Mlinzi Suma JKT ajiua kwa kujipiga risasi shingoni

Nawaza tu kuna baadhi hapa mnasema stress juu ya mshahara mdogo nk.

What about jobless? Mmefikiria japo na upande huu, how do they feel??

Izi mambo sio za kufagilia kabisa, kujitoa uhai kizembe damn!!

Mtoto wa kiume ni kugangamanya vijana acheni hizi mambo kabisa.

Nikawaza vile life’s good. Afu huku kuna watu wanajitoa uhai damn useless kabisa

Give me a break!!

Mungu atuepushe na ujinga huu wa kifkra
 
Short gun ni silaha ya hovyo!
huyo kijana huenda kalilalia bahati mbaya tu na kummaliza!

waliokuwa wa kwanza kumuona watueleze alivyokutwa na silaha, kama kajishoot inafahamika, na kama bahati mbaya yaweza fahamika pia
 
Kwa kweli kwa hali ya maisha ya ubepari kama huna Mungu ndani yako au mental na psychological calmness unaweza kufanya vitu ambavyo watu watakuona hauna akili kumbe mwisho wako wa kufikiri ndipo ulipoishia.

Unaweza in au kusikia watu mliokuwa nao shuleni au kambini washatoboa. Au unaenda maeneo kama Mlimani ukiona jinsi vijana au watu wanavyospend unaweza kujisonya sana.

Ktk nchi za Ulaya na US suicide na kuuana cases ni nyingi koz ubepari umekomaa. Sitamani tufike huko lakini kwa hali ilivyo ni kama vile safari imekaribia.

Zamani mtu akijinyonga inakuwa taabu kila mtaa utajua au kusimulia kwa wikii na mawiki ila Sasa imekuwa kawaida na sababu ni nyingi kuanzia maisha, mapenzi, kazi, kukataliwa, Kukosa tumaini, Kukosa Mali, kudharauriwa, masomo, kubakwa, kushindwa kuhimili tatizo nk.

Hivi karibu kuna kijana wa hapa Stend ya Magufuri wale wanaoshika chati za magari naye kajinyonga kwa sababu ya mapenzi. Mke wake alikuwa anamsumbua jamaa sana.
 
Mbeya hii ni case pili ndani ya mwezi mmoja na nusu. Kwamaana hiyo takribani walinzi wa suma JKT 8 wanajiua kwa kujipiga risasi katika mwaka mzima. Wekeni vitengo vya psychology and counseling viwe active huko makambini na kabla ya kuripoti kazini. Vilevile wizara ya ulinzi na mambo ya ndani itengeneze majeneza ambayo hawa watu wa security wawe wanawekwa kwa saa moja kila week wawe wanajitafakari.
Unasema??..Ha haaa
 
Wanaona watu wnaingia na mandinga makali, wanakula vizuri mara wawaletee nyodo au kuwatuma, na ukiangalia mtu anakaelimu kake, lazima apate depression. Walinzi wanatakiwa wale waliokubaliana na hali ya maisha au polisi wenye maisha yao.
Short gun zinawapiga kwa bahati mbaya tu wala sio kujishoot
 
Dogo alikuwa na Stress sana chanzo cha habari Dogo alikosa alichotarajia
 
Wazee hili laifu sio poa hasa ukiwa mzaliwa wa kwanza...kwa kifupi mimi pia napita hardtime sana

Sina kazi (jobless)

Nadaiwa kodi tangu October navumiliwa tu (kichwa kinauma machozi yanatoka)

Umri umesogea miaka 26 mates wenzangu wengi wana maisha na darasani nilikuwa bora kuliko wao.nimeomba makazi ya majeshi yote mwaka jana mpka nimekataa tamaa

Kula yangu mzozo,unaumwa ila unapona kwa nguvu za Mungu...

Kushinda week mfukoni huna mia ni kawaida

Kwa kifupi depression is real ukiona unaaamka unakula unavaa mshukuru Mungu

Mungu anisaidie nivuke salama nakiri sometimes najifikiriaga sana kujipoteza(kujitoa uhai) sema namuonea huruma mama na madogo zangu....


Naombeni kazi au mtaji wa biashara kwa makubaliano mniokoe ndugu zangu......
 
Back
Top Bottom