Kuna sababu zaidi ya elfu, lakini Kwanza kabisa kwa sababu hakuna hata tafsiri ya uchawi iliyonyooka, karibia kila mtu au jamii wana tafsiri zao tofauti kuhusu uchawi.
Pili sijawahi kuona ushahidi wa uthibitisho wa uchawi, nimekuwa nikisikia tu story ambazo karibia zote zina contradictions nyingi, zinahusu kukosa uelewa na akili ndogo za kuelewa mambo na imagination.
Tatu kwa sababu naona jamii nyingi zilizojikita katika imani za uchawi/ushirikina zina ujinga mwingi sana na mambo mengi ya hovyo sana tofauti na zile zinazoongozwa na sayansi zaidi.
Nne, ukweli ni kwamba kuna mambo mengi tu ambayo hayajulikani au hayawezi kuelezwa na sayansi kwa sababu kwanza ulimwengu ni mkubwa sana na una mambo sana na kila siku sayansi inapiga hatua kwa baadhi ya mambo na mengine yanabaki gizani. Chukulia mfano wa jambo dogo tu kama mechi ya mpira ambapo kuna refa, kuna wasaidizi wake , kuna VAR na kuna sheria 17 za mpira lakini refa anaweza kutoa matokeo ya utata yakabishaniwa hata miaka 10 kwa sababu binadamu wana biases zao na kwa sababu tofauti ya tafsiri za ubongo wa binadamu katika mambo hasa yaliyo subjective.
1. Kuhusu tafsiri ya uchawi kutofautiana sio hoja ya msingi, kitu muhimu inajulikana ni kipi kinakusudiwa kwa suala hilo sio kwenye neno uchawi tu hata maneno kama uhai na kifo pia yana maana mbalimbali kila mmoja anaweza kueleza anavyoelewa yeye.
2. Kuhusu kutowahi kuona ushahidi. Sijui kama umewahi kujiuliza unaelewa huo uchawi hasa ni nini na unaposema hujawahi kuona ushahidi wa uchawi huo ushahidi unataraji kuweje kwa namna unavyoelewa wewe uchawi?
Mimi naona huwa mnataka kushuhudia kitu tofauti na hali ya kawaida yani mfano labda muone mtu katokwa mapembe kichwani au kaota mkia pengine hiyo ndio mifano ya vitu mnataraji kuona kwenye huo ushahidi wa uchawi, kinyume na hivyo sioni ni aina gani ya ushahidi wa uchawi ambao mnataraji na kusema haujawahi kuona ushahidi huo.
Kwa sababu kwanza huwa hamfanyi uchunguzi na ndio maana hata hapa tunavyojadiliana inakuwa kama nyinyi mnaishi ulimwengu tofauti na tunaoishi sisi hivyo habari za mambo yenye kuhusu uchawi ni story tu ambazo mnasikia kutoka katika ulimwengu tunaoishi sie ila nyie wenyewe binafsi hamjawahi kukutana na matukio yenye kuhusishwa na uchawi.
Ndio maana hata tukiwaelezea mambo ambayo watu tumepitia na kufanya kuhusu mnaishia kupinga kinadharia nadharia tu.
3. Kuhusu jamii zilizojikita kwenye uchawi kuwa zina ujinga. Niseme suala la ujinga kwenye jamii halisababishwi na watu kuamini uchawi kwa sababu uchawi haujachukua nafasi ya shule kwamba uchawi unafanya watu wasiende kusoma kuondoa ujinga.
Nilikwambia kwamba wenye kuamini na wasioamini uchawi wote tunafanya mambo sawa tu tunaenda shule, tunaenda hospitali n.k kwahiyo kama ni ujinga basi ni ujinga wenye kuhusu sisi wote na sio wale wenye kuamini uchawi tu.
Mfano hao unaosema wanaongozwa na sayansi kama hao wazungu ila bado wana workshops zenye kufundisha uchawi pamoja na psychic abilities na vitabu kibao tu vyenye kuhusu mambo hayo. Kuna watu huko kazi zao ni kutoa mizimu(ghost hunter) kwenye nyumba za watu na wanalipya kwa kazi hizo, kuna watu wengine kazi zao ni kuongea na watu waliyokufa(medium) na watu wanaenda kwao ili kuweza kuwasiliana na watu zao waliyokufa.
Hayo ni machache sana ambayo yapo huko kwa hao wenzetu ambao wanaongozwa na sayansi, lakini pamoja na wao kuamini kufanya hayo ila bado ni watu waliyoelimika na hufuata sayansi huwezi kuwalinganisha na sisi.
4.Hili la sayansi shida ni kwamba siku hizi watu mnaamishia imani kama dini katika sayansi, yani jinsi mnavyoichukulia sayansi ni kama vile waumini wa dini walivyo na imani kuhusu dini. Mmeifanya sayansi kama dubwasha fulani ambalo ndio linaamua kipi sawa na kipi sio sawa, yani wewe hapo unasubiri mpaka yapatikane maelezo ya sayansi ndio ukubali jambo na kusahau sayansi ni elimu na tafiti zake hufanywa na binaadamu. Na hii ndio shida waliyonayo hizo jamii zenye kujifanya kuamini sana katika sayansi tu watapinga kitu kisa tu hakuna maelezo ya kisayansi.
Nimekuwa nikitoa sana mfano wa meditation hapa kwamba watu walijua faida za meditation na kuifanya toka karne hizo wakiwa hawajui zaidi mambo ya ubongo wala hawana vifaa kama vilivyopo leo.