Mnara wa Babeli na historia ya kutisha

Mnara wa Babeli na historia ya kutisha

Hizi chai mbana hazina vitafunwa mnatupa chai ya mkono moja
Haahaaa sio chai mkuu ni vitabu vyao watu wa mashariki ya kale vinadai hicho kitu kma ambavyo na ssi tuna stori za miujiza ya Ng'hwanamalundi ama Hunku Bin Hunuk n.k

Kuhusu Uwepo wa mnara wa Babeli ushahidi upo huko Iraq ya ssa madude hayo yaliitwa El Ziggurat.

Mfalme Nimrod kihistoria ya kisayansi anafahamika kma Enmmekar.

Utawala wake ulikua sumeria ya kale kwa maeneo tajwa kma Ur,uz,Akkad,Eridu n.k

Kagoogle Sumerian kings Tablet iliopo kwenye museum ufaransa alafu urudi kusema kma kuna chai juu ya hii simulizi ya Nimrod/Tower of Babel.
 
Amna cha mnara mkubwa kama nini sijui pale kuna mnara wa kawaida tu na upo mpka leo waitwa zyguratus kama skosei,sio mnara siju ulokuwa mrefu hapana.

Sent from my TECNO-J5 using Tapatalk
 
Historia ya mnara wa Babeli inaelezwa kwa undani kwenye biblia katika kitabu cha Mwanzo 11 katika mistari michache tu. Hii ni stori fupi tu ya mnara wa Babeli unaweza kusoma kwa undani katika mistari au maandiko hapo chini ili kujua zaidi juu ya Babeli na maana yake katika biblia.

Kizazi cha Nuhu kilikuwa kinaishi katika Mesopotamia ndani ya Babeli na kuchagua kuishi katika nchi ya Shina. Kizazi chao kikazidi kukuwa huku wakiwa wanaongea lugha moja wote. Muda ulivyozidi kwenda watu wa Babeli wakaaamua kujenga mnara mkubwa kama alama ya nchi yao na kujionesha kwa mataifa mengine ukuu wa nchi yao ya Babeli. Watu wa Babeli walitaka kujenga mnara ambao unaweza kufika mpaka mbinguni, ili wawe kama mungu na wasimuhitaji tena mungu kwenye maisha yao ndipo hapo wakaanza ujenzi wa mnara huo na kuuita mnara wa Babeli.

Babeli ni mji maarufu sana ndani ya Mesopotamia ambako kwa miaka ya sasa mji huu unapatikana maili 59 Iraq kusini magharibi mwa Baghdad ambao ni mji mkuu wa Iraq.

Jina hili linatokana na lugha ya ki-akkadian (Bav-ill) lenye maana mlango wa mungu 'Gate of God'.

Historia ya biblia inatuonesha maeneo mbalimbali ya mabadiliko ya dunia mfano Uumbaji, anguko na gharika la NUHU. Kwa kufuatilia mfululizo mzuri wa matukio ya kibiblia ambayo yalishawahi kutokea na ni ya kweli tunaweza tukaelewa asili ya maisha yetu na kuachana na mambo ya EVOLUTION OF MAN. Babeli ndiyo ulikuwa mwanzo wa mgawanyo wa mataifa na mkanganyko wa lugha ulimwenguni.

Baada ya Nuhu na familia yake kushuka kwenye safina katika milima ya Arafati, Mungu aliwaagiza waende kuzaana na kutawanyika mbele ya uso wa nchi. (\mwanzo9:1) , wao wakaamua kuishi Babeli nchi iliyokuwa chini ya Nimrodi (Mpinga kristo) ambapo hapo ndipo ujenzi wa mnara wa Babeli ulipoanzia. (Baadae tutaona ni kwanini Nimrodi alikuwa mpinga kristo). Mnara huu wa Babeli ndio uliokuja kuwa makutano ya kuabudia miungu na sio Mungu muumbaji.

KWANINI MUNGU ALIAMUA KUANGAMIZA BABELI?

Katika utawala wa Nimrodi, miaka mingi baada ya uumbaji kukamilika, Ndipo ujenzi wa mnara wa Babeli ulipoanza. Ikumbukwe mpaka muda huu nchi ilikuwa sehemu moja. Baada ya gharika kutokea na Nuhu na familia yake kusalimika, ulimwengu mzima ulikuwa sehemu moja kwa sababu dunia/nchi haikuwa na watu wengi na ndio maana Mungu alimwagiza Nuhu baada ya gharika kuisha kuwa waende wakaijaze nchi.

