Regia Mtema
R I P
- Nov 21, 2009
- 2,970
- 873
ooh Nyani Ngabu umenitoroka.
Hata mimi nashangaa.Hata Kikwete kuendelea kuitwa Rais mi bado sielewi..
kesi ya Rais haina tatizo kwa sababu Urais haupotezwi kwa Bunge kuvunjwa ila siku Rais mpya anapoapishwa.
Asante kwa kunielewesha Mkuu nilikuwa silijui hili.
Mkuu haukupaswa kukiri kutofahamu hili, angalia usije ukawakatisha tamaa wafuasi wako.
Sijui kipindi hiki hawa mawaziri utaona plate number za magari yao zimebadilishwa na zinatumia STK na sio zile plate number za mawaziri
Je kisheria katika kipinid hiki kuna vitu hawawezi kufanyia maamuzi? Je Kuna stahili zao zinapunguzwa? Wataaalam nielimisheni
Ukifuatilia mfululizo na kusoma vifungu vya katiba utaona mawaziri wanaendelea kuwa mawaziri na wana nguvu zote za kiwaziri mpaka baraza jipya la mawaziri litakapotangazwa na kuapishwa rasmi.
Sijui kipindi hiki hawa mawaziri utaona plate number za magari yao zimebadilishwa na zinatumia STK na sio zile plate number za mawaziri
Je kisheria katika kipinid hiki kuna vitu hawawezi kufanyia maamuzi? Je Kuna stahili zao zinapunguzwa? Wataaalam nielimisheni
Kwa sababu si mawaziri
hakuna jambo lolote wanaloweza kufanya wakiwa ni mawaziri ni kinyume na katiba.. tngekuwa na able opposition ingefunguliwa mara moja kesi ya Kikatiba kwani hawa jamaa wanatumia madaraka wasiyokuwa nayo unless kama tumetangaziwa kuwa Jamhuri iko vitani na Rais kawateua kutekeleza mambo fulani. Nje ya hapo wanatuibia huku tunawaangalia. Matokeo yake Masha anafikiria bado ana cloud na mambo ya ndani na Ngeleja anafikiria kuwa yeye bado ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje.
Kwa sababu kama siyo wabunge wameweza vipi kuwa Mawaziri?
(b) ikiwa mwenye madaraka hayo atakoma kuwa Mbunge kwa sababu yoyote isiyohusika na kuvunjwa kwa Bunge;
KirangaDada kuna wengine tuishasema usiyoelewa mbona mengi sana tu na unahitaji exposure zaidi.
Ukifuatilia mfululizo na kusoma vifungu vya katiba utaona mawaziri wanaendelea kuwa mawaziri na wana nguvu zote za kiwaziri mpaka baraza jipya la mawaziri litakapotangazwa na kuapishwa rasmi.
Watu wameweka vifungu vya katiba na kuvielezea, sasa unataka kuelimishwa zaidi vipi mkuu wangu ?
Are you serious unaposema Jaji si sehemu ya mahakama ?
Hahaha, unajua Tanzania tuna mambo ya ajabu sana. Hapa kuna a very big potential conflict of interest.
Hivi imekuwaje Kikwete akamteua Jaji, mtetezi wa judiciary, aende kuwa A.G, mtetezi wa executive ? This is a big no no.
Na huyu Jaji naye kakubali appointment tu, sasa anapoongea na kuitwa A.G Jaji Werema watu wanakuwa wanajiuliza anaongea kama nani ?
Kuna wakati Jaji Edward Mwesiumo alikuwa Mbunge, Jaji na Naibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani. Mtu mmoja huyo huyo yupo katika legislature, executive na judiciary. Ingekuja showdown kati ya mihimili hii mitatu sijui ange resolve vipi conflicts of interest.
Wabunge wa bunge lililovunjwa, kabla ya kuchaguliwa bunge jipya, hata wale ambao hawakuwa mawaziri wanaweza kuteuliwa kushika nafasi ya uwaziri, implying kwamba uwaziri unaweza kushikwa by virtue ya mtu kuwa mbunge katika bunge lililovunjwa in the interim before a new parliament is elected.
Tunachoshindwa kuelewa, au kukataa kukubali, ni kwamba hawa watu waliokosa ridhaa ya kuwakilisha wananchi wamekosa ridhaa hii kwa bunge lifuatalo, na ingawa bunge lililopita limekwishavunjwa, rais ana uwezo hata wa kuwateua watu ambao hawakuwa mawaziri kushika uwaziri kwa nguvu yao ya kwamba walikuwa wabunge katika bunge lililopita mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa.
Ukisema katiba ina walakini unaweza kuwa na point, lakini ukisema Mawaziri hawa hawafai kuwa mawaziri kwa sababu si wabunge, na kwamba kuna violation ya katiba, utashangaza watu kwa sababu katiba yenyewe imetoa provision wabunge wa bunge liliopita walio mawaziri kuendelea kuwa mawaziri, na hata kumpa uwezo rais kuteua mawaziri wapya miongoni mwao, in the interim.
Sababu ingine ya mwaziri kutopaswa kuwa wabunge.
Yaani vitu vyepesi vyepesi tu lakini tuna vi complicate wenyewe.
Wabunge wanaweza kufanya kampeni wakati bunge likiwa kwenye recess huku baraza la mawaziri likiendelea kuwepo na kufanya kama kawaida hadi hapo litakapoundwa jingine na mawaziri wapya kuapishwa. Simple as that.
Mazee nimeweka vifungu vya katiba vinavyoonyesha kwamba kuvunjwa kwa bunge sio msingi wa uwaziri kuisha, kama unavyo vingine vinavyosema tofauti, kwamba kuvunjwa kwa bunge ni msingi wa uwaziri kuisha tuwekee hapa tuelimike zaidi.
Ngeleja kawa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kuanzia lini ? Afikiri yeye Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwa sababu gani ?
Katiba imesema wazi kuhusu grounds za Waziri kuacha kuwa waziri
Meaning kwamba Waziri haachi kuwa Waziri kwa sababu ya kuvunjwa kwa bunge.
Sasa tuonyeshe unaposema wewe basi tujue argument yako ina ammunition gani.
sasa hivi Bunge halipo kwenye recess. Bunge limevunjwa, hakuna Spika, hakuna wabunge hakuna mawaziri.
Oh wait....ningependa kujua kama hao wabunge walio mawaziri bado wanaendelea kulipwa mishahara yao....
Kianga
Mengi yapi asiyiayelewa dada wa watu
siasa, sheria, kilimo, biashara, michezo utamaduni, kazi, katiba. jaribu kumsaidia wapi apige msasa zaidi maaana binafsi naona dada yetu ana kiu ya kujua mengi.
Regia usikate wale kukatishwa tamaa hizo ni constructive criticism. Unaweza kujaribu kuiga mbinu hii. Google it kabla. Nadani part ya exposure anayosema kiranga itapata dawa.