Mnaotaka na kulilia jeshi lichukue nchi hamjitambui

Hapo utakuwa umeiokoa CCM pakubwa saaana. Watajipanga upya na kurudi kivingine huku wakiepuka njia zote za kuwawajibisha kwa waliyofanya.

CCM ili ipotee mazima inabidi ishindwe katika sanduku la kura na ikataliwe na wananchi kwa njia hiyo. CCM haijawa designed kuwa wapinzani. Hawataweza kudumu katika hali hiyo hasa kama mifumo ya kiutawala, kisheria na kiuchaguzi ikibadilishwa.
Wanyang'anywe na mali zote walizorithi kutoka TANU
 
Screenshot_20251005-123234.jpg
Screenshot_20251005-123251.jpg
 
Nakuelewa sana.

Kuna Watanzania wengi hawapingi mambo kwa principle.

Wanapinga kuumizwa wao tu.

Hawapingi ubaguzi kwa principle kwamba wanapinga ubaguzi. Wanapinga ubaguzi wanapobaguliwa wao tu.

Wao wakipata nafasi ya kuwabagua wenzao kwa maslahi yao, wanawabagua tu bila kuona ubaya wa ubaguzi huo.

Mfano, leo hapa JF nimekutana na mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa CCM na watawala. Anamshabikia Kapteni Tesha. Nikamwambia mwanaharakati wa demokrasia kumshabikia Kapteni Tesha, mwanajeshi anayechochea mapinduzi ya kijeshi, anayemsifia na kumlilia Magufuli, ni contradiction.

Mwanaharakati huyo hakupenda nilivyomwambia, akaniambia wewe ni mkimbizi tu, huna moral authority ya kutupangia mambo ya nchi yetu.

Huyu mburula haelewi hata wakimbizi wana haki, haelewi kuwa ubaguzi anaonifanyia mimi anayeniita mkimbizi ndio huo huo anaoupinga CCM inapomfanyia yeye kwa kumuita mwanaharakati.

Kimsingi hapingi ubaguzi. Angepinga ubaguzi asingenibagua mimi.

Anapinga kubaguliwa yeye tu, lakini yeye kubagua wengine walio na mawazo tofauti naye anaona sawa.

Kuna Watanzania wengi wako hivyo.

Hawa watu wanaoshabikia jeshi kuchukua nchi, kimsingi si wanaharakati wa demokrasia, ni watu ambao hawapendi utawala uliopo na ukija utawala wanaoupenda hata ujiwa wa kijeshi watafurahi tu.
Unajua kuna wakati raia wanakuwa hawana machaguo mengi kwa hiyo kinachobaki ni kuchagua lesser evil tu. Chukulia mfano wa yaliyotokea Misri ambapo raia waliandamana mpaka wakafanikiwa kumuondoa dikteta wa muda mrefu Hosni Mubarak lakini mwishowe kupitia uchaguzi kwa sababu ya siasa zilizovurugwa sana na Mubarak wakaishia kuwa na Mohamed Morsi kama rais ambaye alikuwa mhafidhina na mtu wa mrengo mkali wa kidini na kupelekea kuendelea maandamano makubwa yasiyoisha. Hapo sasa ndipo General Al-Sisi anapoingia na kutwaa madaraka na kuonekana kama mwokozi wao kuzuia taifa la Misri lisiangamie na wengi wao wakapoa japo kuna walioendelea kupinga lakini hakukuwa na namna bora tena zaidi ya hiyo kuokoa hali japo ilikuwa na mapungufu makubwa kidemokrasia lakini kulikuwa na uhafadhali kutoka Mubarak na Morsi.
 
Kwa hiyo raia wanasema bora Magufuli kuliko Samia siyo?

Maana wamemshangilia sana yule Kapteni Tesha, na Kapteni Tesha hasema anampenda sana Magufuli, anamlilia sana Magufuli.
 
Wewe mpaka sasa huelewei kwa nini raia wanasema bora jiwe kuliko huyo mama??
Mimi imenichukua muda kuelewa hili jambo/contradiction lakini kadri muda ulivyoendelea nimeweza kuelewa sababu ni zipi na nimeshakubaliana na huo uhalisia wa hali halisi.
 
