Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

Mmepoteza Ubunge kwanini bado ninyi mawaziri?

mmh.. HAKUNA wabunge, so hakuna mawaziri anything nje ya hapo ni kuibiana.

Sawa nimekuelewa ila ningependa kujua kama jamaa (mawaziri) wanaendelea kuchukua mshiko na perks zingine zinazoendana na kazi zao. Do you know if they do?
 
Whatever the case hoja yangu bado iko pale pale kuwa hakuna ulazima wa mawaziri kuwa wabunge na pindi bunge livunjwapo basi hata uwaziri wao unakoma.

Kwa hiyo kama hakuna mawaziri ina maana basi hata serikali kwa namna fulani haipo, si ndio? Kwa hiyo tupo tupo tunaeleaelea...

hapana serikali ipo kwa sababu serikali haitegemei uwepo wa moja kwa moja wa mawaziri ndio maana Rais bado yupo. Kumbuka Mawaziri ni wasaidizi tu wa Rais kwani madaraka yote ya utendaji yamo mikononi mwa Rais. Yaani, katiba iko wazi kwamba hata yale mambo ambayo rais amempa waziri kushughulikia haina maana yeye mwenyewe anazuiliwa kuyafanya. Ndio maana wakati mwignine Rais anaweza kuachilia baadhi ya wizara mikononi mwake yeye mwenyewe. Kwenye nchi nyingine utaona Rais ndiyo Waziri wa Ulinzi vile vile.

Hakuna wakati ambapo hatuna serikali; ndio maana hata Rais akiwa anaapishwa say Rais mpya anakuja (in this case Dr. Slaa) basi pale atakapoapishwa tu Dr. Slaa wateule wote wa Rais (ukiondoa wa kada fulani) wanapoteza madaraka yao. Lakini Mawaziri wanakuwa wameshapoteza uwaziri pale Bunge lilipovunjwa.
 
Sawa nimekuelewa ila ningependa kujua kama jamaa (mawaziri) wanaendelea kuchukua mshiko na perks zingine zinazoendana na kazi zao. Do you know if they do?

I really don't ila kama wanaamini bado ni mawaziri na wabunge basi watalipwa kama kawa!
 
mmh.. HAKUNA wabunge, so hakuna mawaziri anything nje ya hapo ni kuibiana.

Unataka kulazimisha wakati nimekuwekea vifungu vinavyosema wazi kwamba mtu hahitaji kuwa mbunge ili kuwa waziri, na mtu anaweza kuteuliwa kuwa waziri by virtue ya kuwa alikuwa mbunge katika bunge lililovunjwa kabla bunge jipya halijachaguliwa.

Katiba yenyewe ndiyo inahitaji kuacha kuwa na vifungu vinavyohitaji qualifications ( kama kusema kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa, halafu ku qualify hili kwa kusema wanaochaguliwa ni lazima wawe wanachama wa vyama vya siasa)

Mawaziri wanaendelea kuwa mawaziri mpaka baraza jipya la mawaziri litakapoapishwa baada ya bunge jipya kuchaguliwa, kuvunjwa kwa bunge si ground ya waziri kupoteza uwaziri, kama mnataka kuoperate na katiba yetu ya sasa katiba imesema hili wazi, kama mnataka kuleta katiba yenu nyingine ikatae hili labda mnaweza kueleweka.
 
hapana serikali ipo kwa sababu serikali haitegemei uwepo wa moja kwa moja wa mawaziri ndio maana Rais bado yupo. Kumbuka Mawaziri ni wasaidizi tu wa Rais kwani madaraka yote ya utendaji yamo mikononi mwa Rais. Yaani, katiba iko wazi kwamba hata yale mambo ambayo rais amempa waziri kushughulikia haina maana yeye mwenyewe anazuiliwa kuyafanya. Ndio maana wakati mwignine Rais anaweza kuachilia baadhi ya wizara mikononi mwake yeye mwenyewe. Kwenye nchi nyingine utaona Rais ndiyo Waziri wa Ulinzi vile vile.

