Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,472
- 12,889
- Thread starter
- #41
Mkuu basi vijana wote wa bara la afrika na uarabuni na asia ya kati ni watumwa kwa asilimia 97%.Binadamu tunaishi kwa kutegemeana Mungu ndo alivyo iumba dunia na hakuna atakaye weza kubadilisha.
Hao wazungu unao wasema na wao wanatumia tarakimu zilizo buniwa na waarabu yaani 0 to 9 kwenye elimu yao kama wangekuwa na akili nyingi wangebuni za kwao.
Alafu unacho takiwa kujua ni kuwa kila jamii hapa duniani ina mchango wake kwenye ukuaji wa teknolojia na sio wazungu tu, ukienda kwenye makampuni makubwa ya kiteknolojia duniani yana wataalamu kutoka jamii mchanganyiko duniani na sio wazungu tu.
Alafu hiyo hoja ya kusema sijui watu wanapenda kukimbilia Ulaya na Marekani mbona huwa ni hoja ya kipumbavu sana.
Kwani hakuna raia wa Marekani na Ulaya walioko kwenye nchi za watu wengine? Ya kwamba wao wana haki ya kwenda kuishi kwenye nchi za wengine ila sisi tukienda kwao tunaonekana tuna shida sana sio?
Hapa duniani kila binadamu ana haki ya kwenda sehemu yeyote kutokana na mahitaji yake la msingi afuate taratibu tu.
Hiyo dhana yenu ya kusema eti kila mtu hapa duniani anatamani kuishi Marekani ni dhana ya kipumbavu na kitumwa kwa sababu hapa duniani hakuna taifa lisilo kuwa na raia wa kigeni kwenye ardhi yake,
Mfano Tz ni nchi maskini ambayo haiwezi hata kuwahudumia raia wake lakini ina mamilioni ya raia wa kigeni wanao ishi hapa nchini wakiwemo hao raia wa Marekani na Ulaya.
Maana wote ndoto zao ni kuishi ilaya au marekani.