zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,314
- 40,068
Mkuu nashukuru kwa maarifa ingawa nimewahi soma hichi kitabu cha Yasheri lakini controversy inaanzia sehemu moja hapa...... Kuna source credible ya Flavius Josephus kwenye kitabu chake cha Antiquities of the jews anaandika kuwa Shem ndie alimuua Nimrod na kuugawa mwili wake vipande vipande ilihali Book of jasher inasema Esau ndio alimuua Nimrod na kumuibia vazi lake la maajabu.Hebu pitieni na hii wakuu (ZITTO JUNIOR NA HAMMAZ) kuhusu kifo Cha Nimrodi.
Shida inaanzia hapa Nimrod alizaliwa na cush mjukuu wa Nuhu lakini Esau ni kizazi cha 10 toka Nimrod azaliwe so unaweza ona hamna uhalisia sana wa Esau kumkuta nimrod akiwa hai maana sources nyingi zinadai nimrod alifariki akiwa na miaka 300+ ilihali gap kati ya Nimrod kuzaliwa mpaka Esau kuzaliwa ni miaka 400 ikimaanisha Esau akizaliwa Nimrod alikuwa ameshakufa!!!
Huu mkanganyiko unaweza fanya tuamini kuwa Nimrod original aliuawa na shem kwa sababu moja kuu..... Baada ya Nimrod kuuawa alimuacha mkewe semiramis akiwa na mimba na alipozaa yule mtoto (Tammuz) ambaye sherehe yake ni 25 December..... Aliitwa NIMROD pia na wafalme wote wa huko Erech na Akkad (mesopotamia) waliotokana na damu ya Nimrod original walipotawala wote waliendelea kuitwa jina la Nimrod hivyo inawezekana Esau alikuja kumuua mmoja wa hawa kina NIMROD warithi ila original Nimrod probability kubwa ni kwamba aliuawa na shem na hii inaleta maana kidogo maana nimrod ni sawa na mjukuu kwa Shem tofauti kabisa na gap la miaka kati ya Nimrod na Esau ambalo haliko na uhalisia kabisa
Hayo ndio maoni yangu kwa upande wa source za wayahudi yaani Jasher na Flavius Josephus.