Hakuna wakati ambapo hatuna serikali; ndio maana hata Rais akiwa anaapishwa say Rais mpya anakuja (in this case Dr. Slaa) basi pale atakapoapishwa tu Dr. Slaa wateule wote wa Rais (ukiondoa wa kada fulani) wanapoteza madaraka yao. Lakini Mawaziri wanakuwa wameshapoteza uwaziri pale Bunge lilipovunjwa.

Maelezo maridhawa kabisa haya.
 
Kwa kweli kuna ulazima wa hii katiba kuandikwa upya maana yaelekea hata sisi wenyewe hatuielewi vizuri na ndio maana kunakuwa na tafsiri mbalimbali.

Mambo kama haya ya uwaziri na ubunge yalitakiwa yawe ya kueleweka moja kwa moja bila hata tafsiri.
 
mi naona sarakasi tu sikuhizi na mambo yanavyokwenda...
 
Unataka kulazimisha wakati nimekuwekea vifungu vinavyosema wazi kwamba mtu hahitaji kuwa mbunge ili kuwa waziri, na mtu anaweza kuteuliwa kuwa waziri by virtue ya kuwa alikuwa mbunge katika bunge lililovunjwa kabla bunge jipya halijachaguliwa.

Ibara ya 55(4) - Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.

Huwezi kuwa Waziri kama si Mbunge.

Mawaziri wanaendelea kuwa mawaziri mpaka baraza jipya la mawaziri litakapoapishwa baada ya bunge jipya kuchaguliwa, kuvunjwa kwa bunge si ground ya waziri kupoteza uwaziri

Of course it is... kwa sababu kama wabunge wanapoteza ubunge kwa Bunge kuvunjwa inakuwaje uwe na mawaziri wakati qualification ya lazima ni kuwa ili uwe waziri lazima uwe mbunge?

kama mnataka kuoperate na katiba yetu ya sasa katiba imesema hili wazi, kama mnataka kuleta katiba yenu nyingine ikatae hili labda mnaweza kueleweka.

katika hili katiba yetu wala haina tatizo. Huwezi kuwa waziri kama si mbunge na Bunge linapovunjwa wabunge wanapoteza Ubunge wao na so sifa nyingine zote zinazotokana na ubunge huo yaani pamoja na Uwaziri. Vinginevyo, wabunge wanaweza kudai bado ni wabunge hadi bunge jingine litakapoapishwa. Hili halimo kwenye katiba yetu. Nchi haina wabunge, na hivyo haina mawaziri wala manaibu wao. Very simple.
 
Kiranga:

a. Wabunge wanapoteza Ubunge wao vipi?

b. Ni sifa gani zinamfanya mtu awe Waziri?

a. wabunge wanapoteza ubunge kwa njia nyingi, njia iliyo relevant katika swala letu hapa ni ile ya kuvunjwa kwa bunge.

b. Sifa zinazomfanya mtu kuwa waziri ni nyingi, ikiwamo ya kuwa mbunge, au hata kuwa mtu aliyekuwa mbunge katika bunge lililovunjwa wakati bunge jipya halijaapishwa.

Kwa hiyo utaona, strictly speaking, as long as mtu alikuwa mbunge katika bunge lililovunjwa, na bunge jipya halijachaguliwa/ apishwa, mtu huyu hahitaji kuwa mbunge ili kuwa waziri.

Leo hii Kikwete anaweza kumchagua Malecela kuwa Waziri kikatiba mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa, ingawa Malecela si mbunge kwa sababu bunge lililopita limeshavunjwa (It's ugly, I know, I am not saying it has any semblance of elegancy, but that's not the point being discussed here). Bunge jipya likishaapishwa Malecela anakosa sifa za kuendelea kuwa Waziri (assuming hatachaguliwa kuwa mbunge na wananchi au kupewa special seats) na wabunge wapya wataapishwa kuwa wabunge, kuteuliwa na kuapishwa kama mawaziri.
 
for 'endorse': 1

-ridhia verb Root -ridhi accept, endorse, support, back up, agree, concur, consent, approve, agree to
-ridhi verb consent, approve
kuridhia infinitive Stem -ridhia

Kiranga rudi kule kwenye "endorsement" ya Slaa

Others: sorry for digressing
 
Ibara ya 55(4) - Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.

