Mnazikumbuka sabuni na mafuta haya?

Mnazikumbuka sabuni na mafuta haya?

Kwenye maduka ya kaya ulikuwa unajipatia pen iliyoitwa ELIMU kabla ya kuingia pen ya LASKA. Bila suluari ya don't touch my shoes na viatu komfuu disco ulikuwa hujalipatia. Ukikosa komfuu dunda na chachacha
 
Nimekumbuka sana miaka ya 80 wakati huo tunatumia sabuni za MBUNI,ILULA,BOBY SOAP,KODRAI.NA MAFUTA YA KUPAKAA YA LADY GUY,YU,SABUNI ZA KUOGEA ZA RUMI KUTOKA KIWANDANI TANGA.HII LEO VIWANDA HIVI HAVIPO TENA.TUJIKUMBUSHE WADAU WA MIAKA HIYO.

kwa wale wanaotoka kanda ya ziwa, kulikuwa na sabuni inaitwa magwanji, mafuta, mwalimu, rays, jua kali, mamisi, sabuni aina ya kwanga
 
Mi naimiss sana dawa ya meno ilikuwa ikiitwa bonamed, ilikuwa ina marash ya karafuu hivi.
 
Mkuu Duuh! wewe unapaswa kuitwa mama mkubwa na siyo mama mdogo! Umenikumbusha mbali sana hasa pale kwa soda ya VIMTO, na pale kwenye Uchumi! Uko vizuri mkuu.

Vimto ilikuwa tamu hadi unatamani kuongeza maji.
 
Kuna sabuni iliitwa mbunju,mashati ya Juliana,jeans aina ya savco, c.h.u.pi aina ya VIP ilikuwa inakatika na kupanda mpaka kifuani.Mafuta ya shanti ukijipaka halafu ukapita maeneo yenye nyuki lazima wakufuate.Ilimtokea rafiki yangu pale chang'ombe primary dar 1990
 
Lakuchumpa lakuparama aina ya Kawasaki na Benqi ukivaa hivyo viatu halafu mfukoni una shilingi tano wa kike wote lazima wakufuatefuate ili uwanunulie kacholi.Shule za zamani zilikuwa na raha yake.
 
kwa wale wanaotoka kanda ya ziwa, kulikuwa na sabuni inaitwa magwanji, mafuta, mwalimu, rays, jua kali, mamisi, sabuni aina ya kwanga

Eeehe bwana weee! Amagwanji bhwaana! sabuni hii ilikuwa inatokana na makapi ya mbegu za pamba wakati wa kukamua mafuta.
 
Umenikumbusha rexona. Ile harufu yake iko akilini kwangu na naihusisha na mauti. Kuna ndugu alilazwa hospitali kwenye private room na walikuwa wanamuogeshea hiyo. Mwaka 1992 hiyo, nikamuona mgonjwa nikaskia hiyo harufu halafu kesho yake akawa amefariki. Yaani nilikuwa nikisikia hiuo harufu nahisi niko mortuary.
Kabla ya hapo, kulikuwa pia na sabuni za Gardenia, mafuta ya mikebe yenye harufu nzuri sana yakiitwa Sudania, Yollanda, Sabuni za Life Boy, n.k.
 
Kwa wanafunzi waliokuwa dsm walikuwa wanapata mahitaji yao pale posta ya zamani SHIRIKA LA VIFAA VYA ELIMU.kwa bei poa.
 
Eeehe bwana weee! Amagwanji bhwaana! sabuni hii ilikuwa inatokana na makapi ya mbegu za pamba wakati wa kukamua mafuta.

Kwa familia za maisha ya kawaida chai walikuwa wanatumia sukari gulu.
 
Enzi hizo stand ya mabasi ya mikoani ilikuwa pale kisutu.moja ya mabasi maalufu lilikuwa LANG'ATA (dsm-arusha)
 
Back
Top Bottom