Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

Hata mimi nashangaa.Hata Kikwete kuendelea kuitwa Rais mi bado sielewi..
JK bado ni rais mama,hii ni kwa mujibu wa elimu ndogo ya uraia niliyopata shuleni. Hata hivyo hao mawaziri kikatiba wameshapoteza uwaziri wao. Nadhani uwaziri nao umechakachuliwa hapa.
 
Hata mimi nimegundua hili, ila sijawasamehe. Kuwasamehe ni uhaini.

Watu wana psychological problems zinazowafanya wajione wanaweza hata yale wasiyoweza, ego hizi zinawafanya waende kugombea nafasi zenye dhamana kubwa kwa umma huku wakifikiri "mtu yeyotte anaweza kuwa mbunge" na kusema hivi wazi wazi.

Bora hata miye nikiwa na psychological problems nikabwabwaja hapa JF impact yangu ndogo, unaweza kuni ignore tu. Watu wenye psychological problems za kujiona wanaweza vitu wasivyoweza wakiweza kuingia katika kazi zenye dhamana ya wananchi watatuharibia mambo makubwa sana.

Wewe mtu unaenda kugombea ubunge hujui hata katiba inasemaje kuhusu urais na unavyoathiriwa na kuvunjwa kwa bunge, wewe uko serious kweli au unacheza cheza tu?

Watu wakikwambia huko seroius kweli utasema wanakuonea ?
Japokuwa ni kweli kuwa hakuna anayejua kila kitu lakini hapo kwenye nyekundu mkuu umenena kitu cha msingi sana. Yaani leo tumefikishwa mahali inaonekana kama vile mtu yeyote anayeweza kubwabwaja anaweza kuwa mbunge. So annoying ... :mad2:
 
Ishu hapa ilikuwa ni iwapo kuna uhalali wa kikatiba kwa mawaziri kuendelea kushika nyazifa hizo ilhali wamepoteza ubunge. Lakini naona mmetupeleka kwingine.

Mngetundea haki zaidi kama mngeanzisha thread nyingine juu ya mgombea ubunge kutoijua vizuri katiba!
 
Bado mnashindana na KATIBA yetu!? Ombeni Bunge lijalo ambalo naona lina vilaza na majambazi wengi tu waiondoe serikali bungeni, i.e mawaziri wasiwe wabunge.
 
Kuna sera ya diversity katika kila kitu lol! Bunge lijalo litakuwa na kila aina ya watu mradi wananchi wamesema.
Hapo ndo suala la MGOMBEA BINAFSI linapochapua mwendo.
Haiwezekani kuwa na wabunge wanaoshiriki masuala ya kishirikina (sheria inakataza ushirikina) halafu tuseme kuwa wananchi wamesema. Hapo nadhani wananchi watakuwa wamelazimishwa kusema au wamesemewa. Aibu kubwa hii.

Siku nyingine tutawapigia kura MAJAMBAZI halafu tutasema kura zimeamua.
 
Tecnically wabunge bado wanaendelea kuwa wabunge mpaka uchaguzi mpya ufanyike.

Ukiwapotezea uwaziri wabunge kabla ya uchaguzi mpya utatengeneza leadership vacuum (as if we didn't have one already).
Mkuu, Katiba ya nchi inabainisha ukomo wa mtu kuwa Mbunge. Vile vile imeweka wazi mahitaji ya mtu kuwa Waziri.

Miaka yote, katika serikali zote zilizopita, mara baada ya Bunge kuvunjwa, Mawaziri wote waliacha kuwa katika nafasi zao. Sielewi wakati huu kwanini Katiba ile ile iliyowaweka isifuatwe.
 
Umevipitia vifungu vya katiba nilivyoweka na unaweza kubase criticism kutoka katika katiba?