Huwezi kuwa Waziri kama si Mbunge.

Of course it is... kwa sababu kama wabunge wanapoteza ubunge kwa Bunge kuvunjwa inakuwaje uwe na mawaziri wakati qualification ya lazima ni kuwa ili uwe waziri lazima uwe mbunge?

katika hili katiba yetu wala haina tatizo. Huwezi kuwa waziri kama si mbunge na Bunge linapovunjwa wabunge wanapoteza Ubunge wao na so sifa nyingine zote zinazotokana na ubunge huo yaani pamoja na Uwaziri. Vinginevyo, wabunge wanaweza kudai bado ni wabunge hadi bunge jingine litakapoapishwa. Hili halimo kwenye katiba yetu. Nchi haina wabunge, na hivyo haina mawaziri wala manaibu wao. Very simple.

Hapa mazee ni sawa na kusema "katiba inaruhusu wagombea binafsi kwa sababu imesema Mtanzania yeyote mwenye umri wa miaka 18 asiye na matatizo ya akili na asiyekuwa na rekodi ya kufungwa anstahili kupiga na kupigiwa kura katika chaguzi" bila kuangalia kwamba kuna qualification nyingine imewekwa kwamba "ili kupigiwa kura inabidi mgombea awe anawakilisha chama cha siasa"

Huwezi kuchukua first principle iliyokuwa further qualified, halafu ukataka ku operate kama vile hamna hiyo further qualification. Kama huipendi hii qualification iondoe, usitake kui ignore na kuoperate kama haipo. Badilisheni katiba, msiseme kwamba qualification haipo.

Katiba ikisema "Watanzania wote wanaruhusiwa kusafiri nje ya Tanzania, kasoro Mwanakijiji" huwezi kutaka ku ignore hii sehemu inayosema "kasoro mMwanakijiji" eti kwa sababu sentensi imeanza kwa kusema "Watanzania wote wanaruhusiwa kusafiri nje ya nchi". Ukiona kama kuna contradiction ( hakuna by the way, ndiyo maana kuna neno "kasoro") kama hupendi hii kasoro iondoe, usiseme kwamba haipo.

Bado hujanipa kifungu cha katiba unachotoa mawazo yako.

Una quote 55.4 lakini unaacha ku quote 55.5

(4) Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge.

(5) Bila ya kujali masharti ya ibara ndogo ya (1) ikitokea kwamba Rais anahitajiwa kumteua Waziri au Naibu Waziri baada ya Bunge kuvunjwa, basi aweza kumteua mtu yeyote ambaye alikiwa Mbunge kabla ya Bunge kuvunjwa.
 
for 'endorse': 1

-ridhia verb Root -ridhi accept, endorse, support, back up, agree, concur, consent, approve, agree to
-ridhi verb consent, approve
kuridhia infinitive Stem -ridhia

Kiranga rudi kule kwenye "endorsement" ya Slaa

Others: sorry for digressing

Ku endorse ni active, kuridhia ni passive.
 
Who runs the country during an election campaign in UK ?

..........."Ministers may be out on the stump campaigning but departments continue to send ministerial boxes with papers that need signing.In the case of a serious event - like a terrorist attack - the Cobra emergency committee would still be activated, with relevant ministers present.
However, Cabinet Office guidance states that major policy decisions should be postponed until after the election, provided it "would not be detrimental to the national interest or wasteful of public money".
"It is customary for Ministers to observe discretion in initiating any action of a continuing or long-term character," it states.
MPs - whether new or returning - will not take up their seats in the Commons again until 18 May.
Until then, while the political world is turned upside-down during the pre-election tussle, the electorate need not quite expect the rest of the country to descend into chaos.

