zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 24,265
- 39,869
1. Kuhusu mishale ya Nimrod ni kwamba haikutoka dunia hadi mbinguni kupitia space hapana geti lilifunguka kwahiyo ilikuwa mishale inatoka directly kwenye mnara kwenda mbinguni maana walishakuwa wameivuta karibu kama sniper vile akitaka kushoot!!! Hivyo waliipunguza distance ya mbingu hadi duniani kiasi kwamba hata mshale unaosafiri kwa spidi ya kuongea kwa Lowassa bado ilifika haraka tu maana mbingu ilishavutwa mpaka mita chache tu kutoka kwenye mnaraIla mimi bado najiuliza huko mbinguni ni wapi ki location yaani? Ni huko tunapotazama jua ama? Au ni nje ya ulimwenguu huu labda..
Maana Yesu Kristo alipokua akipaa kwenda mbinguni alipaa kwenda juu uelekeo wa jua kwa mujibu wa maandiko. Lakini zama hizi sayansi imeweza kutoka nje ya dunia na kuona umbali wa ma bilion ya km mbele, sasa hio mishale ya nimrodi ilirushwa kwa style ya namna gani mpaka kufika huko aliko Mungu?
Sambamba na hilo ikiwa wana sayansi wameweza kuona umbali ambao ukitaka kwenda itakuchukua miaka bilion kufika tena kwa speed ya mwanga, na mpaka hapo mbingu hawajaiona huenda iko mbele zaidi. Sasa Yesu aliepaa tuchukue alikua na speed ya mwanga mara 1000 huenda mpaka leo hajafika bado, zingatia mwanga husafiri km 300000 kwa sekunde?
2.Kuhusu location ya mbingu or at least sehemu walioenda waliotenda mema baada ya kufa zamani ilikuwepo duniani physically ila baada ya Yesu kwenda kuzimu na kuhubiria watu.... Alifufuka nao na kupaa nao kwenda huko mbingu ya Saba ambayo ipo somewhere nje ya galaxy yetu sababu nakumbuka kwenye Book of Enoch (watchers) pamoja na book of giants kuna muda Nabii Enoch alikuwa akitoka mbinguni kurudi duniani alikuwa anapishana na Malaika aliotupwa semyaza na kumuonya asipae karibu sana na jua meaning mbingu ilikuwa somewhere in the galaxies ila mbele kidogo na dunia/galaxy yetu.
3.Ushahidi mwingine Zamani hata wachawi walikuwa na nguvu ya kumuita mtu aliyekufa na kwenda mbinguni arudi duniani kuongea na ndugu au yeyote aliyemuhitaji ila kwa sasa sababu hawapo duniani tena hakuna mganga ana huo ubavu wa kurudisha roho ya mtakatifu duniani.... Ila zamani waliweza sababu mbingu ilikuwa hapahapa duniani
So conclusion yangu ni kwamba mbingu ipo kiroho zaidi ila haipo duniani iko somewhere nje ya milkway galaxy maana dunia biblia inasema utakunjwa na kutupwa kwenye moto sasa sioni vp mbingu iwepo duniani ilihali atakuja kuiteketeza kwa moto huko mbeleni..... Kuhusu speed ya kufika nafkiri immortal beings wana uwezo wa kusafiri kuliko hta spidi ya mwanga au at least kutengeneza GETI ili wapunguze distance ya hapa na mbingu labda wajuvi watusaidie
Kudo900 Mshana Jr impongo Mchawi Mkuu Palantir Malcom Lumumba hearly
Elungata Mchawi Mkuu