Mnaotaka na kulilia jeshi lichukue nchi hamjitambui

Mnaotaka na kulilia jeshi lichukue nchi hamjitambui

Nini kitazika demokrasia endapo jeshi litachukua nchi?

Kwa taarifa yako jeshi litachukua nchi kwa kipindi cha mpito tu, na katika kipindi hicho wataruhusu marekebisho ya katiba na kisha uchaguzi utaitishwa.

aliekwmabia jeshi likashachukua nchi litakaa kipindi cha mpito ni nani? yani wahuni wakamate keki ya taifa halafu waje waiache? munatakiwa musome kwa nchi za jirani hapa barani africa yaliyowatokea.
 
Acha Jeshi lichukue Nchi tu mbona ninyi hamkushauri Chadema ilipozuiliwa kushiriki uchaguzi? mbona mlikaa kimya Tundu Lissu alipo onewa na Mahakama ya CCM ?

Hao mabwana zenu CHadema hakuna hata mmoja anaelitaka hilo, wanajua siku Jeshi wakichukua nchi ndio mwisho wao, mana hawachelewi kupiga marufuku hata vyama vya siasa.
 
CCM wanaweza kufanya udhalimu wao kwa sababu kumekosekana umoja miongoni mwetu. Sisi tunategeana, ni wavivu, wabinafsi, tumekosa ubunifu na hatuko tayari kwa umoja wetu kufanya yale yatupasayo kufanya. Wachache waliojitoa muhanga wameumia na wanaumia huku tunawaangalia.

Tunashindwa hata kutumia njia zetu za kiswahili za kuwasuta huku mitaani hawa wadhalimu? Bado tunasapoti wasanii na matimu ya mpira ambayo yamejipambanua wazi yanasapoti udhalimu. Kama hata hayo yanatushinda, tutaweza nini?
Mkuu, 'Keynez', unataka umoja wetu utoke wapi, nani aulete huo umoja kati yetu ndipo tufikirie kupambana na hao CCM?

Kwa nini usifikirie kuwa ni CCM hao hao ndio wanaovuruga umoja usiwepo ili wazidi kutawala?
Wewe hata mfano tu wa yaliyo tokea ndani ya chama cha CHADEMA hayakufundishi chochote?

Umejaribu kujihoji mwenyewe kabla ya kuleta mada hii kama kweli unachangia uwepo wa umoja wa waTanzania kuwakabili CCM? Mbona ni kama wewe mwenyewe ni wakala mzuri sana wa kuwafanyia kazi hao hao CCM?

Sasa tumefikia hapa; kwenye wakati 'critical' kabisa kwenye hatma ya nchi yetu, watu wanajaribu kujenga huo umoja angalau upumbavu huu wa kututawala kwa nguvu tuukomeshe kwa kutokwenda kupiga kura au/na kujiunga kwenye maandamano. Wew unaibuka na mada ya kuwasuta hao hao!
Inaingia akilini kweli??
 
Umenifurahisha sana mkuu. Wajeda wachukue kwa mwaka mmoja au miezi 6. Tundu Lissu apewe jukumu la kuiboresha rasimu ya katiba ya Warioba. Halafu wanarudisha madaraka kwa raia na uchaguzi mpya unafanyika chini ya katiba na tume huru mpya huku Lissu akiwa mgombea. Dah!

utoto raha sana
 
Kwanza Kuna sahihi kuwa hatupo salama kwenye mazingira ya sasa .. tunapaswa kufungua mkebe wa dharura ili kuishinda hii hali.. kinachowashangaza wengi ni kana kwamba wasiwasi upo kwa wananchi na raia wa kawaida pale juu wala Hawaoni kile ambacho hayo makundi wanayaona

Sasa msingi wa maelewano ni maridhiano kwamba wote tukili kuwa kunachangamoto then tukubali kuikabili kwa pamoja... lakini tukienda na mtindo huu hata kama tutavuka salama kwenye uchaguzi bado hatutakuwa na uhakika ya kesho ya kila mmoja watu.. taifa litakuwa na watu wenye hofuu wasio kuwa huru kusema au kutenda jambo kwa mapana yake... na hapo sasa swala wengi wanaona ni heri tutumie shortcut jambo ambalo ni la hatari kubwa mnoo

Tuwaomba walioko juu kabla ya uchaguzi tukae kwenye meza ya mazungumzo ili tuwe na usemi mmoja inawezekana tusikubaliane yote ila yale ya msingi tukubaliane then haya mtambuka tuyasogeze mbele...