Read the full article at BBC News - Who runs the country during an election campaign?
Our Colonial master ambao kwa kiasi kikubwa tunafuata mfumo wao wa wa sheria a utawala wanafanya hivyo.
 
kesi ya Rais haina tatizo kwa sababu Urais haupotezwi kwa Bunge kuvunjwa ila siku Rais mpya anapoapishwa.

Lkna kipindi anachogombea Rais anatakiwa awe 'lame-duck';asiruhiswe kuteua mtu wala kutoa directives ili kuondoa mabadiliko yasiyo na lzm akija kuangushwa kwenye kinyang'anyiro hicho!Anyways kwa hilo inabidi kwanza tubadili katiba!
 
Huwezi kuwa Waziri kama si Mbunge.
Huwezi kuteuliwa Waziri kama si Mbunge.

...Home sweet home.Kuwa nyumbani kuzuri jamani...Full kujiachia..
We dada unagombea ubunge unaongelea mambo ya ''full kujiachia" si vema maana hutachukuliwa kiumakini. Ungetulia kwanza na hizo lugha, tayari una kashfa ya kutumia tarakishi za CHADEMA au ofisi au muda wako kutafuta wanaume mitandaoni ambao hawakutaki kwa sababu tayari wana wenzao. Haipendezi.

Mtakumbuka niliwahi kuanzisha masa hapa ikisomeka"nimempenda mtu nisiyemfahamu-sijawahi kumuona" ...jamaa akachomoa,nikaendelea kuvumilia na kuendelea kumsisitiza,hivi karibuni ameniambia ana mtu,nimeumia sana kwani nilkuwa najifariji huenda akawa hana mtu...Kifupi ni kwamba kanitolea nje..Nampenda..Niko njia panda sijui nifanyeje.....
 
Huwezi kuteuliwa Waziri kama si Mbunge.

We dada unagombea ubunge unaongelea mambo ya ''full kujiachia" si vema maana hutachukuliwa kiumakini. Ungetulia kwanza na hizo lugha, tayari una kashfa ya kutumia tarakishi za CHADEMA au ofisi au muda wako kutafuta wanaume mitandaoni ambao hawakutaki kwa sababu tayari wana wenzao. Haipendezi.

Dang son,

Kumbe watu kwa extra curricular activities hawajambo. No wonder. Anayevuma Sophia Simba kumbe wengine wamo.
 
Tangu wiki iliyopita mwishoni na hata leo nimeendelea kusikia ati "Waziri" fulani kafanya jambo hili au lile. Hivi Mwanasheria Mkuu hawezi hata kutoa maelekezo kuwa sasa hivi nchi haina mawaziri au waziri mkuu? Baada ya Bunge kuvunjwa rasmi kwa kuanza kampeni ya uchaguzi Augusti 20 wabunge wote walipoteza ubunge wao na hivyo waliokuwa mawaziri nao wamepoteza uwaziri wao. Haijalishi kama baadhi yao wamepita bila "kupingwa" lakini siyo wabunge hadi siku watakapoapishwa.

Hivyo, aidha Rais Kikwete awateua baadhi yao na kuwaapisha kuwa mawaziri sasa kwa mujibu wa katiba (japo sioni haja ya kufanya hivyo) ama wale wote wanajiona ni bado "mawaziri" wapigwe makonzi na kuambiwa waondokane na fikra hizo kwani wao siyo mawaziri na uhondo wote na madaraka yao ya uwaziri hayapo sasa na wizara zao ziko chini ya Makatibu Wakuu.

So.. sitaki kusikia chombo cha habari kinatuambia ati "Waziri wa Ulinzi na JKT Dr. Hussen Mwinyi" amefanya hili au lile au "Waziri wa Nishati Bw. William Ngeleja amefungua". Hawa watu SIYO MAWAZIRI!!!!!!!!!!!!!!!