Kuna nyakati kweli mnakunjana mashati kwa kushindwa kuelewana na kukubaliana ila hiyo ni bora kuliko "sauti ya mmoja ndiyo amri".
Obama ni mzungumzaji/mjenga hoja mzuri; lakini bado haisaidii kitu. Angalia chama chake kilikofikia sasa!

Hapana. binafsi sishabikii "'amri za mtu mmoja'", bila ya ushiriki wa maauzi ya wengi katika swala lolote. Ni muhimu kabisa kulibainisha hili na kuonyesha tofauti iliyopo.

Ngoja nitumie mfano wa aina ya viongozi tuliokwisha shuhudia staili ya uongozi wao hapa kwetu.:
Tukianza na Mwalimu Nyerere, sikumbuki mfano wowote wa yeye kutoa "amri" ya yeye pekee juu ya swala zito la nchi bila ya kushikisha vikao vya chama kufanya maamuzi na hata kuliwahi kuwepo na ushirikishwaji wa vikao vya chini kabisa vijijini kabla ya utekelezaji wa maswala husika.

Mara nyingi nasita kutumia mfano wa Pombe Magufuli, lakini sina mfano wa karibu zaidi wa kuonyesha tofauti yake katika maamuzi ya "mtu mmoja" (amri ya mtu mmoja kama ulivyo sema). Na swala ninaloweza kuweka kama mfano ni wakati ule wa UVIKO.

Nilitaja mfano wa China; na hata Vietnam; ambako kuna vyama vya kikomunist vinavyo tawala nchi hizo. Hata huko hakuna maamuzi ya "amri ya mtu mmoja". Ni vikao vya chama vinavyo amua

Hapa kwetu sasa hivi, chini ya Samia. Wanaotuamria ni GENGE kupitia kwa Samia. Mifano ipo mingi sana.

Demokrasia ni nzuri; hasa inapohusu kuchagua viongozi kwa njia zilizo wazi na Haki, ili viongozi hao wakawawasilishie wananchi wao maoni na matakwa yao katika mhimili wa Bunge. Hapa kwetu sasa hivi ni aibu kubwa kusema tunalo Bunge.

Ngoja nimalize kwa kurudi kule kwenye mifano ya viongozi wetu hapa hapa Tanzania. Na ninarudi kwa mfano niliosema ni mbovu kiuhalisia; wa Pombe Magufuli.

Maamuzi ya mtu mmoja ambayo yanafanywa kwa nia thabiti kwa maslahi ya wananchi, na yakitekelezwa kwa amri thabiti; huleta tofauti kubwa sana. Lile bwawa la umeme kule Rufiji, wakati huu wala tusingekuwa tunaliwazia kabisa. Ule ujenzi wa reli ya SGR, sijui tungekuwa tumefikia wapi. Serikali ingekuwa bado imeganda Dar es Salaam; n.k., n.k..
Maana yangu hapa ni kwamba, katika hali yetu ya kimaendeleo tulipo sasa; kuna uwakati kuwepo na ulazima wa kuwa na kiongozi mwenye maamuzi magumu.

Ukiwatazama vizuri wenzetu; kama vile Korea Kusini, Taiwani. Singapore; hawa wote hawakufikishwa walipo kutokana na "demokrasia" zao kuwa bora. Walikuwa kwenye u-dikteta walipokuwa wakijijenga kuja kufikia walipo sasa.
Mwisho, mwisho...; tunachohitaji Tanzania ni viongozi wanaoghuswa kwa karibu sana na hali duni za wananchi wao na kuwa na uwezo wa kufanya maamuzi ya kuibadilisha hali hiyo katika muda mfupi iwezekanavyo. Sasa sijui kama ni "demokrasia" ndiyo itatufanya tuwapate hawa au vipi; SIJUI!
 
Wewe mpaka sasa huelewei kwa nini raia wanasema bora jiwe kuliko huyo mama??
Mimi imenichukua muda kuelewa hili jambo/contradiction lakini kadri muda ulivyoendelea nimeweza kuelewa sababu ni zipi na nimeshakubaliana na huo uhalisia wa hali halisi.
Kuna mambo mengi.

I am going to state some unpopular observations.

Please note, simtetei Samia. Samia ana mabaya mengi sana, kama aliyokuwa nayo Magufuli.

