Chimunguru
JF-Expert Member
- May 3, 2009
- 10,679
- 4,382
Kiwembe Perma Sharp
Nimekumbuka sana miaka ya 80 wakati huo tunatumia sabuni za MBUNI,ILULA,BOBY SOAP,KODRAI.NA MAFUTA YA KUPAKAA YA LADY GUY,YU,SABUNI ZA KUOGEA ZA RUMI KUTOKA KIWANDANI TANGA.HII LEO VIWANDA HIVI HAVIPO TENA.TUJIKUMBUSHE WADAU WA MIAKA HIYO.
Hii ilikua ni shirika la umma. Ilikufa kifo cha mende kama akina Ganeral Tyre, ZZK Mbeya, Mwatex na ATC. Majengo yake (yaite magofu) bado yapo pale Iyunga, opposite na Malawi Cargo Centres.Wapi HISOAP Iyunga Mbeya...?
Duh. Savco imenikumbusha mbali sanaNakumbuka wadada wa enzi zile wakivaa magauni yaliitwa Read made na skuna, wanaume wanatokelezea na suruali Savco au Tokyo, chini raba aina ya Ndopa na juu shati na jacket zimeandikwa MBW (Bwana Mavi Wilayani)
......nimekumbuka mbuni na kodrai, hizo nyingine sikuziona. Labda useme punda na komesha,foma na omo hizi nimetumia.
Enzi zetu tunasoma MTC ndo ilikuwa njia yetu kwa gariHii ilikua ni shirika la umma. Ilikufa kifo cha mende kama akina Ganeral Tyre, ZZK Mbeya, Mwatex na ATC. Majengo yake (yaite magofu) bado yapo pale Iyunga, opposite na Malawi Cargo Centres.
Soda: Vimto
Sabuni: Rexona na Lifebuoy
Shati za shule: Shikibo
Sketi za shule: Nytil Jinja
Viatu: Globe master
Rais: Nyerere
Treni: (Dar-Mwanza, Kigoma-Dar, Tabora-Dar, Mpanda-Kaliua, Arusha-Dar, Arusha-Tanga, Tanga-Dar).
Bus: Railway, Tanganyika Bus, DMT,
Muziki: Mbaraka, Salum Abdalah
Waziri Jembe: Sokoine
Uchumi: 1 US $ = 7 Tshs
Hivi Revola ni ya miaka gani
Maskini Tanga,ilikuwa na viwanda vingi sana,mashamba makubwa ya mkonge,Railway,Bandari,vyote vimekufa.Tanga kunani?Nimekumbuka sana miaka ya 80 wakati huo tunatumia sabuni za MBUNI,ILULA,BOBY SOAP,KODRAI.NA MAFUTA YA KUPAKAA YA LADY GUY,YU,SABUNI ZA KUOGEA ZA RUMI KUTOKA KIWANDANI TANGA.HII LEO VIWANDA HIVI HAVIPO TENA.TUJIKUMBUSHE WADAU WA MIAKA HIYO.