Raisi ajavunja baraza la mawaziri, kwa hivyo hawa wanaendelea kuwa mawaziri mpaka baraza la mawaziri livyunje na maraza lingine liundwe na Raisi mtarajiwa akisaidiana na waziri mkuu mtarajiwa..
 
Huwezi kuteuliwa Waziri kama si Mbunge.

We dada unagombea ubunge unaongelea mambo ya ''full kujiachia" si vema maana hutachukuliwa kiumakini. Ungetulia kwanza na hizo lugha, tayari una kashfa ya kutumia tarakishi za CHADEMA au ofisi au muda wako kutafuta wanaume mitandaoni ambao hawakutaki kwa sababu tayari wana wenzao. Haipendezi.

you guys give the poor girl a break.

mlijuaje kama ulikuwa muda au tarakishi za chadema? hana lunch break? hana internet yake binafsi? hana likizo na kutumia kufanya hicho alichokifanya?

alipofanya hivyo alikuwa gender sensitive na si regia mtema na wala alikuwa hajatangaza nia ya kugombea ubunge bado.

mhukumuni kwa aliyoyafanya baada ya kutangaza nia (japo kuwa sidhani kama inaweza kumsaidia sana kwa kuwa haonyeshi mabadiliko ya kabla na baada) :confused2:
 
a. wabunge wanapoteza ubunge kwa njia nyingi, njia iliyo relevant katika swala letu hapa ni ile ya kuvunjwa kwa bunge.

b. Sifa zinazomfanya mtu kuwa waziri ni nyingi, ikiwamo ya kuwa mbunge, au hata kuwa mtu aliyekuwa mbunge katika bunge lililovunjwa wakati bunge jipya halijaapishwa.

Kuwa mbunge ni SIFA YA LAZIMA: Katiba inasema mawaziri wote ni lazima watokane na wabunge. Period.

Kwa hiyo utaona, strictly speaking, as long as mtu alikuwa mbunge katika bunge lililovunjwa, na bunge jipya halijachaguliwa/ apishwa,

Kuna mazingira ya Kikatiba ambapo Rais anaweza kuteua mtu ambaye si mbunge kuwa Waziri (lakini lazima awe mtu aliyekuwa Mbunge katika Bunge lililopita). Mazingira hayo yameanisha katika ibara ya 90. Kwamba Jamhuri iko vitani au kuna jambo ambalo linalazimu Rais aunde serikali. Sasa hivi hakuna na nilazima Rais "ateue" siyo wao "waendelee" kuwa mawaziri kana kwamba hawakupoteza ubunge wao.

mtu huyu hahitaji kuwa mbunge ili kuwa waziri.

Ndio lakini katika mazingira fulani si kwamba anaendelea kuwa Waziri wakati Bunge limevunjwa.

Leo hii Kikwete anaweza kumchagua Malecela kuwa Waziri kikatiba mpaka hapo bunge jipya litakapoapishwa, ingawa Malecela si mbunge kwa sababu bunge lililopita limeshavunjwa (It's ugly, I know, I am not saying it has any semblance of elegancy, but that's not the point being discussed here).

"Hivi leo" hawezi kwa sababu hakuna mazingira ya kuteua mtu kuwa Waziri bila kuwa Mbunge. Na unaposema kuteua maana yake, si kwamba waliokuwepo wanaendelea kuwa mawaziri.

Bunge jipya likishaapishwa Malecela anakosa sifa za kuendelea kuwa Waziri (assuming hatachaguliwa kuwa mbunge na wananchi au kupewa special seats) na wabunge wapya wataapishwa kuwa wabunge, kuteuliwa na kuapishwa kama mawaziri.

Kuna mazingira ya Rais kuteua watu nje ya Bunge na mazingira hayo hayapo kwa sasa.
 
Back
Top Bottom