Katiba imesema wazi kwamba waziri hapotezi uwaziri kwa bunge kuvunjwa, na in fact rais anaweza hata kumteua mbunge yeyote wa bunge lililovunjwa ambaye hakuwa waziri, kuwa waziri mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa. Kwa hiyo hata mtu kama Malecela ambaye hakuwa waziri katika bunge lililopita, anaweza kuteuliwa kuwa waziri, unataka iwe explicit kivipi zaidi ya hivyo ?
 
Ishu hapa ilikuwa ni iwapo kuna uhalali wa kikatiba kwa mawaziri kuendelea kushika nyazifa hizo ilhali wamepoteza ubunge. Lakini naona mmetupeleka kwingine.

Mngetundea haki zaidi kama mngeanzisha thread nyingine juu ya mgombea ubunge kutoijua vizuri katiba!

Thread za JF zina evolve, huwezi kuwa na threads static, uta defeat maana ya forum. You are trying to herd cats anyway, the internet does not work that way.
 
Umevipitia vifungu vya katiba nilivyoweka na unaweza kubase criticism kutoka katika katiba?

Katiba imesema wazi kwamba waziri hapotezi uwaziri kwa bunge kuvunjwa, na in fact rais anaweza hata kumteua mbunge yeyote wa bunge lililovunjwa ambaye hakuwa waziri, kuwa waziri mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa. Kwa hiyo hata mtu kama Malecela ambaye hakuwa waziri katika bunge lililopita, anaweza kuteuliwa kuwa waziri, unataka iwe explicit kivipi zaidi ya hivyo ?
Mkuu, nimevipitia upya. Uko sahihi kabisa. Sijui kwanini hili liliniruka.

Kwa faida ya wengine, nadhani ni vyema niviweke hapa (vinajitosheleza).

57.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri
utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lo
lote kati ya mambo yafuatayo:-

(a) endapo mwenye madaraka atajiuzulu au kufariki
dunia;
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge
kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa
Bunge;
(c) ikiwa Rais atafuta uteuzi na kumuondoa kazini
mwenye madaraka hayo;
(d) iwapo atachaguliwa kuwa Spika;
(e) iwapo Waziri Mkuu atajiuzulu au kiti chake kikiwa wazi
kwa sababu nyingine yoyote;
(f) ukiwadia wakati wa Rais mteule kushika madaraka ya
Rais basi mara tu kabla Rais mteule hajashika
madaraka hayo;
(g) iwapo Baraza la Maadili linatoa uamuzi unaothibitisha
kwamba amevunja Sheria ya Maadili ya Viongozi wa
Umma.
 
NB

57.-(1) Muda wa kushika madaraka ya Waziri na Naibu Waziri utaanza tarehe atakapoteuliwa kushika madaraka hayo.
(2) Kiti cha Waziri au Naibu Waziri kitakuwa wazi litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo:-
...........
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;

Kifungu kinamaanisha Waziri haaachi kuwa waziri kwa sababu bunge limevunjwa.

Kama watu wanalalamika kwamba katiba ina vifungu vinavyoonekana kuwa contradictory, then kitu cha kufanya ni kurekebisha katiba. Lakini huwezi kusema "the constitution is unconstitutional" . Unless otherwise stated, hakuna sehemu moja ya katiba iliyo na primacy over sehemu nyingine.

Majaji walioamua kesi ya kuhusu ugombea binafsi wamesisitiza hili walipotoa uamuzi wao na kulitaja kama sababu mojawapo iliyowafanya wasiamue kesi na kuirudisha bungeni.

Na kwa sababu katiba yetu haina sehemu moja iliyo na primacy juu ya nyingine, huwezi kusema ile rule ya kwamba "mawaziri watateuliwa miongoni mwa wabunge" ina primacy inayokuwa violated na exception iliyotolewa kwamba:-

"bunge likishavunjwa, na kabla ya kuapishwa kwa bunge jipya, mawaziri wataendelea kuwa mawaziri na rais anaweza hata kuchagua mawaziri wapya kutoka katika watu ambao walikuwa wabunge wa bunge lililovunjwa, na mawaziri hawa wataendelea kuwa mawaziri mpaka bunge jipya liapishwe na mawaziri wapya waapishwe "

Hatuna sehemu inayosema kwamba hii ni cardinal rule yenye primacy over the other parts of the constitution, so let's not act like we have such a primacy.
 