Naelezea tu kwa nini watu wanaona afadhali Magufuli kuliko Samia.

Nimegundua Watanzania wana mfumodume sana.

Watu wengi wanamchukia zaidi Samia kwa mambo yaleyale aliyoyafanya Jiwe kwa sababu Samia ni mwanamke.

Pia Samia hajui kuleta figisu kibongobongo kwa show za kibabe complicated kama Magufuli. Magufuli alikuwa anaweza kuwa kakosea yeye lakini akaku gaslight wewe mpaka ukajiona wewe ndiye umekosea. Unambana kumwambia habari za kikatiba, halafu yeye anakwambia mihimili yote iko sawa lakini mmoja umechimbiwa chini zaidi. Samia hawezi show hizo.

Pia Magufuki alijua kuwauzia "watu wanyonge" story fake kwamba anawapigania. Kuanzia kwenye makinika na figisu za migodi mpaka kwenye kutunga sheria ya kulinda maliasili (to his credit, kwenye sheria kulikuwa na kitu cha msingi hapo).

Samia reversed that kwenye kuuza bandari. So at least on this one point kuna sababu ya msingi kabisa ya kuona Magufuli was better. But it is mainly a PR issue, not substance.

Pia, Uzanzibari.

Habari za Watanganyika kutawaliwa na Wazanzibari. Habari za Waarabu kuuziwa bandari, Wazanzibari kufanya kazi bara lakini Watanganyika kutofanya kazi Zanzibar, hazimsaidii Samia.

Pia kuna angle ya udini. Samia kuonekana anafungia makanisa haimsaidii kwa Wakristo wengi ambao hata hawajali sana siasa lakini ukiwaingilia kwenye dini wanakuja mbogo.

Pia, Samia kawa disappoint watu wengi. Alivyoanza kuruhusu mikutano ya siasa, watu wengi waliona Samia anakuja kubadilisha pale Jiwe alipoharibu. Alipokuja kujionesha kuwa ni walewale tu, hata 4Rs zake zikaonekana magumashi. Lissu kafungwa kisiasa na haachiwi, nitandao inafungwa mpaka JF tunaingia kwa VPN, watu wengine wakamchukia kuliko Jiwe kwa sababu walikuwa na matumaini naye makubwa sana. Mtu ukiwa na matumaini naye makubwa akaku let down unaweza kumchukia sana.

Na hii habari ya kuweka matumaini kwa mtu emotionally bila ya kuwa na nuance ni tabia inayojirudia sana kwa Watanzania wengi.

Walifanya hivyo kwa Mkapa, kwa Kikwete, kwa Magufuli na Samia. Wote hao wakawa disappoint.

Na sasa hivi Watanzania wanarudia habari hizohizo kwa Gwajima, kwa Polepole, kwa Kapteni Tesha. Kwa jeshi.

Watu tunaoangalia historia tunaona hii pattern ya kuweka matumaini kwa watu, kihisia tu, bila strategy, bila kuweka misingi ya kitaasisi, ya kuwapa nguvu watu kidemokrasia, ni hatari.

Watanzania wengi wanapenda sana shortcuts za kubadili mambo kwa haraka bila kufanya kazi kubwa ya kubadili jamii na kupata mageuzi ya kifikra ya kudumu na yenye msingi mzuri.

Ndiyo maana wengine tukionesha hizi contradictions na kusisitiza mageuzi ya kweli, ya kitaasisi, ya kijamii, yasiyotegea watu wachache au hata mtu mmoja, mara nyingi tunakuwa kama hatueleweki, tunaonekana tuko out of touch, tunaonekana watu wa diaspora tu wakimbizi.

Haya mambo ya msingi hatuwezi kukwepa kuyafanyia kazi.

Otherwise tutazunguka kqenye mashairi ya Linton Johnson Kwesi katika "Di Eagle an' Di Bear".

"Dictators get dethroned
Now clown are quickly found".

Ndiyo hiyo habari uliyosema ya kutoka kwa Mubarak mpaka Al-Sisi Misri.
 
Pia Magufuki alijua kuwauzia "watu wanyonge" story fake kwamba anawapigania. Kuanzia kwenye makinika na figisu za migodi mpaka kwenye kutunga sheria ya kulinda maliasili (to his crwdit, kwenye sheria kulikuwa nankitu cha msingi hapo).

