Mambo/vitu gani vilikushangaza sana ulipokuja rasmi kuishi Dar es Salaam?

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,224
22,305
Ni ndoto ya watu wengi mikoani na hata nchi za jirani kama Zambia, Malawi, Burundi na Rwanda siku moja kutia mguu Dar au kuishi kabisa mjini Dar. Hata mimi ilikuwa ndoto yangu pia. Kile kibao kilichoandikwa DAR ES SALAAM pale Chalinze kinachoonekana wakati ukitokea Arusha kilikuwa kinanipa moto balaa kina nilipokuwa nikienda Shule Iringa.

Nikawa najiambia lazima nisome kwa bidii ili chuo kikuu nisomee Dar kwasababu ndo namna pekee iliyokuwepo kufika Dar kwa sababu inayoeleweka. Kabla ya kuanza chuo safari zangu zilikuwa ni za Moshi, Magugu, Orkesmet, Mdorii, Karatu, Mbulu hadi Dongobesh.

Baada ya kupata Admission nakumbuka nilipanda Lim Safaris kuelekea Dar kwa mara ya kwanza. Siku ya kwanza nilifikia kwenye gesti fulani nje ya Mabibo hostel. Ile gesti ilikuwa ni full uzinzi. Mimi nilikuwa nashangaa tu kwasababu hadi wakati huo sikuwa nimejiingiza kwenye mambo ya kuchakata mbususu.

Katika maisha yangu ya Dar nilikuwa nikishangazwa na mambo yafuatayo;

1. Vigodoro - mara ya kwanza kuona hii kitu ilikuwa maeneo ya Ilala Kota. Nilishangaa kuona mabinti wakicheza huku wakijifunua kuonyesha nguo za ndani waziwazi bila kujali kuna watoto, mama au baba zao. Ni kitu ambacho kwa mkoani ni ngumu kuona.

2. Muziki wa mnanda
- kwa wasiojua muziki wa mnanda waende Ilala Kota karibu na msikitini waulizie tu wanapofanyia mazoezi ya huo muziki. Hadi leo sijawahi kuuelewa. Wadau wanasema mnanda ndo ulizaa Singeli.

3. Mahindi ya kuchoma kuwekewa chumvi na pilipili
- hii kitu pia sio ya kawaida kwa mikoani. Ni Dar peke yake.

4. Watu kujenga mabondeni yanapopita maji
- na kinachoshangaza ni zile akili za kurudi tena bondeni mara baada ya mafuriko kupita. Watu wa mabondeni hupata hasara kubwa kwa kuingiliwa na maji lakini utashangaa maji yakipita hurudi tena kuendelea kuishi bondeni. Mafuriko ya 2012 yalikuwa fungakazi.

5. Ulaji wa chipsi wa kushangaza - hili ni jambo linaoongelewa kimasikhara ila ni ukweli mtupu. Mjini Dar watu hawali vyakula bali chipsi. Nilikuwa napata shida kuelewa mtu anawezaje kulala kwa kula chipsi tu tena mwanaume. Mimi huwa nakula chipsi kama kiburudisho tu au siku nikiwa sina apetite kabisa. Ukihesabu vibanda cha chipsi kuanzia shekilango hadi Afrikasana ni balaa.
 
Chips, kuna brother wangu Arusha yeye pia ananiambiaga..

Arusha mtu akitafuta ugali/wali/ndizi..ikitokea vimeisha hotelini ndio anawwza fikiria chips..

Yaani sio msosi, mtu anaweza kupanga subiri nikale chips..ni chagulio la mwishoo sanaa
Hahahaha
 
Ile nimeingia Dar, sijawahi kwenda beach bhana nikawa nimepanga chumba maeneo ya mikadi beach pale huku nasoma IFM pale,duu siku naenda beach mamaaaa! Nikasema dunia imeishaaaa! 😄 Kumbe nilikuwa sijaona mengi bado
 
Back
Top Bottom