Walioko juu sikieni bado nafasi ipo msifanye mioyo yenu kuwa mizito..
 
Imenilazimu nisome kilichomo ndani ya mada.
Hata kama sitakiita t"akataka" kama nilivyo andika hapo juu; lakini bado sioni la maana zaidi kwa sababu tu ya kuhimiza "demokrasi".

CCM hawataki demokrasi, na wanajipambanua kuwa ni wao milele. Kukudhihirishia hilo ni matendo yaliyo wazi ya kuwabakisha madarakani kwa gharama yoyote.
Halafu anatokea mtu anakuwa na matumaini ya uwepo wa demokrasi chini ya CCM? Itatoka wapi?

Kama unaliogopa sana Jeshi juu ya ukosefu wa demokrasi, unapata wapi matumaini ya demokrasi chini ya CCM?

Unaweka mifano ya Sudan na Misri; bila ya ufafanuzi wowote ili kuwatisha watu juu ya jeshi kuiondoa CCM madarakani?

Hata sielewi maana ya hiyo demokrasi tunayo imbiwa kila mara itakuwa na maana gani endapo kama itabaki kuwa ni kuachiana tu nafasi za viongozi kwa kubadili vyama, huku tofauti kati ya wanayofanya hayaonekani.
Haya mambo ya kulilia demokrasi kila mara bila ya kuainisha ni mambo yapi yatalifaa taifa kwa maendeleo yake nalo limekuwa tatizo kubwa miongoni mwetu. Hii tabia imekuwa ni kama yumekaririshwa tu bila ya kujuwa nini hasa kinatufaa kwa maslahi ya nchi yetu

Jeshi halijawahi kuwa suluhisho la matatizo, tujifunze hilo kwa nchi nyingi sana za africa zaidi ya kuzidisha matatizo. Ikiwa CCM wamemuwaka ndani Lissu jeshi wao watampoteza kabisa, jamaa hawachelewi kupiga marufuku vyama vya siasa au kujianzishia chama wao.
 
Ni bora kabisa kuliko kubaki na Samia na Genge lake wakinyanyasa na kutenda maovu ndani ya nchi hii.

Usitishe wengine kwa vile wewe ni mnufaika wa utawala huu.

mkuu wewe upo ughaibuni unakula mema ya dunia halafu unatwambia sisi huku ni bora kulala saa 12? kuwa serious mkuu
 
Jeshi halijawahi kuwa suluhisho la matatizo, tujifunze hilo kwa nchi nyingi sana za africa zaidi ya kuzidisha matatizo. Ikiwa CCM wamemuwaka ndani Lissu jeshi wao watampoteza kabisa, jamaa hawachelewi kupiga marufuku vyama vya siasa au kujianzishia chama wao.
Mimi unayo eleza hapa siyajui mkuu, kwa maana hatujawahi kuwa na utawala wa kijeshi. Kwa hiyo hayo unayo zungumzia wewe ni mifano ya huko kwingine, ambako hata hatuwezi kusema kuwa paliwahi kuwepo na utawala wa CCM kama tunavyo ushuhudia sisi hapa wakati huu!

Ni elewa kwamba swala muhimu hapa si kutawaliwa na jeshi au la; swala ni namna gani tunaweza kuondokana na zimwi hili la CCM, ambao wanafanya kila njia wasiondoke kututawala kwa nguvu.