Samia reversed that kwenye kuuza bandari. So at least on this one point kuna sababu ya msingi kabisa ya kuona Magufuli was better. But it is mainly a PR issue, not substance.

Pia, Uzanzibari.

Habari za Watanganyika kutawaliwa na Wazanzibari. Habari za Waarabu kuuziwa bandari, Wazanzibari kufanya kazi bara lakini Watanganyika kutofanya kazi Zanzibar, hazimsaidii Samia.

Pia kuna angle ya udini. Samia kuonekana anafungia makanisa haimsaidii kwa Wakristo wengi ambao hata hawajali sana siasa lakini ukiwaingilia kwenye dini wanakuja mbogo.

Pia, Samia kawa disappoint watu wengi. Alivyoanza kuruhusu mikutano ya siasa, watu wengi waliona Samia anakuja kubadilisha pale Jiwe alipoharibu. Alipokuja kujionesha kuwa ni walewale tu, hata 4Rs zake zikaonekana magumashi. Lissu kafungwa kisiasa na haachiwi, nitandao inafungwa mpaka JF tunaingia kwa VPN, watu wengine wakamchukia kuliko Jiwe kwa sababu walikuwa na matumaini naye makubwa sana. Mtu ukiwa na matumaini naye makubwa akaku let down unaweza kumchukia sana.

Na hii habari ya kuweka matumaini kwa mtu emotionally bila ya kuwa na nuance ni tabia inayojirudia sana kwa Watanzania wengi.

Walifanya hivyo kwa Mkapa, kwa Kikwete, kwa Magufuli na Samia. Wote hao wakawa disappoint.

Na sasa hivi Watanzania wanarudia habari hizohizo kwa Gwajima, kwa Polepole, kwa Kapteni Tesha. Kwa jeshi.

Watu tunaoangalia historia tunaona hii pattern ya kuweka matumaini kwa watu, kihisia tu, bila strategy, bila kuweka misingi ya kitaasisi, ya kuwapa nguvu watu kidemokrasia, ni hatari.

Watanzania wengi wanapenda sana shortcuts za kubadili mambo kwa haraka bila kufanya kazi kubwa ya kubadili jamii na kupata mageuzi ya kifikra ya kudumu na yenye msingi mzuri.

Ndiyo maana wengine tukionesha hizi contradictions na kusisitiza mageuzi ya kweli, ya kitaasisi, ya kijamii, yasiyotegea watu wachache au hata mtu mmoja, mara nyingi tunakuwa kama hatueleweki, tunaonekana tuko out of touch, tunaonekana watu wa diaspora tu wakimbizi.

Haya mambo ya msingi hatuwezi kukwepa kuyafanyia kazi.

Otherwise tutazunguka kqenye mashairi ya Linton Johnson Kwesi katika "Di Eagle an' Di Bear".

"Dictators get dethroned
Now clown are quickly found".

Ndiyo hiyo habari uliyosema ya kutoka kwa Mubarak mpaka Al-Sisi Misri.
Karibia yote uliyoyaandika hapa yanaweza kuwa sahihi kasoro machache kama hayo ya kwamba Tanzania kuna mfumo dume, show za kibabe na jiwe kuwauzia wanyonge story fake za kuwapigania.

Tanzania mfumo dume umepungua sana na ushahidi wa kutosha upo wazi. Nakuhakishia kama huyu mama angeweka demokrasia ya kweli angependwa na wengi sana na angechukiwa na wahafidhina wachache wa chama chake na wanamtandao pekee ambao ni wachache sana bila kujali uanamke wake, show au story za wanyonge.

