Kiranga,
Unachokifanya hapa bodini dhidi ya Regia ni "BULLYING".
You should know better; please stop it.
Unaweza kufafanua bullying iko wapi? Kila kitu kina source, mostly mwenyewe Regia. Kama unabisha sema Kiranga umefanya bullying hapa, nikuonyeshe nimepata wapi hayo mawazo.
Moja ya matatizo yetu makubwa kama jamii na nchi ni kwamba hatutaki kuambiana ukweli, hatutaki ukweli hasa kama hatuupendi.Wengi wetu najua ni wakereketwa wa mageuzi, na tungependa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani viongeze wabunge, na hata kushinda urais. Hata mimi pia ningependa hili, lakini hili halimaanishi nikubali mtu asiye uwezo anapita mbele ya macho yangu kutaka kuingia bungeni, nitasema ukweli dhidi ya CCM, na nitatumia kanuni hizo hizo kuusema upinzani.
Upinzani una uungu gani mpaka uwe juu ya kukosolewa ?
Kwangu mimi, JF ni soko la mawazo, na kila mtu yuko huru kutoa mawazo yake, na kila kitu ili kiheshimiwe inabidi kiwe na source ya kukiback, sasa niambie hiyo bullying iko wapi na kitu gani kikufanyacho unione mimi ni bully tu na sio whistleblower anayesema kweli.
Ili kuendelea tunahitaji ushindani, sio ushindani kati ya CCM na upinzani tu, bali hata katika upinzani kuwe na mawazo tofauti yanayoruhusiwa kushindana. Kanuni hii hii inayotufanya tupende upinzani kati ya CCM na CHADEMA itufanye tupende kuona ushindani wa mawazo kati ya watanzania na upinzani, upinzani na upinzani, na CHADEMA na CHADEMA. Upinzani/ ushindani huu si mbaya, ni kitu tunachohitaji ili kuendelea. Maendeleo si kucheza lelemama, maendeleo yanataka kuumiza vichwa, yanataka ukiweka claim kwamba "Kiranga ni bully" uje na supporting evidence, hii na hii na hii, watu watakuelewa.Ama sivyo utaonekana mpambe wa Regia tu asiyependa watu waseme ukweli.
Ushindani huu wa kuwabana wapinzani na kutaka wafanye vizuri zaidi unaweza kuzaa mambo ya manufaa kwa taifa letu kiujumla kama mambo tunayosema hapa yatatiliwa maanani na watu tunaowasema na vyama vyao.
Hata mfalme wa Roma, Marcus Aurelius, alipokuwa akiranda mitaa ya Roma na kuamkuliwa kwa salamu zote zimfaazo mfalme mwenye bashasha zote kutoka kwa waja wake - nyingine bila shaka za kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa-, alikodi mtumwa mmoja kutembea nyuma yake karibu kabisa naye.Kazi ya mtumwa huyu ilikuwa ni moja tu, kumnong'oneza mfalme kwa karibu na kumwambia "Respica te, hominem te memento" ("Look behind you, remember you are only a man") na "Memento mori" ("Remember (that you are) mortal").
Regia na CHADEMA ni miungu gani hawa mpaka wasionyeshwe wanapofanya vibaya ? Miungu wapya hawa wameshushwa kwa msahafu gani huo ambao sijauona miye ? Analects? Torat? Quran? Baghavad-Gita ? Rig-Veda ? Dhammapada ? Talmud ? Tripitaka? The Bible ? The Egyptian Book of The Dead ? Zhuan Falun? The Book of Mormons? Kebra Negast ? The Communist Manifesto ? Mbona sikuyaona habari hizi kote huko ?
Mimi hapa kazi yangu ni kama huyu mtumwa wa Marcus Aurelius - tena bila malipo- CHADEMA wanapopandishwa kichwa na wafuasi wao wasioangalia hali halisi, mimi nawakumbusha mortality yao, nawaonyesha ninachofikiri si sawa, tena nawaonyesha hakuna chama chenye monopoly ya JF, nawaonyesha kwamba ingawa tunapenda mageuzi, kuna watu tunaheshimu kanuni na hatuwezi ku suspend kanuni eti kwa sababu tu huyu ni mgombea wa CHADEMA, kama tunakemea mediocrity CCM tutakuwa watovu wa uungwana na wengi wa hiyana kama hatutatanabahi ubaya wa kutokemea mediocrity CHADEMA. Hata kama tunaipenda CHADEMA, tunaipenda Tanzania zaidi.
Na tunaheshimu ukweli usiobadilika kwa kumuangalia mtu. Hatuwezi kuwa na double standards, eti set moja ya standards kwa CCM na kina Sophia Simba, na nyingine tofauti kwa CHADEMA na kina Regia Mtema, huu utakuwa unafiki.
Again, hebu nioneshe nimekuwa bully katika kipande gani nikuonyeshe kwamba siongei kufurahisha baraza tu, nikupe vielelezo, vingi sana kutoka kwa Regia mwenyewe.