Mlolongo wa Ajali za Barabarani Tanzania 2007-2011

Nakubaliana na wewe,maana serikali imekaa kimya kama hakuna kitu kinaendelea.Wana ogopa maana wakienda kwenye ofisi zao wanaona mwenye bus kapiga picha na mkuu
Labda ndio mwisho wa dunia unaanzia tanzania,waarabu wakiwa facilitators. Nadhan serikali iko usingizini,wanahitaji kuamshwa. Wananchi tujitokeze wenyewe barabarani tuyazuie haya majeneza yasipite tena. Hatuna haja ya kutangulia kwa Muumba kabla ya wakati wetu.
 
Nafungulia Redio One, habari za ajali ya moto zinaishia, majeruhi ni wengi na hakuna msaada wa vyombo husika vya huduma za dharura, mwenye habari kwa kina atujuze
 
Na kuna hbr ya basi la Hood kugongana uso kwa uso na lori la Mohamed trans na kisa na mkasa ni kila mmoja alitaka kukwepa moshi kubwa iliyokuwa imetanda barabarani ndani ya hifadhi na majeruhi walio mahututi ni kibao sana.
 
Kiangaz hiki,ndio wanapeenda kuchoma moto ili kuwinda,,,,,,wanyama
Na kuna hbr ya basi la Hood kugongana uso kwa uso na lori la Mohamed trans na kisa na mkasa ni kila mmoja alitaka kukwepa moshi kubwa iliyokuwa imetanda barabarani ndani ya hifadhi na majeruhi walio mahututi ni kibao sana.
 
Wana jf,nimepewa habari muda mfupi uliopita kwamba basi la hood toka mbeya kwenda dodoma limepata ajali maeneo ya mikumi,yasemekana limeungua na baadhi ya ndani...
 
Ndo niko hapa du basi la hood limeungua looote na naona maiti moja ikiwa chini imefunikwa na kanga
 
Safari nchini kwetu hasa za njia ya barabara ni hatari tupu. Saa zote unakuwa roho mkononi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa katika hiki kipindi kigumu kwao.
 
Ni karibu na geti la kutokea mikumi national park kama unaenda iringa, hood imegongana na semitrela lenye mafuta ya kupikia...yoote yameunguzwa na moto uliokiwa ukichoma majani huku mbugani. Msururu mrefu wa magari umetanda njia zimefungika, hakukuwa na msaada mpaka nafika na kuondoka sijaona msaada wowote watu wanaangalia tuu magari yanavyo ungua. Nasikia watu wengi wameungua ila sijaweza ona vizuria.nina picha ila ziwezi upload na cm yangu mchina
 
Back
Top Bottom