Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.

  Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.

  So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Tecnically wabunge bado wanaendelea kuwa wabunge mpaka uchaguzi mpya ufanyike.

  Ukiwapotezea uwaziri wabunge kabla ya uchaguzi mpya utatengeneza leadership vacuum (as if we didn't have one already).
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwa haraka inaweza kuonekana hivyo:

  Lakini ibara ya 55(4) inasema kuwa "(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge."

  Lakini ibara ya 65(2) inasema kuwa uhai wa bunge unakuwepo kuanzia " muda wote unaoanzia tarehe ambapo Bunge jipya limeitishwa kukutana kwa mara ya kwanza baada ya Uchaguzi Mkuu na kuishia tarehe ya kuvunjwa kwa Bunge kwa ajili ya kuwezesha Uchaguzi Mkuu mwingine wa kawaida kufanyika."

  Kwa mujibu wa maelezo ya Spika Bunge lilivunjwa rasmi siku ambapo kipindi cha kampeni kinaanza; na hivyo wabunge wote (bila kujali nafasi zao) walipoteza Ubunge wao; hii ina maana kama mawaziri ni lazima watoke miongoni mwa wabunge na wabunge wamepoteza viti vyao, mawaziri waliopo uwaziri wao wanaupata vipi?

  Na hili pia ni kweli kwa sababu hata ukirejea hiyo ibara ambayo Werema anaidai kuwa na nguvu utaona kuwa inakiri kuwa mawaziri hawawezi kuendelea kuwa mawaziri wakati wamepoteza Ubunge isipokuwa kama wameteuliwa katika mazingira fulani (Ibara ya 90 nayo inashuhudia hili) kwa mfano nchi ikiwa Vitani na kunahitajika uundwaji wa serikali basi Rais anaweza kuwateua waliokuwa wabunge katika Bunge lililopita kushika mawaziri.

  Ndiyo maana inasema "Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa."

  Kwa maneno mengine, Rais alitakiwa kulingana na mazingira ya ibara ya 90 kufanya uteuzi wa mawaziri wapya baada ya Bunge kuvunjwa. Hajafanya hivyo.

  Kipengele ambacho Wereme anakitumia yaani Ibara ya 57(2b) kwamba Waziri atapoteza nafasi yake "ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;" amekipa tafsiri isiyo sahihi kwani inasema kile ninachokisema kwamba njia ya kawaida ya kupoteza uwaziri ni bunge kuvunjwa; lakini mtu anaweza kupoteza uwaziri kabla ya Bunge kuvunjwa. Yaani, Ukiondoa sababu ya Bunge kuvunjwa Waziri bado aweza kupoteza uwaziri wake. Nadhani Kiswahili kimempiga chenga msomi wetu.


  Jaji Werema amekosea. At least according to moi!
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0

  Hata mimi nashangaa.Hata Kikwete kuendelea kuitwa Rais mi bado sielewi..
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kesi ya Rais haina tatizo kwa sababu Urais haupotezwi kwa Bunge kuvunjwa ila siku Rais mpya anapoapishwa.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Interpretation ya Jaji Werema, kutoka mhimili unaotoa tafsiri ya katiba kisheria, hii hapa.

   
 8. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Dada kuna wengine tuishasema usiyoelewa mbona mengi sana tu na unahitaji exposure zaidi.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  hapana.. mhimili unaotoa tafisi ya sheria ni Mahakama na Werema siyo sehemu ya Mahakama ni sehemu ya Executive kama Mwanasheria Mkuu. Lakini ukisoma ibara nzima ya 57 utaona kuwa inasupport my assertion and not his.
   
 10. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,305
  Trophy Points: 280
  Wacha kukoromea watu hapa...hii ni mijadala ya kuelimishana! Wewe unajua yote? Pengine ndivyo unavyojidanganya!
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Asante kwa kunielewesha Mkuu nilikuwa silijui hili.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Are you serious unaposema Jaji si sehemu ya mahakama ?

  Hahaha, unajua Tanzania tuna mambo ya ajabu sana. Hapa kuna a very big potential conflict of interest.

  Hivi imekuwaje Kikwete akamteua Jaji, mtetezi wa judiciary, aende kuwa A.G, mtetezi wa executive ? This is a big no no.

  Na huyu Jaji naye kakubali appointment tu, sasa anapoongea na kuitwa A.G Jaji Werema watu wanakuwa wanajiuliza anaongea kama nani ?

