Kuwa mbunge ni SIFA YA LAZIMA: Katiba inasema mawaziri wote ni lazima watokane na wabunge. Period.
Kuna mazingira ya Kikatiba ambapo Rais anaweza kuteua mtu ambaye si mbunge kuwa Waziri (lakini lazima awe mtu aliyekuwa Mbunge katika Bunge lililopita). Mazingira hayo yameanisha katika ibara ya 90. Kwamba Jamhuri iko vitani au kuna jambo ambalo linalazimu Rais aunde serikali. Sasa hivi hakuna na nilazima Rais "ateue" siyo wao "waendelee" kuwa mawaziri kana kwamba hawakupoteza ubunge wao.
Ndio lakini katika mazingira fulani si kwamba anaendelea kuwa Waziri wakati Bunge limevunjwa.
"Hivi leo" hawezi kwa sababu hakuna mazingira ya kuteua mtu kuwa Waziri bila kuwa Mbunge. Na unaposema kuteua maana yake, si kwamba waliokuwepo wanaendelea kuwa mawaziri.
Kuna mazingira ya Rais kuteua watu nje ya Bunge na mazingira hayo hayapo kwa sasa.
Kuna vitu vilivyosemwa katika katiba, na vitu anavyosema Mwanakijiji.
Katiba ilivyosema ni kwamba, sifa ya kuteuliwa kuwa waziri ni ubunge, pia mawaziri hawakomi kuwa mawaziri kwa bunge kuvunjwa, pia rais anaweza kumteua mtu ambaye hakuwa waziri, lakini alikuwa mbunge katika bunge lililovunjwa, kuwa waziri baada ya bunge kuvunjwa na kabla ya bunge jipya kuapishwa.
Ni vitu vilivyowekwa wazi katika katiba, sasa kama hukubali exceptions na qualifications hizi na unataka katiba irekebishwe nitakuelewa.
Lakini ukijifanya kukomaa shingo, kwamba mtu akikwambia statement a, na kutoa exception b, kwamba useme ukishatoa statement a huwezi kutoa exception b, utakuwa ume fail somo la logic. Hata misahafu ina qualifications, itakuwa hiyo katiba ?
Nikiwambia natengeneza Non Euclidean Geometry kwamba pembe zinapimwa kwa nyuzi, lakini pembetatu zote zina nyuzi zaidi ya 180, huwezi kuanza kupinga eti hakuna pembetatu iliyo na nyuzi zaidi ya 180, utakuwa unapingana na axioms za Non Euclidean Geometry.
Vivyo hivyo, katiba ni axiomatic, huwezi kupinga axioms zilizo katika katiba. Kama huzikubali zibadilishe, lakini zikiwemo tu katika katiba ni valid mpaka utakapozibadilisha.