Nimefuatilia kwa muda mijadala mitandaoni nikawa nakutana na hizo kauli za kutaka jeshi lichukue nchi ndiyo maana nilisema nilitaka kuleta mada hii kwa muda nilipoona hizo kauli zinakuwa nyingi.
Ni kweli ni contradiction ndiyo maana nikatumia maneno "hawajitambui" kwa sababu wanachokitaka na wanachokisema haviendani.
Sidhani kama ukimuuliza Lissu, atakwambia ni bora jeshi kuliko CCM, sidhani!
Nakuelewa sana.
Kuna Watanzania wengi hawapingi mambo kwa principle.
Wanapinga kuumizwa wao tu.
Hawapingi ubaguzi kwa principle kwamba wanapinga ubaguzi. Wanapinga ubaguzi wanapobaguliwa wao tu.
Wao wakipata nafasi ya kuwabagua wenzao kwa maslahi yao, wanawabagua tu bila kuona ubaya wa ubaguzi huo.
Mfano, leo hapa JF nimekutana na mwanaharakati anayepinga ubaguzi wa CCM na watawala. Anamshabikia Kapteni Tesha. Nikamwambia mwanaharakati wa demokrasia kumshabikia Kapteni Tesha, mwanajeshi anayechochea mapinduzi ya kijeshi, anayemsifia na kumlilia Magufuli, ni contradiction.
Mwanaharakati huyo hakupenda nilivyomwambia, akaniambia wewe ni mkimbizi tu, huna moral authority ya kutupangia mambo ya nchi yetu.
Huyu mburula haelewi hata wakimbizi wana haki, haelewi kuwa ubaguzi anaonifanyia mimi anayeniita mkimbizi ndio huo huo anaoupinga CCM inapomfanyia yeye kwa kumuita mwanaharakati.
Kimsingi hapingi ubaguzi. Angepinga ubaguzi asingenibagua mimi.
Anapinga kubaguliwa yeye tu, lakini yeye kubagua wengine walio na mawazo tofauti naye anaona sawa.
Kuna Watanzania wengi wako hivyo.
Hawa watu wanaoshabikia jeshi kuchukua nchi, kimsingi si wanaharakati wa demokrasia, ni watu ambao hawapendi utawala uliopo na ukija utawala wanaoupenda hata ujiwa wa kijeshi watafurahi tu.