Kama ni jeshi ndilo linaweza kuwatoa, kwa nini tusilikubali hilo; kwa nini tuwe tu kila mara na picha hii hasi ya mifano ya utawala wa kijeshi mbaya huko kwingine?

Je, Jeshi hawawezi kuwalinda wananchi wakati wakishughulikia kuwaondoa CCM kwa kuzuia mitutu ya polisi wanaotumiwa na CCM kuwaua waTanzania?

Hili jeshi, siyo waTanzania?
 
Embu fafanua kidogo. Wamewapa au wanawapa nini?
Wamewapa matumaini kwamba vilio vyao ambavyo kwa wingi vipo mitandaoni tu, vimesikika. Kwamba hata mwanajeshi, kiumbe anayeogopeka zaidi Tanzania baada ya Mungu, naye ana-support vilio hivyo. Sio hapo tu, bali wamewapa na content ya kugossip for months bila ya kufanya chochote, kitu ambacho Watanzania wanapenda zaidi ya kula.
 
Mkuu, 'Keynez', unataka umoja wetu utoke wapi, nani aulete huo umoja kati yetu ndipo tufikirie kupambana na hao CCM?

Kwa nini usifikirie kuwa ni CCM hao hao ndio wanaovuruga umoja usiwepo ili wazidi kutawala?
Wewe hata mfano tu wa yaliyo tokea ndani ya chama cha CHADEMA hayakufundishi chochote?

Umejaribu kujihoji mwenyewe kabla ya kuleta mada hii kama kweli unachangia uwepo wa umoja wa waTanzania kuwakabili CCM? Mbona ni kama wewe mwenyewe ni wakala mzuri sana wa kuwafanyia kazi hao hao CCM?

Sasa tumefikia hapa; kwenye wakati 'critical' kabisa kwenye hatma ya nchi yetu, watu wanajaribu kujenga huo umoja angalau upumbavu huu wa kututawala kwa nguvu tuukomeshe kwa kutokwenda kupiga kura au/na kujiunga kwenye maandamano. Wew unaibuka na mada ya kuwasuta hao hao!
Inaingia akilini kweli??
Nakuelewa unachosema. Katika spirit ya demokrasia na kuwekana sawa ili kuhakikisha tunatembea katika njia sahihi, mijadala kama hii ni muhimu.

Sina kawaida ya kuchangia mijadala inayoibuka kila siku kwa sababu mingi inaendeshwa na mihemko kabla watu hawajafanya tafakuri ya kutosha na ni rahisi sana kwa watawala kutumia njia hiyo kupenyeza watu na hoja za kuvuruga njia sahihi.

Ninachotaka kusema, pamoja na maumivu yote tunayopitia, kamwe tusiache njia ya kusikilizana na kukosoana na tusikubali kwenda njia ambayo itafunga uwezo wetu wa kujadiliana kwa wazi. Wakati mwingine mtu anaweza kukosoa kwa lugha ngumu ila ni vizuri kuvumiliana. Tutakomaa kifikra na kimatamshi kwa jinsi tunavyokwenda. Peace.
 
Wamewapa matumaini kwamba vilio vyao ambavyo kwa wingi vipo mitandaoni tu, vimesikika. Kwamba hata mwanajeshi, kiumbe anayeogopeka zaidi Tanzania baada ya Mungu, naye ana-support vilio hivyo. Sio hapo tu, bali wamewapa na content ya kugossip for months bila ya kufanya chochote, kitu ambacho Watanzania wanapenda zaidi ya kula.
Alichofanya huyo Kapteni hakiingii akilini kabisa na nashangaa watu wana akili zao wamelibeba kama lilivyo. Kitambo sana niligundua kuna watu wengi hawaijui Tanzania vizuri na mifumo yake.
 
