Pia kuna angle ya udini. Samia kuonekana anafungia makanisa haimsaidii kwa Wakristo wengi ambao hata hawajali sana siasa lakini ukiwaingilia kwenye dini wanakuja mbogo.
Pia, Samia kawa disappoint watu wengi. Alivyoanza kuruhusu mikutano ya siasa, watu wengi waliona Samia anakuja kubadilisha pale Jiwe alipoharibu. Alipokuja kujionesha kuwa ni walewale tu, hata 4Rs zake zikaonekana magumashi. Lissu kafungwa kisiasa na haachiwi, nitandao inafungwa mpaka JF tunaingia kwa VPN, watu wengine wakamchukia kuliko Jiwe kwa sababu walikuwa na matumaini naye makubwa sana. Mtu ukiwa na matumaini naye makubwa akaku let down unaweza kumchukia sana.
Na hii habari ya kuweka matumaini kwa mtu emotionally bila ya kuwa na nuance ni tabia inayojirudia sana kwa Watanzania wengi.
Walifanya hivyo kwa Mkapa, kwa Kikwete, kwa Magufuli na Samia. Wote hao wakawa disappoint.
Na sasa hivi Watanzania wanarudia habari hizohizo kwa Gwajima, kwa Polepole, kwa Kapteni Tesha. Kwa jeshi.
Watu tunaoangalia historia tunaona hii pattern ya kuweka matumaini kwa watu, kihisia tu, bila strategy, bila kuweka misingi ya kitaasisi, ya kuwapa nguvu watu kidemokrasia, ni hatari.
Watanzania wengi wanapenda sana shortcuts za kubadili mambo kwa haraka bila kufanya kazi kubwa ya kubadili jamii na kupata mageuzi ya kifikra ya kudumu na yenye msingi mzuri.
Ndiyo maana wengine tukionesha hizi contradictions na kusisitiza mageuzi ya kweli, ya kitaasisi, ya kijamii, yasiyotegea watu wachache au hata mtu mmoja, mara nyingi tunakuwa kama hatueleweki, tunaonekana tuko out of touch, tunaonekana watu wa diaspora tu wakimbizi.
Haya mambo ya msingi hatuwezi kukwepa kuyafanyia kazi.
Otherwise tutazunguka kqenye mashairi ya Linton Johnson Kwesi katika "Di Eagle an' Di Bear".
"Dictators get dethroned
Now clown are quickly found".
Ndiyo hiyo habari uliyosema ya kutoka kwa Mubarak mpaka Al-Sisi Misri.