  Kuna wakati Jaji Edward Mwesiumo alikuwa Mbunge, Jaji na Naibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Mtu mmoja huyo huyo yupo katika legislature, executive na judiciary. Ingekuja showdown kati ya mihimili hii mitatu sijui ange resolve vipi conflicts of interest.

  Katiba hii hapa

  http://www.tanzania.go.tz/images/katibamuungano.pdf

  Wabunge wa bunge lililovunjwa, kabla ya kuchaguliwa bunge jipya, hata wale ambao hawakuwa mawaziri wanaweza kuteuliwa kushika nafasi ya uwaziri, implying kwamba uwaziri unaweza kushikwa by virtue ya mtu kuwa mbunge katika bunge lililovunjwa in the interim before a new parliament is elected.

  Tunachoshindwa kuelewa, au kukataa kukubali, ni kwamba hawa watu waliokosa ridhaa ya kuwakilisha wananchi wamekosa ridhaa hii kwa bunge lifuatalo, na ingawa bunge lililopita limekwishavunjwa, rais ana uwezo hata wa kuwateua watu ambao hawakuwa mawaziri kushika uwaziri kwa nguvu yao ya kwamba walikuwa wabunge katika bunge lililopita mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa.

  Ukisema katiba ina walakini unaweza kuwa na point, lakini ukisema Mawaziri hawa hawafai kuwa mawaziri kwa sababu si wabunge, na kwamba kuna violation ya katiba, utashangaza watu kwa sababu katiba yenyewe imetoa provision wabunge wa bunge liliopita walio mawaziri kuendelea kuwa mawaziri, na hata kumpa uwezo rais kuteua mawaziri wapya miongoni mwao, in the interim.
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kula tano...
   
 14. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Labda mtu akiwa aggressive katika kukataa weak minds na mediocrity, mediocres wengine wenye inferiority complex wanaona kama kuna "kukoromeana"

  La uvundo halina ubani.
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Aug 23, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kiranga bana mbona uko hivyo mazee...yaani mchokozi chokozi tu.....

  Unajua nataka siku nishuhudie makutano yako na Regia...sijui yatakuwaje tu...sijui nani ataanza kumwongelesha mwenzake....sijui mtasema nini....
   
 16. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Siyo uchokozi mazee, ni zero tolerance for bs tu, sasa hatuwezi kutaka kutoa bs moja kwa kupandikiza bs nyingine.Kama mtu hana uwezo hana uwezo tu.
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Aug 23, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ila kwa nini wabunge wasiendelee kuwa wabunge hadi siku ambayo wabunge wapya wataapishwa? Hii itaondoa huu mkanganyiko ulioko sasa. Maana kila mtu anakuja na tafsiri yake wakati mimi naona ni jambo rahisi tu.

  Wakati mwingine tuna complicate mambo ambayo hayako complicated kabisa.
   
 18. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #18
  Aug 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Nimegundua kuna watu humu ndani wana Pyschological problem ila hawajijui tu.Nimewasaamehe bure na ninaadhi sitapoteza muda wangu kujibishana nao.Let me concetrate on issues..Home sweet home.Kuwa nyumbani kuzuri jamani...Full kujiachia..
   
 19. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nimegundua hili, ila sijawasamehe. Kuwasamehe ni uhaini.

  Watu wana psychological problems zinazowafanya wajione wanaweza hata yale wasiyoweza, ego hizi zinawafanya waende kugombea nafasi zenye dhamana kubwa kwa umma huku wakifikiri "mtu yeyotte anaweza kuwa mbunge" na kusema hivi wazi wazi.

  Bora hata miye nikiwa na psychological problems nikabwabwaja hapa JF impact yangu ndogo, unaweza kuni ignore tu. Watu wenye psychological problems za kujiona wanaweza vitu wasivyoweza wakiweza kuingia katika kazi zenye dhamana ya wananchi watatuharibia mambo makubwa sana.

  Wewe mtu unaenda kugombea ubunge hujui hata katiba inasemaje kuhusu urais na unavyoathiriwa na kuvunjwa kwa bunge, wewe uko serious kweli au unacheza cheza tu?

  Watu wakikwambia huko seroius kweli utasema wanakuonea ?
   
 20. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #20
  Aug 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,185
  Trophy Points: 280
  Yeah, this would be the easiest solution.

  Nafikiri wanataka kutengeneza a level playing field katika kampeni za ubunge, sio mtu anaenda kugombea ubunge wakati akiwa mbunge.

  Which would make sense if they had a similar set up for the presidency, although an argument can be made that doing the same for the presidency, due to the central nature of the presidency, would create a counterproductive power vacuum. I believe this is their reasoning.
   
Loading...