Kitu kingine unachopaswa kujua na kwa kuongezea ni kwamba huyu mama ni kama amepitiliza kwenye mambo hasi zaidi ya jiwe. Gharama ya maisha imeongezeka sana, huduma na uwajibikaji katika ofisi nyingi za umma zimedorora sana(ile nidhamu japo ilikuwa ya uoga ya enzi za jiwe imepotea kabisa), hali ya miundombinu sehemu nyingi barabara ni mbovu mno kuna barabara nyingi wakandarasi wanachimbuachumbua tu ila hakuna cha maana wanchofanya, maji ni shida hata katika mkoa kama Mwanza, nepotism imepindukia, utekeji na watu kupotea inawezekana ikawa imezidi kipindi cha jiwe ila tofauti kipindi cha jiwe wengi waliokuwa wanatekwa walikuwa maarufu kwa hiyo kelele zilikuwa zinakuwa kubwa zaidi na pia tukio la Lissu kupigwa risasi ndio likafunika zaidi, kipindi cha huyu mama wapinzani wawili wakubwa wa serikali wamepewa makosa ya ugaidi na uhaini, chama kikubwa zaidi cha upinzani kimeondolewa kabisa katika uchaguzi mkuu.

Juu ya haya yote kuna ufisadi mkubwa na wanaofanya wanajiachia hadharani kwa maisha ya anasa na ufahari, hili linawekera watu zaidi, ni kama matusi . Huenda hata wakati wa jiwe kulikuwa na ufisadi ila ulikuwa wa kujificha na mgumu kidogo kuulezea.
 
Kuna mambo mengi.

I am going to state some unpopular observations.

Please note, simtetei Samia. Samia ana mabaya mengi sana, kama aliyokuwa nayo Magufuli.

Naelezea tu kwa nini watu wanaona afadhali Magufuli kuliko Samia.

Nimegundua Watanzania wana mfumodume sana.

Watu wengi wanamchukia zaidi Samia kwa mambo yaleyale aliyoyafanya Jiwe kwa sababu Samia ni mwanamke.

Pia Samia hajui kuleta figisu kibongobongo kwa show za kibabe complicated kama Magufuli. Magufuli alikuwa anaweza kuwa kakosea yeye lakini akaku gaslight wewe mpaka ukajiona wewe ndiye umekosea. Unambana kumwambia habari za kikatiba, halafu yeye anakwambia mihimili yote iko sawa lakini mmoja umechimbiwa chini zaidi. Samia hawezi show hizo.

Pia Magufuki alijua kuwauzia "watu wanyonge" story fake kwamba anawapigania. Kuanzia kwenye makinika na figisu za migodi mpaka kwenye kutunga sheria ya kulinda maliasili (to his credit, kwenye sheria kulikuwa na kitu cha msingi hapo).

Samia reversed that kwenye kuuza bandari. So at least on this one point kuna sababu ya msingi kabisa ya kuona Magufuli was better. But it is mainly a PR issue, not substance.

Pia, Uzanzibari.

Habari za Watanganyika kutawaliwa na Wazanzibari. Habari za Waarabu kuuziwa bandari, Wazanzibari kufanya kazi bara lakini Watanganyika kutofanya kazi Zanzibar, hazimsaidii Samia.

Pia kuna angle ya udini. Samia kuonekana anafungia makanisa haimsaidii kwa Wakristo wengi ambao hata hawajali sana siasa lakini ukiwaingilia kwenye dini wanakuja mbogo.

Pia, Samia kawa disappoint watu wengi. Alivyoanza kuruhusu mikutano ya siasa, watu wengi waliona Samia anakuja kubadilisha pale Jiwe alipoharibu. Alipokuja kujionesha kuwa ni walewale tu, hata 4Rs zake zikaonekana magumashi. Lissu kafungwa kisiasa na haachiwi, nitandao inafungwa mpaka JF tunaingia kwa VPN, watu wengine wakamchukia kuliko Jiwe kwa sababu walikuwa na matumaini naye makubwa sana. Mtu ukiwa na matumaini naye makubwa akaku let down unaweza kumchukia sana.

Na hii habari ya kuweka matumaini kwa mtu emotionally bila ya kuwa na nuance ni tabia inayojirudia sana kwa Watanzania wengi.

Walifanya hivyo kwa Mkapa, kwa Kikwete, kwa Magufuli na Samia. Wote hao wakawa disappoint.

Na sasa hivi Watanzania wanarudia habari hizohizo kwa Gwajima, kwa Polepole, kwa Kapteni Tesha. Kwa jeshi.

Watu tunaoangalia historia tunaona hii pattern ya kuweka matumaini kwa watu, kihisia tu, bila strategy, bila kuweka misingi ya kitaasisi, ya kuwapa nguvu watu kidemokrasia, ni hatari.

