywa na USA na NATO yakishirikisha silaha nzito nzito kuwaua wa Iraq wa Syria na wengineo.

Mtoto anaona wazee wake wameuliwa mbele yake halafu akikuwa unategemea atampenda aliowaua wazee wake?

Unyama wa kuuwana kwa mamilioni uliofanywa kwa kuuwana Wakristo kwa Wakristo vita ya kwanza na ya pili ya Dunia sijasikia mtu akiushutumu Ukristo kuwa ndiyo uliofanya mauaji hayo.

Mauaji ya kutisha yaliofanyika Ireland ya kuuwana Wakristo kwa Wakristo sijasikia mtu akilalamikia Ukristo.

Mauaji waliouna Rwanda Wakristo kwa Wakristo ki unyama kabisa sijasikia mtu anaulaumu Ukristo.

Mauaji yanayofanywa leo hii na anti balaka ya kusafisha kabisa kila Muislam anaekutwa sijasikia ukilaumiwa Ukristo.

Leo mtu anakuja na daku zake halafu anaulaumu Uislam kwa mambo ambao hatuyajui na nna wasiwasi mkubwa sana kuwa wanayoyafanya hayo ni hao hao adui za Uislam ili kuupaka matope Uislam.

Red Indians Masacre.JPG

Ushahidi wa Mauaji ya Marekani huu hapa !
 
Nashukuru sana kwa habari za ndani ambazo sikuzijua, lkn swali langu linabaki pale pale kuwa waarabu bado hajitambui au hawana ushirikiano au hawana interijensia kujua adui yao ni nani hasa. kwa maelezo yako marekani anacheza na akili za waarabu huku akijifanya rafiki wa nchi furani lkn mission ikikamilika anabadirika, waarabu wanapaswa kupata somo toka iraq, libya na nk. tuache IS bado kuna maeneo mengine ambayo waislamu wanauana wao kwa wao, me nijuavyowaislamu ni ndugu ni dhambi kumuua mwislamu mwenzako, sasa mbona hawalitambui?
Kil mtu ana ajenda yake,hata sehemu zingine wakiristo pia wanauana sana,rejea ukraine kwa mfano wa haraka.
sawa quran inawataka waislamu wawe kama ndugu ,sawa,umesema wazi baadhi ya sehemu.
pia maandiko yapo ili yafuatwe japo hayafuatwi kwa asilimia zote.
unataka kunambia wewe mkiristo na wenzako mnafuata bible kwa asilimia mia kwa mia?,japo sikatai wapo wakristo wacha mungu.
we binafsi ushawahi kugeuza shavu la pili baada ya kuchapwa kofi?.
ushauza kila kilicho chako ukamfuata yesu?,
 
Naomba niweke wazi kuwa mimi ni mkristu. Baba yangu kabla hajasitaafu aliwahi kufundisha shule moja huko Kigoma ujiji shule iitwayo Bugamba.

Wenyeji wa kule asilimia kubwa ni waislam, waislamu wa Kigoma ni wakarimu sana hakika nilijumuika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kuamsha waumini wa kiislamu kula daku usiku kwa ngoma baada ya kupitiwa na rafiki yangu muislamu kwa jina la Migezo pamoja na marehemu Pili watoto wa mwalimu Babu.

Baadae miaka ya 2004 nilienda kutafuta maisha Zanzibar na sehemu ya kwanza kuishi ilikuwa Mwembemchomeke kabla sijahamia Melisita ukivuka Kwerekwe kuelekea Fuoni. Ndg zangu ukisikia watu wema basi ni Wazanzibar japo wapo wachache wenye chuki zao binafsi na wabara.

Nilitafutiwa kazi na marafki zangu wa kiislamu nikaanza kazi huko Bwejuu (hotel sitaitaja). Niliamua kurudi bara nikiwa tayari na mtaji wangu wa kuanzia biashara.

Mwezi uliopita nikiwa naangalia Aljazira na mke wangu niliona rubani wa Jordan akikamatwa na kundi la wanajeshi wa ISIL lakini nikajipa moyo kuwa watamuachia kwa vile ile ni kazi yake, pili ni ndugu yao (mwarabu), tatu ni muislamu mwenzao. Nimetoka dukani usiku huu na kukuta Breaking news Aljazeera wakiwa wamemuua kwa kumubanika kwa moto.

Mara ya mwisho nilimuonyesha mke wangu video kupitia youtube jinsi walivyomkamata. Mke wangu amelia kabisa kwa ukatili wa hawa jamaa zetu waarabu waislamu wa ISIL. Hakika sitawasahau waarabu wa ISIL.

We endelea na mapambano kaka, nchi yko kila siku watu wanapiga billions we unefatilia mambo ya dunia nyingine, kwani muislamu nwnzangu ukileta ujinga nikubebe kwa kuwa ni muislamu.... bullshit kwani dini ndo nini?
Wewe waache na dunia yao, wakata Benjamin Netanyau anapiga shule kule Pallestina na watoto wanakufa wewe na mkeo mlikuwa mnaangalia bongo muvi.. Mind your businez man
 
Mtu akiwa mkristo au wa dini yoyote akifanya mauaji au maovu kwa sababu au malengo yake binafsi hatuwezi kulaumu dini yake, mambo wanayofanya wamarekani na nchi nyingine za magharibi hayafanywi katika jina la ukristo bali kwa sababu na malengo yao ya kisiasa, hawasemi kwamba imani yao ya kikristo ndio inawatuma kufanya hivyo la hasha!

Na hata inapotokea mkristo au kikundi cha kikristo kinafanya maovu kwa kisingizio cha ukristo kamwe hutaona wakristo wakishabikia uovu huo kwa sababu wakristo wanalijua neno lao vizuri, ni nani umemsikia akimshabikia Joseph Kony wa LORD'S RESISTANCE ARMY ya Uganda!? pamoja na kwamba anataka nchi ya Uganda iongozwe kikristo kwa kufuata amri kumi za Mungu, ni wapi kwenye biblia imeandikwa hivyo kama sio uhuni na ushenzi wake!

Ila nashangaa sana baadhi ya waislam kama wewe ambao mnashabikia maovu yanaofanywa na makundi kama boko haram, al qaeda, isis n.k tena wanasema wanafanya katika jina la allah! halafu mnaona ni haki! sasa matokeo yake haya makundi yanaanza kuwadhuru na waislam wenzao, isis wanafanya hivyo, boko haram ndo usiseme wengi wanaodhurika ni waislam wenzao halafu unatetea upuuzi huu, ngoja yakukute ndipo utakapojuta!

Mimi siwezi kutetea uovu wa mkristo mwenzangu eti kwa sababu ni mkristo, never!
Na kuhusu anti-balaka na seleka kule central africa hebu soma vizuri ujue chanzo chake, kwa kifupi rais bozize(mkristo) alipinduliwa na kikundi cha kiislam cha seleka na kumsimika rais wao djotodia ambae aliwaahidi saudi arabia kuwa ata implement sharia law katika central africa na ikapelekea wakristo na waumini wa dini za asili kujiunga pamoja kutengeneza kundi lao la anti balaka ili kupinga nchi kutawaliwa kwa sharia law!hivyo kundi la anti balaka(anti-sword) sio kundi la kikristo only bali wapo na waumini wa dini za asili za kiafrika wengi tu!

Nimekusoma vizuri sana Mkuu,huyu Faiza Fox hakika ni mdini saana,kiukweli nimemfuatilia nakugundua hilo.
 
Back
Top Bottom