Japo swala lenyewe lipo wazi mno (Mwanakijiji hupenda kutengezea mada zenye tafrani za bandia labda akipungukiwa mada za makala) niseme ni Wanasheria wachache sana wana ufasihi wa udadavuzi wa maswala ya Kikatiba na sheria kama ulivyofanya hapo, ahsante.

Hebu fikiria, Mahakama Kuu ilikubaliana na hoja inayosema "Katiba inavunja Katiba." Na Wanasheria wote wenye vipasa sauti mjini wakasema hukumu ya Mahakama ya Rufaa imekosewa. Eti wangependa jaji aweze kufuta kipengele cha Katiba asichokipenda.

Ila niongeze moja ambalo unaweza kuwa unakosea, maana mimi na wewe hatulegezeani wala hatudekezani kwenye udadavuzi: si sahihi kusema kuna kitu kilifanya Mahakama ya Rufaa "isiamue kesi na kuirudisha Bungeni." Waliamua kesi. Ilitangua uamuzi wa Mahakama za chini. Na hawakurudisha kitu Bungeni, kesi haikutoka Bungeni. Walichokisema kuhusu Bunge ni mazungumzo baada ya habari muhimu, wanaita kisheria "dicta," hakitusaidii chochote kiamri, hawakuliamuru Bunge chochote, walishauri tu. Walisema wanasikitishwa na sheria ya mgombea huru, lakini hawana nguvu ya kuandika upya Katiba. Na walikua sawa.

Na wewe uko sawa sawia unaposema kwenye Katiba yetu hakuna kipengele kizito kuliko chenzake.
 
I hope wewe siyo mmoja wa hao wanasheria wenye "vipasa sauti" mjini na hata mitandaoni, bali ni miongoni mwa wale wachache.
 
Taso keshaanza kuharibu watu...:becky:

Ni yeye pekee aliwezaye hilo... may be if it was that interesting, may be if it wasn't disruptive; sote tungelijaribu na ku-maintain. Else, let her/him rule.
 
Nimegundua kuna watu humu ndani wana Pyschological problem ila hawajijui tu.Nimewasaamehe bure na ninaadhi sitapoteza muda wangu kujibishana nao.Let me concetrate on issues..Home sweet home.Kuwa nyumbani kuzuri jamani...Full kujiachia..
Yaani wewe ni mgombea ubunge upo shallow hivi? huko bungeni unaenda kufanya nini kama hata hiki kisheria kidogo tu cha rais kuachia ngazi pale anapoapishwa? Hivi wabunge wengi wa chadema ni wakookoteza tu? na siajabu wengi ni mambumbumbu ila tu wanataka kuukwaa ubunge. Mimi hapa ndo ninapoona wengi humu wanatumwa na misukumo tu na siajabu hawajui hata wakiandikacho au wakiaminiacho, Except for som few people, including Mwakijiji (with respect) ambaye hoja zake zinamashiko, lakini the rest hata hao wanaojiita wagombea ubunge nivichekesho.
 
Je! kama uwaziri unaisha baada ya bunge kuvunjwa, na kuna kama miezi miwili mitatu kabla ya uchaguzi mpya, ina maana kwa kipindi hicho nchi haitakuwa na mawaziri , in other words nchi inaweza kuendelea bila matatizo bila ya mawaziri, kwa hiyo hakuna sababu ya kuwa na mawaziri in the first place. Wadhifa huo basi ni bora ufutwe - tupunguze gharama za kuwa na hawa watu. .........
 
Back
Top Bottom