Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

Mlipuko mkubwa waitikisa Arusha!

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Posts
16,202
Reaction score
8,781
Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.

Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.

========
UPDATES:

- Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha amethibitisha kutokea kwa mlipuko wa bomu Arusha Night Park, hakuna vifo, idadi ya majeruhi haijajulikana bado.

Mlipuko mkubwa umetokea leo majira ya saa 1.30 usiku katika baa maarufu ya Arusha night park "Matak0 bar" iliyopo eneo la Mianzini mjini Arusha.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa mlipuko huo unatokana na bomu lililotengwa katika eneo la bar hiyo na kujeruhi watu zaidi ya 20 waliokuwa wakiangalia mchezo wampira wa miguu ligi kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea.

Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya dk. Mohamed na Mount Meru. Mashuhuda wanaeleza kuwa kuna baadhi ya majeruhi wamekatika viungo kama miguu nakadhalika.

Hili ni tukio la tatu mjini arusha bomu kurushwa na kutegwa katika maeneo ya mikusanyiko ya watu na hadi sasa Polisi hawajawahi kukamata wahusika wa matukio yote matatu.

Eneo ambalo mlipuko huo ulitokea.

attachment.php
 
Attachments

  • BlH3x0TIcAEaVjS.jpg
    BlH3x0TIcAEaVjS.jpg
    26.4 KB · Views: 10,874
watu wote wameshatawanyika...wikiendi Arusha imevurugika....
 
Hadi sasa hapa home Soweto najiuliza ni nini hiko! Mwenye taarifa kamili asikawie kutujuza
 
Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.
Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.

Fuatilia kwa karibu utushibishe mkuu
 
Nipo hapa Picnic na mie nimeucikia huo mlipuko.....mmmh...ngoja niwahi home.
 
Mkuu huu uchoyo wote wa nini?? Si ungejinyamazia tu? Si lazima uwe wa kwanza kurepoti jambo. Utakuwa wa maana ikiwa utaleta ripoti yenye mifupa na minofu juu yake. Siyo Skeleton. Eleza jambo tulielewe. Wengine tuna ndg huko. Wengine bado tuna mawazo fresh ya Olasiti na Unga ltd. Usitupandishe BP bure.
Mwingulu yuko wapi jamani??? Hivi yupo bungeni kweli naona kakaa kimya saana this week. Aisaidie polisi kubaini chanzo wasije sema ni kitu kibutu kwani Chagonji hachelewi
 
Ingekua unavyotaka wewe mangatara wala kusingekuwa na breaking news!
 
Last edited by a moderator:
Hivi Jk si yupo Arusha jamani?? Jus curious....
 
Kitu kama bomu kimelipuka Hapa Arusha maeneo ya MTK Bar Mianzini na kusababisha mshindo mkubwa sana.
Taarifa zinasema baadhi ya watu wameumia.
Asante PK kwa kuendelea kuifanya jf, "be the first to know!".

Endelea kufuatilia tukio hilo, haswa chanzo cha mlipuko na matokeo!.

Usiwajali watakaokulaumu kwa nini umeleta habari nusu, hao wamezoea kula chakula kikiwa kimeishaiva, na kupakuliwa kwenye sahani, wao kazi yao ni kula tuu, sisi ambao ni wapishi, hata chakula kabla hakijaiva, huonja kwanza, hivyo tunakushukuru kwa kutuonjesha, tunakisubiri kiive utupakulie tule!.
Pasco
 
Poleni wahuko, sisi haya mafuriko yanatutosha huku dar
 
Asante PK kwa kuendelea kuifanya jf, "be the first to know!".

Endelea kufuatilia tukio hilo, haswa chanzo cha mlipuko na matokeo!.

Usiwajali watakaokulaumu kwa nini umeleta habari nusu, hao wamezoea kula chakula kikiwa kimeishaiva, na kupakuliwa kwenye sahani, wao kazi yao ni kula tuu, sisi ambao ni wapishi, hata chakula kabla hakijaiva, huonja kwanza, hivyo tunakushukuru kwa kutuonjesha, tunakisubiri kiive utupakulie tule!.
Pasco
Well spoken bro!
 
Back
Top Bottom