Watanzania wengi wanapenda sana shortcuts za kubadili mambo kwa haraka bila kufanya kazi kubwa ya kubadili jamii na kupata mageuzi ya kifikra ya kudumu na yenye msingi mzuri.

Ndiyo maana wengine tukionesha hizi contradictions na kusisitiza mageuzi ya kweli, ya kitaasisi, ya kijamii, yasiyotegea watu wachache au hata mtu mmoja, mara nyingi tunakuwa kama hatueleweki, tunaonekana tuko out of touch, tunaonekana watu wa diaspora tu wakimbizi.

Haya mambo ya msingi hatuwezi kukwepa kuyafanyia kazi.

Otherwise tutazunguka kqenye mashairi ya Linton Johnson Kwesi katika "Di Eagle an' Di Bear".

"Dictators get dethroned
Now clown are quickly found".

Ndiyo hiyo habari uliyosema ya kutoka kwa Mubarak mpaka Al-Sisi Misri.
Ukweli ni kwamba karata kubwa aliyokuwa nayo huyu mama ilikuwa ni kuweka demokrasia ya kweli na utawala bora ulio huru tu hata kama ingemaanisha chama kumfia mikononi bado historia ingemuandika vizuri, ila kama JK alivyoamua chama kimsifie akaivuruga katiba mpya nafikiri na yeye ametanguliza maslahi ya chama chake na kakikundi kadogo cha wanamtandao mbele zaidi kuliko taifa.

Huyu mama hataweza kujenga miundombinu kama jiwe kufunika legacy ya jiwe na yeye aweze kuacha legacy yake katika hili eneo. Miradi mingi mikubwa itakayovuma muda mrefu japo jiwe aliiacha ikiwa katikati ila siku zote bado itahesabika ni yake jiwe, kuanzia Bwawa la umeme, Daraja la Kigongo, daraja la Wami, flyovers, barabara za Dar, stendi, masoko, Serikali kuhamia Dodoma, Shirika la Ndege n.k hata SGR kama anataka kuwa na legacy yake labda ajenge nyingine kuelekea Mbeya mpaka Tunduma au Arusha ila hiyo anayomalizia kwa kusuasua kuelekea Mwanza na Rwanda litaimbwa jina la jiwe tu.
 
Huyu mama hataweza kujenga miundombinu kama jiwe kufunika legacy ya jiwe na yeye kuacha legacy yake katika hili eneo. Miradi mingi mikubwa itakayovuma muda mrefu japo jiwe aliiacha ikiwa katikati ila siku zote bado itahesabika ni yake jiwe, kuanzia Bwawa la umeme, Daraja la Kigongo, flyovers, barabara za Dar, Serikali kuhamia Dodoma, Shirika la Ndege n.k hata SGR kama anataka kuwa na legacy yake labda ajenge nyingine kuelekea Mbeya mpaka Tunduma au Arusha.
Unafikiri Samia akitaka kuleta mabadiliko ya kweli anaweza?

Au kuna "Politburo" ya CCM na "the power behind the throne", na ile inayoitwa "deep state" hao ndio wanampangia ajenda, kama Polepole anavyosema hata E. Nchimbi Samia hakumtaka kapangiwa tu aende naye?

Sasa kama Samia anapangiwa mpaka mgombea mwenza kweli anaweza kuamua muelekeo wa nchi?
 
Kama akitaka kuleta mabadiliko nina uhakika anaweza kuleta mabadiliko wakati wowote, Rais wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa CCM ni mtu mwenye nguvu sana bila kujali jinsia yake, dini yake au anatoka Zanzibar au bara. Suala ni je ana hiyo nia, uthubutu, political acumen na grand vision, simuoni kama anayo haya.
 
Nilikaa mbali na mijadala ya kisiasa kwa muda ila nimelazimika kulisema hili. Huu uzi nilikusudia kuuleta kitambo sana ila nikawa napotezea au kuahirisha kuuleta.

Kuna watu kutokana na sababu wanazojua wao wamekuwa wanatoa kauli za kutaka JWTZ lichukue uongozi wa nchi. Kuna wakati hadi nahisi kuna wanaharakati ambao ni mapandikizi waliowekwa ili kuwalinda CCM na viongozi wake pale hali itakapokuwa ngumu sana kwao.