Wewe ndiyo ambaye umekuwa unapigia chapuo mapinduzi ya Marekani. Nimetaka tu kukuonyesha kuwa si kila mapinduzi yako perfect au yana sababu ambazo unaweza kulinganisha na mustakabali wa Tanzania ya sasa.
I didn't flatter nobody, all I did is to demonstrate long term outcomes of military takeover. They're messy but necessary against despots​
 
I didn't flatter nobody, all I did is to demonstrate long term outcomes of military takeover. They're messy but necessary against despots​
Siyo kila mapinduzi ni mazuri au yana nia njema kwa raia. Haiti, Zaire, Ghana (Nkrumah) kote huko walipata mapinduzi ambayo hayakuwa chanya na hayakutokana na matakwa ya wananchi.
 
Nakuelewa unachosema. Katika spirit ya demokrasia na kuwekana sawa ili kuhakikisha tunatembea katika njia sahihi, mijadala kama hii ni muhimu.

Sina kawaida ya kuchangia mijadala inayoibuka kila siku kwa sababu mingi inaendeshwa na mihemko kabla watu hawajafanya tafakuri ya kutosha na ni rahisi sana kwa watawala kutumia njia hiyo kupenyeza watu na hoja za kuvuruga njia sahihi.

Ninachotaka kusema, pamoja na maumivu yote tunayopitia, kamwe tusiache njia ya kusikilizana na kukosoana na tusikubali kwenda njia ambayo itafunga uwezo wetu wa kujadiliana kwa wazi. Wakati mwingine mtu anaweza kukosoa kwa lugha ngumu ila ni vizuri kuvumiliana. Tutakomaa kifikra na kimatamshi kwa jinsi tunavyokwenda. Peace.
Ninaelewa 'tone' ya mchango wako hapa.
Lakini, kumbuka, mara nyingi kutosikilizana ni kukosa 'flexibility' ya msimamo unaoshikiliwa na kila upande katika mjadala; na kwa kweli kuna nyakati hili linabidi liwe hivyo. Sasa kama hakuna utaratibu wa kura kuamua upande gani unabeba hoja; kama ilivyo hapa, inabidi tu kukubaliana kutokubaliana. Na kama mjadala haukuwa na lugha ngumu, sioni tatizo la kuwepo hali hiyo.

Hii tunayo sisitiziwa kuwa ni'demokrasia' kuna nyakati inakuwa ni ngumu sana hasa katika hizi nchi zetu huku; kwa hiyo binafsi nipo wazi; kama demokrasia inafanya kazi vizuri, tuitumie, vinginevyo, kama kuna matatizo; kwa nini tusitumie utaratibu ambao unatuwezesha kupata viongozi wazuri wanaosimamia maslahi ya nchi. China hawana demokrasi, lakini wamefika huko walipo sasa na ukomunisti wao.
CCM wanajigamba ni 'wajamaa' lakini tazama wanavyo tupeleka shimoni.
 
Utabili wa kipuuzi,kuna jema gani lipo kwa, uta wala wa ccm, watu wanakufa kwa umaskini, sawa Sudan jeshi limeshindwa, vipi kuhusu Misri, Burkina Faso, Mali nk?
Misri wamerudi kwenye utawala wa kijeshi na naamini wanakataa mfumo tofauti na huo kwa sababu za kijeografia na kiusalama. Huko Burkina Faso na Mali, subiri kwanza usiongee mengi. Kwani Compaore si alimpindua Sankara?
 
Mimi unayo eleza hapa siyajui mkuu, kwa maana hatujawahi kuwa na utawala wa kijeshi. Kwa hiyo hayo unayo zungumzia wewe ni mifano ya huko kwingine, ambako hata hatuwezi kusema kuwa paliwahi kuwepo na utawala wa CCM kama tunavyo ushuhudia sisi hapa wakati huu!

Ni elewa kwamba swala muhimu hapa si kutawaliwa na jeshi au la; swala ni namna gani tunaweza kuondokana na zimwi hili la CCM, ambao wanafanya kila njia wasiondoke kututawala kwa nguvu.

Kama ni jeshi ndilo linaweza kuwatoa, kwa nini tusilikubali hilo; kwa nini tuwe tu kila mara na picha hii hasi ya mifano ya utawala wa kijeshi mbaya huko kwingine?