Hapo ndipo Nimrodi na wenzake walipoamua kujenga mnara mkubwa sana kwa malengo makubwa mawili.

1. Kujitafutia jina wao wenyewe juu ya nchi
2. Kufika mbinguni

Nimrodi akaanza kujenga mnara ambao ulikuwa mkubwa sana mpaka hapo mungu aliposhuka chini na kuamua kuuangamiza huo mnara kwa kuwachafulia lugha zao.

Mungu hakuiangamiza Babeli kwa sababu aliwaogopa wanadamu au labda aliona kuwa wanadamu wanaweza kufika mbinguni, hapana. Dunia sasa hivi ina maghorofa makubwa sana hata tunaona ndege zikienda hewani lakini hakuna ambayo imeshawahi kufika mbinguni ambako mungu yupo, kwa hiyo mungu hakuwahofia wanadamu kabisa ila kulikuwa na sababu za msingi zilizofanya mungu afanye vile.

Mungu hakupendezwa na kiburi na kutokutii kwa wanadamu. Ikumbukwe kuwa dhambii hii hii ya kiburi ndiyo kwanza ilimuangusha shetani kutoka mbingu mpaka nchi, pia dhambi hiyo hiyo ilimuangusha Adamu ndani ya Edeni na dhambi hiyo hiyo iliangusha Babeli kuu ya Nemrodi.

Watu wa Babeli walitaka wakae sehemu moja kinyume na matakwa ya mungu. Ikumbukwe mungu alimuagiza Nuhu waende wakatawanyike mbele ya uso wa nchi, lakini wao wakaamua kufanya kinyume na amri ya mungu ili wajitwalie utukufu wao wenyewe (KIBURI).

Dhambi kubwa iliyofanya mungu awachafulie usemi wao ilikuwa "Na tujifanyie jina wenyewe", Je wakati huo kulikuwa nchi ambayo walikuwa wanataka kushindana nayo? Je walitaka nani awasifu? Kulikuwa na nchi ya jirani? Ila walikuwa wanashindana na Mungu mwenyewe.

Nimrodi alikuwa na makundi matatu
1. Kundi la kwanza lilikuwa kwa ajiri ya kumuua mungu
2. Kundi la pili walikuwa na kazi ya kutengeneza mishalie kwa ajili ya kumuua mungu
3. Kundi la mwisho kwa ajiri ya ujenzi wa Babeli
Tembelea (skiba 2012) kwa mapitia .

Hapo ndipo utakapogundua kuwa Nimrodi alitaka kwenda kukaa kwenye kiti cha enzi cha mungu.

Hayo yote ndiyo yaliyomchukiza mungu na kuamua kuwachafulia usemi wao ili wapate kujifunza na kuwalazimisha kugawanyika mbele ya uso wa mungu

HII INAENDA SAMBAMBA KABISA NA ANGUKO LA SHETANI KWA KUTAKA KUWA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MUNGU

View attachment 757831

Makala safi sana hii.
Sasa na Wale Wanyama waliobebwa kwenye Safina ya Nuhu waliishia wapi?
Na baada ya mnara wa Babeli kuangushwa Nuhu alienda wapi?
Na je iliwezekana vipi Nuhu aliyekombolewa na Mungu aje aungane na watu wanaotaka kumuua Mungu ?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba Nimrod alikuwa ni mpinga kristo huu ni uongo wa kiwango cha aina yake,wakati Nimrodi alikuwepo maelfu ya miaka kabla ya kristo.

Pia hakuna ushahidi wa huo mnara wa babel,
Nimrod alipata kuwa mtawala huko Akkadian,kama vile tu akina Hammurabi etc,
cha ajabu anatokea kwenye bible kama sijui mtoto wa mtu anaeitwa caanan,

wakati ukweli ni kuwa caanan ilikuwa ni jina la eneo kama mfano afika mashariki,sahara etc,
how came caanan linageuka linakuwa eti jina la mtoto wa Adam?

Yesu alisema ukweli kuwa kalamu ya waandishi imeifanya torati kuwa ni uongo,

na mfano ni pale walipochukua habari za mfalme Shalmaneser wa Asyria na kubuni mfalme suleman wakitumia inspiring toka kwa mfalme wa Asyria
Una ubishi wa kizamani kweli. kWamba hakuna mtu anaitwa caanan
Kwahiyo unadhani Yesu hakuwepo kabla ya Adam?
Tulia ujifunze
 
Wakuu, mimi nilijua gharika iliangamiza watu wote duniani isipokua Nuhu na wenzie waliokua kwenye safina.