Nasema hili la jeshi linaweza kuwa pona ya CCM. Kama mnataka mrudi nyuma hatua 50 kwenye demokrasia basi mkubaliane na hilo.

Sehemu kama Sudan, harakati za demokrasia zilizikwa rasmi baada ya jeshi kuingilia kati. Misri ni hivyo hivyo. Maeneo mengi tu demokrasia ilirudi nyuma sana baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Mnapopambana kupata uchaguzi huru na wa haki, msitamani kamwe njia za mkato kama hizo za kutaka jeshi lichukue nchi.
Kwa hiyo wewe unayeshabikia wizi wa Rais mwanamke na wanae ndo hujidanganyi au siyo?

Swali tu rahisi, kama CCM hawataki kushindana kwa haki katika chaguzi huru na za haki wanataka nini? Manake wanaalika wenye nguvu kujitwalia madaraka kwa nguvu pia, mfano Jeshi…it is such Simple!
 
CCM inaweza kuondoka vizuri tu kwa mashinikizo ya kisiasa. Hao wanajeshi wangesisitizwa wabaki makambini watimize viapo vyao kwa ukamilifu, siasa wawaachie wananchi, wanasiasa na vyombo vya kisiasa.
Hujaona wakiandamana kila siku mitaani kuwatisha wananchi? Hayo makambi unayozungumzia ni mashamba ya babu yako?
 
Ukweli ni kwamba karata kubwa aliyokuwa nayo huyu mama ilikuwa ni kuweka demokrasia ya kweli na utawala bora ulio huru tu hata kama ingemaanisha chama kumfia mikononi bado historia ingemuandika vizuri, ila kama JK alivyoamua chama kimsifie akaivuruga katiba mpya nafikiri na yeye ametanguliza maslahi ya chama chake na kakikundi kadogo cha wanamtandao mbele zaidi kuliko taifa.

Huyu mama hataweza kujenga miundombinu kama jiwe kufunika legacy ya jiwe na yeye aweze kuacha legacy yake katika hili eneo. Miradi mingi mikubwa itakayovuma muda mrefu japo jiwe aliiacha ikiwa katikati ila siku zote bado itahesabika ni yake jiwe, kuanzia Bwawa la umeme, Daraja la Kigongo, daraja la Wami, flyovers, barabara za Dar, stendi, masoko, Serikali kuhamia Dodoma, Shirika la Ndege n.k hata SGR kama anataka kuwa na legacy yake labda ajenge nyingine kuelekea Mbeya mpaka Tunduma au Arusha ila hiyo anayomalizia kwa kusuasua kuelekea Mwanza na Rwanda litaimbwa jina la jiwe tu.

Unafikiri Samia akitaka kuleta mabadiliko ya kweli anaweza?

Au kuna "Politburo" ya CCM na "the power behind the throne", na ile inayoitwa "deep state" hao ndio wanampangia ajenda, kama Polepole anavyosema hata E. Nchimbi Samia hakumtaka kapangiwa tu aende naye?

Sasa kama Samia anapangiwa mpaka mgombea mwenza kweli anaweza kuamua muelekeo wa nchi?

Kama akitaka kuleta mabadiliko nina uhakika anaweza kuleta mabadiliko wakati wowote, Rais wa Tanzania ambaye ni mwenyekiti wa CCM ni mtu mwenye nguvu sana bila kujali jinsia yake, dini yake au anatoka Zanzibar au bara. Suala ni je ana hiyo nia, uthubutu, political acumen na grand vision, simuoni kama anayo haya.
Samia hana mizizi ndani ya chama kuweza kufanya hayo mabadiliko.

Ni rare case kupata kiongozi ambaye atazingatia kuacha legacy huku akihatarisha pensheni zake za kustaafu na hata maisha yake. Inahitaji huyo kiongozi awe na conviction ya jambo husika ambayo ni wazi huyu hana. Ni rahisi kumpelekesha mtu wa aina hiyo. Anaona bora amalize awamu yake aende zake. Kama kuna mabaya anayafanya along the way, wanajuaga jinsi ya kuwasafisha mbele ya safari.

