Ahsante kwa mawazo yako murua ila kuna baadhi ya mambo tutatofautiana kuhusu Nimrud ibn Kanan. Huyu jamaa aliishi kipindi cha nabii Ibrahim a.s alikuwa ni mfalme mwenye ufalme usiokuwa na kifani kwa nyakati zake. Alifikia pahala akaona anayoyafanya Mungu basi naye anayaweza na hii yote ni kutokana na ujabali wa ufalme wake. Ibrahim a.s alimhabarisha kuhusu Mungu na utukufu wake akamwambia Mimi Ibrahim Mungu wangu anahuisha na kufisha. Nimrudi akaona mbona hill ni jambo dogo tu, akaamuru watu 2 waletwe mbele yake wakaletwa akasema mmoja auliwe na mwengine aachwe hai. Askari wakatii amri yake kisha akamgeukia Ibrahim a.s na kumwambia anayoyafanya Mungu nami nayafanya vilevile, huyu nimemfisha huyu nimempa uhai.
Nabii Ibrahim a.s akatabasamu akamwambia Mungu wangu analitoa Jua mashariki na kulipeleka magharibi. Nimrud hiyo ilimchukiza sana kwamba ameshindwa katika hilo mbele ya watu wake. Akaamuru jeshi lake kubwa waandae mishale halafu waielekeze juu Mbinguni huku akimwambia Mungu Ibrahim, natangaza challenge kati yangu na wewe Mungu wa ibrahim. Kilichompata ni maafa