Je, Jeshi hawawezi kuwalinda wananchi wakati wakishughulikia kuwaondoa CCM kwa kuzuia mitutu ya polisi wanaotumiwa na CCM kuwaua waTanzania?

Hili jeshi, siyo waTanzania?

Mkuu kuna tofauti kubwa katika jeshi kuwalinda wananchi wakati wakipamabana kuwaondoa CCM na jeshi wao kuchukua hatua kwa maana mapinduzi kuwaondoa CCM. hivo ni vitu viwili tofauti.
Wanachokishabikia hawa vijana wakibongo wanataka jeshi wachukue nchi.
kwa experience yangu ya kiafrika Jeshi wakichukua nchi tutaishia kutamani bora tungebakia hata na hawa CCM lakini ndio muda haurudi tena nyuma.
 
Hapana.
Mimi ninacho kiona wakikishabikia vijana wa Bongo ni kuondolewa madarakani utawala mbovu/ovu wa CCM, bila kujali njia itakayo tumika; iwe jeshi, au wananchi wenyewe. Nami ninawaunga mkono katika hilo; kwa maana CCM (soma Samia na Genge lake), wameziba kila aina ya njia kufanya hivyo kwa nia halali zote.

Jeshi ni waTanzania pia; tunatishana hapa juu ya ubaya wao mkubwa kwa mifano ambayo hatujawahi kuishuhudia hapa.
Kama na wao ni wabaya kama walivyo CCM sasa hivi; itakuwa bahati yetu mbaya; wakiwa ni nafuu na kuruhusu turekebishe mambo yetu ili tusonge mbele, hiyo itakuwa ni bahati kwetu.

Lakini nisichokubaliana nacho ni huku kutishana kwingi juu ya jeshi, huku ikionekana tunatetea maslahi ya waliopo kwenye utawala sasa hivi kinyemela.
 
Ninaelewa 'tone' ya mchango wako hapa.
Lakini, kumbuka, mara nyingi kutosikilizana ni kukosa 'flexibility' ya msimamo unaoshikiliwa na kila upande katika mjadala; na kwa kweli kuna nyakati hili linabidi liwe hivyo. Sasa kama hakuna utaratibu wa kura kuamua upande gani unabeba hoja; kama ilivyo hapa, inabidi tu kukubaliana kutokubaliana. Na kama mjadala haukuwa na lugha ngumu, sioni tatizo la kuwepo hali hiyo.

Hii tunayo sisitiziwa kuwa ni'demokrasia' kuna nyakati inakuwa ni ngumu sana hasa katika hizi nchi zetu huku; kwa hiyo binafsi nipo wazi; kama demokrasia inafanya kazi vizuri, tuitumie, vinginevyo, kama kuna matatizo; kwa nini tusitumie utaratibu ambao unatuwezesha kupata viongozi wazuri wanaosimamia maslahi ya nchi. China hawana demokrasi, lakini wamefika huko walipo sasa na ukomunisti wao.
CCM wanajigamba ni 'wajamaa' lakini tazama wanavyo tupeleka shimoni.
Nakumbuka Obama aliwahi kusema demokrasia ni ngumu ila haina mbadala. Akasema Marekani haijawahi kuwa perfect ila imeacha mlango wazi wa kuwa bora kesho kuliko leo. Hapa na paraphrase tu.

Kuna nyakati kweli mnakunjana mashati kwa kushindwa kuelewana na kukubaliana ila hiyo ni bora kuliko "sauti ya mmoja ndiyo amri".

Pamoja na changamoto ambazo demokrasia yetu imepitia miaka ya hivi karibuni, kuiweka pembeni badala ya kupambana kuilinda na kuiboresha ni kurudi nyuma bila guarantee yoyote kuwa utaboresha kile unachoona sasa kina matatizo.

Wameumia wengi mno kujenga hiki kidogo tulichonacho. Kukata tamaa na kurudi nyuma sasa hivi ni kusaliti machozi, jasho na damu zao.
 
Back
Top Bottom