Kwa mtazamo wangu, nafasi ya mwisho ya kupata hayo mabadiliko ni wakati wa Rais Mstaafu Mkapa huku Magufuli akiwa Rais. Kutokana na historia zao, Mkapa angeweza na nadhani alikuwa anaelekea kumshawishi Magufuli afanye baadhi ya mambo hata kama ni ya kuanzia tu, ila wote tunajua kilichotokea.

Yaani kiufupi kwa mfumo wetu wa kisiasa ulivyo, kupata mabadiliko kupitia maamuzi ya Rais mwenyewe ni upate Rais mstaafu ambaye bado ana nguvu ndani ya chama amuhakikishie Rais aliye madarakani usalama wake wakati na baada ya kustaafu, halafu amuongoze katika kufanya hayo mabadiliko.
 
Samia hana mizizi ndani ya chama kuweza kufanya hayo mabadiliko.

Ni rare case kupata kiongozi ambaye atazingatia kuacha legacy huku akihatarisha pensheni zake za kustaafu na hata maisha yake. Inahitaji huyo kiongozi awe na conviction ya jambo husika ambayo ni wazi huyu hana. Ni rahisi kumpelekesha mtu wa aina hiyo. Anaona bora amalize awamu yake aende zake. Kama kuna mabaya anayafanya along the way, wanajuaga jinsi ya kuwasafisha mbele ya safari.
Sawa labda hana mizizi na hazingatii. Lakini akiamua kuzingatia ataweza?

Yoda anasema ataweza kwa sababu rais na mwenyekiti wa chama ana nguvu kubwa sana Tanzania.

Wewe unasema hawezi?
 
Siyo kila mapinduzi ni mazuri au yana nia njema kwa raia. Haiti, Zaire, Ghana (Nkrumah) kote huko walipata mapinduzi ambayo hayakuwa chanya na hayakutokana na matakwa ya wananchi.
Majukumu ya jwtz ni katiba yetu chakavu 147(1)
1. Kulinda katiba
2. Kulinda raia dhidi ya adui wa ndani na adui wa nje
3. Kulinda uhuru wa Watanzania

Tuanze na katiba
Katiba yetu inasiginwa na mafisadi na deep state kutoka CCM. Mahakama haziko huru kama katiba inavotaka, bunge haliko huru linapitisha miswada ya kuumiza Watanzania
Watu wanauliwa na JWTZ ikae kimya, Sasa si Bora isiwepo tu

Kulinda wananchi dhidi ya adui wa ndani
Adui wa ndani yupo anaumiza Watanganyika Kwa maksudi ambao ni deep state, Rais amepoteza mamlaka yake, kundi la watu linaumiza Watanganyika tu
Yaani Watanganyika wamekuwa kama watumwa wao, yaani Watanganyika wafanye kazi na kulipa kodi ili kutajirisha Abduli, Mombo, Kikwete, Kizinga na Rostam
Haya yote yafanyike na JWTZ ikitazama? Ni Bora hata isiwepo

Kuhusu uhuru wa Watanganyika
JWTZ inapaswa kuhakikisha Watanzania wanakuwa huru katika Taifa letu, JWTZ wamevuja jasho na damu kufanya Watanganyika wawe huru Leo atokee mpumbavu mmoja awafanye Watanganyika watumwa wake, wamlipe Kodi, auze bandari
Wakosoaji wauliwe
Sasa hapo si Bora tungebaki na mkoloni tujue 1

JWTZ laZima isimame kutimiza majukumu yake kikatiba hili jeshi halipo kulinda mafisadi, wauaji, wauza Rasimali za nchi,
Kikatiba JWTZ ipo kulinda wananchi na mipaka ya nchi yetu

Haya Leo Bandari imeuzwa Kwa Qatar
Ngorongoro imeuzwa Kwa UAE
KIA imeuzwa Kwa Oman

JWTZ iwe inatazama tu, laZima ifanye jukumu lake kama katiba inavotaka
 
Sawa labda hana mizizi na hazingatii. Lakini akiamua kuzingatia ataweza?

Yoda anasema ataweza kwa sababu rais na mwenyekiti wa chama ana nguvu kubwa sana Tanzania.

Wewe unasema hawezi?
Hawezi! Hawezi! Labda vyombo vya ulinzi na usalama vimuamuru, kumshauri au kumuelekeza.
 
Back
Top Bottom