Taarifa zilizopo ni kuwa Bomu limelipuliwa (hand thrown Grenade) baada ya mhadhara wa ndani ya msikiti huko Unguja na Ndg yetu kijana Muhammad mkombolaguha amefariki dunia, sheikh Abulfadh'li Qassim mlengwa wa shambulio amejeruhiwa mkono na mguu na yu wapata matibabu hospitalini na hali yake sio mbaya sana.
Aliyefariki ni mwanafunzi wa sheikh ktk Markaz iliyopo Tanga, Abulfadh'li ni miongoni mwa masheikh wanaowindwa sana na wanaharakati, mashia na makhawarij wanaopinga msimamo wake ulio sahihi wa kukataza maandamano, kupinga jihad bila ya shurutwi za kisheria, kupinga kukufurisha watu bila ya sababu za kisharia, kutukana na kulaani viongozi waliokabidhiwa mamlaka. Ni sheikh pekee na wa aina yake hapa Tz alie na low profile lakini akigusa mioyo na kubadilisha misimamo mingi ya kijazba na iliyokosa usuluub na ilm ya kisheria.
Allaah amponye sheikh na ampokee Marehemu wetu ktk pepo yake tukufu firdaous. Inna lillaah wainna ilaih rajioun.
Hayo ndio machache yaliyotufikia kutoka Znz kupitia mitandao ya kijamii