Sasa huyu Nimrod na wenzake walitokea wapi?

Pia mleta mada anasema Nimrod na wenzie walitaka kujenga mnara mrefu ili wajifanyie jina kwa majirani zao.

Hao majirani zao nao walitoka wapi?

Je, ni kweli kwamba gharika haikuangamiza dunia nzima?
Tahadhari usije ukaambiwa una mapepo bure. Kuamini aina hizo za hekaya huitaji maantiki inatakiwa uamini tu
 
Screenshot_20200419-184107.png
 
Na lugha zilizochanganywa zilikuwa za kiroho pia?
Mkuu nani kasema Mungu anaishi mawinguni?? Walijenga mnara wa kiroho sio kimwili ni sawa na mtu afanye tambiko bagamoyo la kumfanya ajisafirishe hadi marekani bila kutumia ndege wala usafiri wowote ndio walivofanya kina nimrod, semiramis na mardon walijenga GETI linalowafikisha mbinguni ambalo walifanikiwa ila walisambaratishwa kabla ya kuiona mbingu yenyewe
 
Amna cha mnara mkubwa kama nini sijui pale kuna mnara wa kawaida tu na upo mpka leo waitwa zyguratus kama skosei,sio mnara siju ulokuwa mrefu hapana.

Sent from my TECNO-J5 using Tapatalk
Kwa watu wazamani,hata mnara uwe na urefu wa ghorofa tatu,hiyo Ni habari kubwa Sana.kumbuka Hawa watu waliamini mungu wao,yaani anaishi milimani,,kwahiyo kujenga nyuma ilioenda juu ilikuwa Ni Kama kutaka kushindana na mungu wao na hivyo ilikua Ni kufuru
 
Na lugha zilizochanganywa zilikuwa za kiroho pia?
Lugha zilikuwa kabla ya ishu ya mnara,japo idadi ya watu ilikuwa bado ndogo,kwa mfano,maeneo ya ulaya hayakuwa yameanza kukaliwa na ilukuwa Ni barafu tupu Kama ilivyo siberia
 
Na lugha zilizochanganywa zilikuwa za kiroho pia?
Mkuu ningeomba ufahamu leo biblia kwa kiasi kikubwa ni figurative yaani inatumia mafumbo.

Lugha sio lazima iwe hzi lugha za kinyakyusa na kiingereza.... Ila pia inaweza kuwa na maana ya ''kuwa na lengo moja'' hivyo kuchafua lugha inawezekana ni kuwapa tofauti ya mitazamo juu ya ujenzi wa mnara.

Sababu hata wakoloni walikuja Africa wakiwa hawajui lugha zetu na sisi hatujui zao lakini mbona waliweza kuleta dini zao na hta tukafanya biashara?

So sidhani eti mnyakyusa na mzaramo kwa kuwa hawaelewani lugha hawawezi kujenga nyumba. Sababu unaweza tumia hata lugha ya ishara na alama kupiga kazi so nakupa tu mtazamo wa upande wa pili.

Kwahiyo kwa mtazamo wa figurative language twaweza sema, walitofautiana mtazamo wao juu ya matambiko/ujenzi wa mnara lakini sio necessarily kinyakyusa na kizaramo!!
 
Mimi kwa upande wangu bado huwa naitafakari Sana babeli.Nimesoma post nyingi ili nipate angalau majibu na nyongeza ya fikra zangu na kwa sehemu nimefurahia.Japo lengo la binadamu lilikuwa kujenga mnara na uwe kumbukumbu bado huwa najiuliza lile wazo lilitoka kwa Nani?

Je yule binadamu alikuwa bado anaexist kwenye realm mbili Kama alivyokuwa Adam?
Maana huu mnara mpaka ukachukua attention ya Mungu itakuwa ulikuwa na mahusiano na ulimwengu wa roho.?

Zaidi Sana naiona babeli Kama lango likitumiwa na Mungu kupitishia lugha iliochafuka na kutoelewana,yamkini na binadamu na huyo mwanaharamu shetani walitumia pia Hilo lango,,sheitwan akimtumia binadamu kwa agenda zake binafsi kujenga mnara .


Sent using Jamii Forums mobile app
 
The book of jasher chapter 9

35 And the Lord smote the three divisions that were there, and he punished them according to their works and designs; those who said, We will ascend to heaven and serve our gods, became like apes and elephants;

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom