Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

Hivi kweli Hussein Mwinyi ana standinding ya kuwa Waziri wakati si mbunge? Labda kama miye nimesahau katika chaguzi zote za nyuma sikumbuki kuona mawaziri wakiendelea na shughuli za uwaziri baada ya Bunge kuvunjwa, naomba nikumbushwe. Inawezekana kabisa nimekosea kabisa katika uelewa wangu kwa sababu toka zamani tulijua Bunge likivunjwa hakuna mawaziri, na shughuli zinafanywa na Makatibu. Why now tunafanya vinginevyo kuna mabadiliko yaliyopita ambayo hatukuyajua?
Mwanakijiji,
AG alishalitolea ufafanuzi hili. Kama ufafanuzi ule hautoshi hilo litakuwa ni suala jingine ambalo linahitaji marekebisho ya Katiba yetu ya JMT. Wenzetu Kenya wameliona hili kwenye Katiba yao mpya. Mawaziri wao sasa hawatatokana na Wabunge na idadi ya wizara imetajwa kabisa kwenye katiba yao mpya. Teuzi zote za Rais wao zitathibitishwa na Bunge. Wana Katiba nzuri sana sasa kuliko hata ile ya South Africa.
 
...ingekuwa hivyo basi kina Mwanakijiji wangebadilisha hii nchi,kila siku wanasoma na kuandika lakini bado tuko pale pale pale.
"Mwanakijiji kila siku anaandika lakini bado tuko pale pale”

Unamshambulia mtu ambae hayumo katika mabishano yako, unanunua tafrani. Mwenzio anaweza kuwa anaona kuandika kwake kunachangia maendeleo kwa kiasi fulani, au ni kazi yake ya mkate wa kila siku, wewe unabeza. Mwanakijiji ambae haishi kukutetea mpaka hata ulipotaka kuenguliwa na kamati za CHADEMA. Halafu unampiga madongo ya chini chini. Regia, kuwa mwangalifu kidogo.

hebu Ms Mtema tufafanulie kidogo ulijuaje kama umemzidi akili ( au japo jibu la general la watu wanajuaje kuwa wamemzidi fulani akili)
Sema wewe kiazi. Mimi nikisema huu muhogo jama, unasema nina mzizi.
 
tatizo lako tindikali, you over kill while you can just give her enough rope........:smile-big:

eeeh,,,,sasa na wewe hapa hapakufai twende kule.....unanunua kesi bure hapa....:confused2:
 
Solution hapa ni kubadili katiba kuondoa huu utata.....maana mnaweza bishana mpaka asubuhi hapa na jibu lisipatikane:becky:

Katiba inasema kila mtanzania ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa......hapo hapo wanakwambia utachaguliwa tu pale utapo pitia kwenye cha cha siasa!!
Katiba inasema huwezi kuwa waziri kama wewe si mbunge......hapo hapo inakwambia uwaziri wa mtu haukomi kwa sababu ya "bunge kuvunjwa" na bunge linapovunjwa wabunge wanapoteza hadhi ya kuwa wabunge!! :confused2:
 
viongozi uchaguliwa kila baada ya miaka mitano, na si miaka minne na miezi saba. Hivyo kuvunjwa kwa Bunge maana yake ni kuvunjwa kwa shughuli za bunge na si kuwapokonya watu Ubunge. Mmbunge anabaki mmbunge mpaka wapiga kura wanapochagua tena kipindi kikifika, kwa sababu mmbunge achaguliwi na bunge bali wapiga kura na wapiga kura hawajoengea bado hivyo ingawa shughuli za bunge zimevunjwa, elected members still act as reps until the day after election if they're voted out (utata uliopo kwetu inakuaje mmbunge anaeshindwa kura za maoni kipindi hiki)

Kwa maana hiyo uwezi kusikia baraza la mawaziri pia linavunjwa, lakini still vikao vya mawaziri havipo tena mpaka baada ya uchaguzi au unless something out of the ordinary happens, hivyo waziri wanabaki na majukumu yao (overseers of their ministrials until then without implementing any changes, vinginevyo kama kila kitu kitavunjwa basi na hao wafanayakazi kwenye mawizara wanafanya nini kipindi hiki) kwa maana hiyo duty zote za public in relation to the ministrial bado una expect the current minister ndio atokee mpaka after the election when the new cabinet as been formed na waziri bado ni mmbunge kama alikuteulia through voting system until democracy takes place again after the election date. Iwapo atashindwa ndio ni longer mmbunge.

Anyhow thats how colonial masters interpret the situation, hila wao uvunja bunge only two weeks before election nadhani.
 
Cha muhimu tunatakiwa kusahihisha katiba yetu huu mwanya unawafanya watu watumie nyadhifa zao kupindisha sheria kama kulazimisha,msimamizi wa uchaguzi waengue wagombea tuu kwa sababu waziri kasema ole wao siku ikifika
 
Solution nzuri tu ni kuondoa ulazima wa mawaziri kuwa wabunge, mawaziri watoke nje ya bunge lakini wawe confirmed na bunge. Simple and clear.

Unaondoa / punguza significantly conflicts of interests za legislature / executive, electioneering, favoritism, backdoor dealings etc na hapo hapo unabakisha ukweli kwamba mawaziri watapata consent ya watu by proxy.

Plus unakuwa na abigger pool to choose from.

Yale yale niliyoyasema mimi.
 
"Mwanakijiji kila siku anaandika lakini bado tuko pale pale"

Unamshambulia mtu ambae hayumo katika mabishano yako, unanunua tafrani. Mwenzio anaweza kuwa anaona kuandika kwake kunachangia maendeleo kwa kiasi fulani, au ni kazi yake ya mkate wa kila siku, wewe unabeza. Mwanakijiji ambae haishi kukutetea mpaka hata ulipotaka kuenguliwa na kamati za CHADEMA. Halafu unampiga madongo ya chini chini. Regia, kuwa mwangalifu kidogo.

Sema wewe kiazi. Mimi nikisema huu muhogo jama, unasema nina mzizi.

Hili nishalisema mara lukuki, no tact, no exposure, no strategy, no method, no priority, you name it.

Halafu huyu anataka kwenda bungeni huyu hajui hata kujenga alliances, anakwenda vitani anaanza kuwapiga risasi wanajeshi wa jeshi lake mwenyewe, bila sababu, huyu mtu ana akili kweli huyu?

Jamani mnaona ninachosema hapa? Mnanielewa ninaposema kwamba huyu bibie ana udhaifu katika kupangilia mawazo yake ? Kwamba kimsingi ana matatizo yaliyo so fundamental kiasi kwamba akienda bungeni atakuwa more of a liability than an asset, mnaona mambo haya ?

And this is not an incident, it is an established pattern. Kuna siku kawatukana "wabeba maboksi" hapa, basically Watanzania wote wa diaspora wanakuwa described kwa jina hili, watu ambao kuna wengi tu walikuwa wana m support. Siku nyingine kawa lambast wanachama wenzake wa CHADEMA wazi wazi hapa, Kitila, Mnyika na Tundu Lissu, in a very unnecessary and tactless post (mpaka yeye mwenyewe akaitoa). Bahati tu hawa watu either hawakuiona post au kama wameiona wamekuwa waungwana na kuachia mambo yaishe tu, je akikutana na vichwa ngumu wasiokubali mambo yaishe kirahisi? Si ataleta vita isiyo sababu huyu? Leo tena anakuja kumu alienate Mwanakijiji kwamba anachoandika Mwanakijiji si lolote si chochote, yaani huyu ana tabia ya kudharau sana watu.

Halafu ananisema sina uwezo wa kumfikia yeye, inaonekana yeye ndiye anakuwa gaffe machine na kujipaka controversy kila mara anapoandika kitu hapa bila hata kujua, kwa sababu she is a birdbrained boondocks bred bargain bilharzia type of social climbing, fame imbibing, fantasy cultivating no good airhead.

And we don't want that kind in parliament, don't say I didn't warn you.
 
Mimi nina kawaida ya kusoma kwanza kabla ya kutoa hoja. Mwanakijiji ungesoma katiba ya nchi yaani URT usingekuwa na hoja hii au ungekuwa nayo wakati Rais mtarajiwa Dr. Slaa anapofanya mchakato wa kubadili katiba yetu ndani ya siku 90 baada ya kuapishwa kwake! Ibara ya 57 (1) na (2) zinaongelea au kujibu hoja hii. Mfano, 57 (2) inasema "kiti cha waziri au naibu waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo: a. ..., b. ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa bunge, c. ..., d. ... e. ... f. ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika madaraka hayo, g. ..." Source: The Tanzania National Website


Hawa jamaa yaani mawaziri wataendelea kushika nyadhifa hizo mpaka siku jamaa anaapishwa. Swali kwa katiba, je kampeni zao zitatenganishwa vipi na shughuli za kiserikali? Je, watatumia magari na fedha za serikali kuchanganya kampeni na serikali? Mimi naona ni ngumu kidogo!!

Hapa ni lugha ama ni nini? "Kwasababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa bunge" ambapo sababu hizo zimetajwa kwenye kifungu (a) ie kifo nk....lakini kifungu b kinaainisha kuwa kuvunjwa kwa bunge ndo sababu ya kukoma kwa uwaziri ama unaibu waziri....Yani sababu hiyo(ya kuvunjwa kwa bunge) ndiyo pekee inayoweza kukwamisha madaraka hayo other than hizo nyingine zilikuwa mentioned kwenye kifungu "A" Kwamba rais ana uwezo wa kuchagua waziri mara baada ya bunge kuvunjwa haina maana kwamba wale wote waliopoteza uwaziri/ubunge wao mara baada ya bunge kuvunjwa bado ni mawaziri.
Tukichukua vifungu vifungu tu itapelekea matatizo ya utafsiri,kama inavyotokea kwenye misahafu.
 
Ukisoma vifungu vidogo (b) na (f) kwa pamoja katika ibara ya 57(2) ya katiba, it is clear viti vya mawaziri havipo wazi kwa sasa.
 
Ndio hivyo. Hii pia italeta confusion maana technically speaking hajastaafu.

Kuondosha confusion ingewezekana kutofautsha inapokuja kumnukuu Werema kwa mfano, kinachotakiwa ni kwa mwandishi kusema "....Judge Werema ( as he then was)......" lakini hili nalo litafinyika nadra maana muktadha mara nyingi hautatoa fursa hiyo.Matokeo yake inatumika "Judge" (Werema) the AG, kama title ya "Mr." au "honorable" ..

Sasa kama "technically speaking hajastaafu" ujaji, this reinforces and reintroduces my original objection.

Kama Jaji technically bado hajastaafu, na jaji ni mtu wa Judiciary, anafanya nini katika kazi ya u A.G ? Ikija showdown kati ya judiciary na executive technically speaking hapa si kutakuwa na a technical conflict of interest ?
 
Mtazamaji thank you for the comment.Mimi wala sikati sikatishwi tamaa na huyu jamaa.nafahamu kwamba namzidi kiuwezo kwa mbali sana,yeye kazi yake ni kubishana na watu tu kila siku na hasa watu tuliomzidi akili.Nimekuwa nikijuliza kwanini ananifuata kiasi hiki lakini sijapata bado jibu.Kutofahamu kipengele kimoja cha katiba haimaniishi kuwa huijui katiba.Maendeleo hayaletwi na kuijua Katiba yote,ingekuwa hivyo basi kina Mwanakijiji wangebadilisha hii nchi,kila siku wanasoma na kuandika lakini bado tuko pale pale.Maendeleo yanaletwa kwa vitendo sio kukaaa kwenye kompyuta masaa 24 na kubishana na watu.Ninafuraha kwamba mimi ni sehemu ya mabadiliko katika nyanja zote,ya kuandika na kufanya kwa vitendo.Wengine watabaki kuwa waongeaji tu.

Dada yangu Regia,

Be careful with what you write, unaweza sababisha watu wanaokuona a real "woman of substance" waka-kudefine vinginevyo; usiruhusu emotions zako zitalawe posting hapa jamvini. Kiranga is a very good person to you, i can see you are taking his challenges personal. Kwa kweli hapo kwenye bold nimeshindwa kukuelewa!! Nimekuwa nasoma sana posts za MKJJ juu yako, infact they are always on your favor, now what is this?

Mabandiko yako yatakufikisha pabaya dada yangu, you are running for a national seat, think twice before post anything. I advice you to take Kiranga's argument positively, they will build you up.

Allow changes from you, before preaching them to Kilombero people.:confused2:
 
Kiranga,Mwanakijiji na wengineo Male-oriented society;

Tuwe kama tu Rais Obama ambaye hata siku moja hakumshambulia jukwaani Mama Clinton kwenye kampeni zake ingawaje mama huyu aliongea sana negative kuhusu yeye hata akaileta hadi ad ikiita "3 am in the morning"ikimuonyesha eti Obama atakuwa legelege kama akija kuwa Rais.

