Mmh!!

Hapo after school bash imepita nimemuona hadi clouds TV akikata mauno alafu report ya shule imekuja kashika nafasi ya 857 kati ya wanafunzi 859, nitakinyoa hicho kiduku kwa style hiyo.
 
Nakumbuka kipindi fulani (pengine darasa la pili au la tatu hivi) nilikuwa na tatizo la chawa basi kunyolewa na walimu wa zamu hata viranja ilikuwa ni kawaida tu. Ila hii ya kupandiwa mabegani aisee hii ni mpya. Si ajabu Mshana Jr anahusika hapa!

Haaahaaaaa,
Live mshana anahusika hapa.
:D:D:D:D:D:D
 
Yep. Watoto wa mjini/geti kali mnashangaa chawa eeh? Kwa wengine kawaida tu na mapito ya maisha. Leo zimebakia historia. Na siku nikipata watoto nadhani watafikiri ni hadithi baba yao natunga . Maisha!
Tz kubwa sana, na wengi hata hawaijui. Wanaongea na kuhoji na kutoa mapendekezo mengimengi wakidhani Tz ni Dar tu na Simiyu au Ifakara au hata vimiji kama Lugoba, Meatu, Kasulu na Turiani ndo vijiji vyenyewe vya Tz ambako maskini huishi huko. Hawajui siku ya kwanza mtu kutoka mbwinde (ndanindani sana) alipofika Chalinze akajua ndo Dar es Salam.Huwa nacheka sana, naskia kuna mzee alienda Tandale sokoni na bintiye asomaye USA tangu utoto wake, eti alilia kumuona mtu kabeba Lumbesa, alidhani atakufa.
 
Hahaha dah afe kwa kubeba lumbesa akat watu wanabeba zege
 
Yep. Watoto wa mjini/geti kali mnashangaa chawa eeh? Kwa wengine kawaida tu na mapito ya maisha. Leo zimebakia historia. Na siku nikipata watoto nadhani watafikiri ni hadithi baba yao natunga . Maisha!

Ha ha ha, enzi zile tulikuwa na utaratibu wetu wa kutoana chawa kichwani, nikikutoa moja nakupiga konzi moja, nikiua mayai 2 nakupiga konzi moja.

Na ilikuwa ni lazima ukubali, hutaki hakuna kucheza na wenzio, baki nyumbani au hakikisha umenyolewa na huna chawa.
 
Back
Top Bottom