Tuwe tu kama Rais Obama ambaye hadi leo hasemi chochote negative kuhusu mashambulizi ya kila siku yanayoletwa kwake na mwana mama Sarah Palin;tumuige hata Makamu wa Rais Biden ambaye kwenye mdahalo wake na Mama Palin alijizuia kabisa kumjibu vibaya Mama mbwatukaji Sarah!

Kiranga ndugu yangu,akina mama wana udhaifu wao hasa wa inferior-complex na study nyingi za physiology zimeonyesha hivyo,cha kufanya ni kupunguza makali ya maneno dhidi ya mgombea Regina hata kama kaandika kinyume na mategemeo yetu;kwa hili namsifu sana Mwanakijiji kwa kukabiliana nalo hasa kwa kukaa kimywa hadi sasa kufuatia andiko la dada Regina lililomdhihaki waziwazi kabisa!

Dada Regina endelea kupambana na kampeni zako,nina uhakika unaweza kushinda na kubadili mamabo mengi sana Bungeni;mm binafsi nipo tayari kwenye upande wa strategies nikitakiwa kufanya hivyo!

Asanteni sana bandugu na bajamaa!
 
yaani malafyale umekuja kumtetea mtu mmoja lakini kama umeitusi jamii nzima ya wanawake hivi!

kwa mwanamke mwenye 'kuweza', kuambiwa asikosolewe kwa sababu ni dhaifu ni tusi la aina yake.
 
yaani malafyale umekuja kumtetea mtu mmoja lakini kama umeitusi jamii nzima ya wanawake hivi!

kwa mwanamke mwenye 'kuweza', kuambiwa asikosolewe kwa sababu ni dhaifu ni tusi la aina yake
.
Ahsante. Gaijin unashtukia hicho kitu?

Nyingine ni ile kauli mbiu ya "Wanawake tukipewa nafasi tunaweza,"ukipewa nafasi na nani? Kwa hiyo wewe dhaifu huwezi kujichukulia nafasi? Waziri Sitta, wa Jinsia na Watoto, kila akiitumia huwa nazima runinga hapo hapo, inanikera kupita kiasi. Huwezi kudai haki kwa kuanza na dhana kwamba we dhaifu.

Na huyu Mtema hatutakiwi kumuonea huruma. Ni mchemfu, awe mwanamke awe mwanamme.
 
yaani malafyale umekuja kumtetea mtu mmoja lakini kama umeitusi jamii nzima ya wanawake hivi!

kwa mwanamke mwenye 'kuweza', kuambiwa asikosolewe kwa sababu ni dhaifu ni tusi la aina yake.

Gaijin;

Hakuna sehemu kwenye andiko langu nimesema akina mama wasikosolewe;kwenye andiko langu nimesemea umuhimu wa kuchagua maneno kwa uangalifu unapoandika au kuongea chochote kuhusu mwanamke,nikaongelea hata kuhusu Obama vs Clinton kama mfano hai!

Gaijin;

Pole sana kama andiko langu lilikukwaza lkn sikuwa na maana hiyo ndugu yangu!
 
... nimesemea umuhimu wa kuchagua maneno kwa uangalifu unapoandika au kuongea chochote kuhusu mwanamke...

Pole sana kama andiko langu lilikukwaza lkn sikuwa na maana hiyo ndugu yangu!
Mbona we mwenyewe hukuchagua maneno kwa uangalifu? Utasemaje mwanamke tumchukulie taratibu kwa vile ana udhaifu ulioonyeshwa kisayansi? Huo kwanza ni uongo mkubwa, ni mchemko mkubwa, na huwezi kuthibitisha tafiti uliyofanya ukang'amua kwamba mwanamke kaumbwa dhaifu.

Tumsifu na kumkosoa Mtema bila kujali jinsia yake.


akina mama wana udhaifu wao hasa wa inferior-complex na study nyingi za physiology zimeonyesha hivyo,cha kufanya ni kupunguza makali ya maneno dhidi ya mgombea Regina hata kama kaandika kinyume na mategemeo yetu;!
 
Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.

Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.

So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!
....Ishu ya BASHE ilisababisha MBUGE MASHA kuitwa wizarani kutolea maamuzi.
Nchi inaongozwa kihuni hii
 
Back
Top Bottom