Mkwasi Rostam na Vodacom

wakati ule unaniandikia sms kwamba unauza computer ulikuwa hutumii voda ? ulikuwa ni mtandao gani ule tena ? ulivyojifanya unafanya kazi kongo kampuni ya mtn lakini uko kigoma kwa muda

hebu nikumbushe
 
Bravo Lunyungu
Hii ni njia moja nzuri ya kuonesha kuwa haturidhishwi na huyu mtu. Ni lazima tuchukue hatua i think it is wise if we get the message sent. Lazima tuoneshe uzalendo kwa taifa letu. Wanaomtetea RA wana lao

Nyinyi ndio mna lenu, hivi inakuingia akilini mtu akwambie bidhaa fulani ni za fulani bila ya vidhibitisho vyovyote na wewe ukubali kuacha kutumia......????? mshkaji inabidi ili waweze kuwashawishi watu aweke vithibitisho hapa.

Hivi wewe bongolander mpk leo hii vingapi unavyotumia ni vya halali????? na una uhakika gani kwamba sio vya mafisadi??
 
No no no hapo bado hauja tushawishi tuache kutumia mtandao wa Voda kisa ni wa RA tena kwa hiyo mada yako isiyokuwa na ushahidi wowote. Please kama una ushahidi wa uhakika uweke hapa kila mtu aone. La sivyo hadi house girl wangu naenda kumnunulia line ya VODA. siwezi kushawishika kwa hayo maneno yako tu.

watanzania kwa kutaka ushahidi hawajambo, lakini wakipewa hawachukui hatua!
 
Kususia huduma za Voda and any Rostam Az related product is not a soln on ufisadi and so. If the price of using Voda is extremely higher compared wit TiGO, Celtel, Zantel and other Netwk providers kwa namna ya kifisadi, then u can convice me kuihama Voda. Mi natumia TiGO, Celtel, Voda & Zantel.
It's free market but we have to be very careful especially when it comes the issue of being against smthg coz of smthg!! Kama huduma inatolewa na fisadi lakini imezingatia taratibu za kisheria na wananchi wameridhika nayo, then binafsi siioni kama kuna haja ya kutaka kuisusia eti kwa sababu tu kuendelea kuitumia unamwongezea mafungu the owner. We gain on both sides the user (consumer) and the provider na ndo maana kuna terms of use!
 
Njia ni kususia biashara zote za kifisadi, kama Vodacom haikupatikana kwa ufisadi mtawaonea; nashauri LUNYUNGU bidhaa zote za kifisadi ziorodheshwe hapa na kuzichambua kwa umakini na kuamua mstakabali wake kila moja, tutakuwa na hoja hapo, tusikimbie, twende mambo taratibu wanashikika wale;
 
Kususia huduma za Voda and any Rostam Az related product is not a soln on ufisadi and so. If the price of using Voda is extremely higher compared wit TiGO, Celtel, Zantel and other Netwk providers kwa namna ya kifisadi, then u can convice me kuihama Voda. Mi natumia TiGO, Celtel, Voda & Zantel.
It's free market but we have to be very careful especially when it comes the issue of being against smthg coz of smthg!! Kama huduma inatolewa na fisadi lakini imezingatia taratibu za kisheria na wananchi wameridhika nayo, then binafsi siioni kama kuna haja ya kutaka kuisusia eti kwa sababu tu kuendelea kuitumia unamwongezea mafungu the owner. We gain on both sides the user (consumer) and the provider na ndo maana kuna terms of use!

SPK

If a thieve comes at your house to sell an item that is sold from money obtained through theft would you buy? If fedha za madawa ya kulevya zikingizwa kama mtaji kwenye biashara fulani, would you entertain that bussiness? Rostam Aziz is a fisadi, he took money from you and invested in Vodacom just like Jeetu Patel took money from BOT and Invested into Bank M. All the principles of ethical investments are being violated nowdays and you still talk of terms of use! Lakini tatizo langu mimi ni je- ni mtandao gani salama? Kwanini hatuitumii mitandao hii hii kuwakaanga wenyewe? I remember sms about Rostam Aziz and Kagoda moved in a speed of light among the people including vodacom subscribers! So let us use they are own network to screw them

Asha
 
Inaweza Kuwa Kweli Alivipata Kwa Ufisadi.lakini Kashfa Zote Za Ufisadi Zimetoka Mwaka 2004/2005 Wakati Yayari Vodacom Ilikuwepo.sasa Hapo Ilianzishwaje Na Hizo Pesa????au Inakuwa Hadithi Ya Mwana Kondoo Ya Kuwa Kama Siyo Wewe Basi Ni Babu Yako Na Lazima Ni Kule?
 
Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?
jamaaa umekosa hoja ukisusia voda what next pato la taifa litashuka halafu Rostam siyo yeye ndiye mwenye hisa soln ni kumfikisha ktk vyombo vya dola ili sheria ichukuwe mkondo wake halafu kama ukiwa umezaliwa mjini unafahamu kama mengi aliwahi kuwazulumu wanzungu kutoka marekani pamoja na wafanyakazi wake katika kiwanda cha dawa za meno akasababisha hadi wazungu wapewe masaa 24 kuondoka nchini huyu...
 
Bravo Lunyungu
Hii ni njia moja nzuri ya kuonesha kuwa haturidhishwi na huyu mtu. Ni lazima tuchukue hatua i think it is wise if we get the message sent. Lazima tuoneshe uzalendo kwa taifa letu. Wanaomtetea RA wana lao

RA hana ubaya na hatetewi bali huo ndio ukweli.Hata kama vodacom ni yake ni vizuri tu.Mtu yeyote yule kama amewazidi maarifa watu lazima awalize.RA kazidi mbinu,kama anatoa somo na wanalikubali kwa nini asitulize?
 
Kuanzia Sasa Hivi Jukwaa La Siasa Liangaliwe Kwa Umakini Sana Leo Lunyungu Kaleta Hii Kesho Mwafrika Wa Kike Ataleta Za Kumsusia Kikwete Zaira Zake , Nae Tanzanianjema Atasema Hata Usisalimiane Na Mtu Ambaye Unahisi Ni Mwanaccm

Wanaanza Kutugawa Makundi Ndani Ya Forum Mpaka Mitaani , Tuogope Sana Watu Hawa Ni Hatari Kwa Ustawi Wa Jamii Zilizobora Na Makini Sehemu Yoyote Duniani .
 
wakati ule unaniandikia sms kwamba unauza computer ulikuwa hutumii voda ? ulikuwa ni mtandao gani ule tena ? ulivyojifanya unafanya kazi kongo kampuni ya mtn lakini uko kigoma kwa muda

hebu nikumbushe

We naye wakati mwingine unakaa kama mke mwenza mwenye gubu, kila uongeacho unadhihirisha jinsi ulivyo mweupe kichwani, no wonder watu hapa wanaignore thread zako kuzichangia hata kama siku hiyo umejitahidi kuongea sense. Hayo mamabo ya wewe kuwasiliana na lunyungu yuko congo sisi yanatuhusu nini, unakuwa kama kitoto kinavyomstaki mwenzie kwa baba yao akirudi jioni, sasa akukumbushe nini wakati unakumbuka na ndo maana ukaandika hapa.
 
Inaweza Kuwa Kweli Alivipata Kwa Ufisadi.lakini Kashfa Zote Za Ufisadi Zimetoka Mwaka 2004/2005 Wakati Yayari Vodacom Ilikuwepo.sasa Hapo Ilianzishwaje Na Hizo Pesa????au Inakuwa Hadithi Ya Mwana Kondoo Ya Kuwa Kama Siyo Wewe Basi Ni Babu Yako Na Lazima Ni Kule?

Ilianza mwaka 2000 ambapo tayari huyu Bwana alikuwa tayari ameshafilisi viwanda vyetu vya ngozi, tayari alishategeneza himaya yake ya kisiasa ndani ya CCM na kuitumia kuhakikisha kampuni yake ya Caspian inapata kandarasi serikali. Na kampuni hii ndio yenye mahisa humo vodacom. Lakini alikuwa pia na makampuni mengine pembeni yaliyokwiba fedha za mfuko wa Japan. Na pia lile kampuni lake lingine lililojibebea fedha za import support. Halafu akaendeleza mtaji wake miaka ya 2002-2006 kwa kutumia mafedha mengine ya BOT. Huyu ndiye Kagoda ninayemfahamu! Sasa ni bilionere, hata mkimchanganya vodacom, mkono wake upo kila mahali. Upo TICS, msuse kuingiza makontena. Upo habari corporation, msuse kusoma rai na mtanzania. Upo Mwananchi, nako pia msuse. Lakini upo pia ndani ya CCM, hisa zake huko ni nyingi zaidi. Mkitaka kumkomoa basi mjitoe kwenye Chama Cha Mafisadi(CCM),atabaki tu na vile vitega uchumi vyake vilivyopo Oman, Iran, Maritius etc. Hivi ile tenda ya kujenga kiwanja cha ndege alishakamilisha?

Asha
 
Lunyungu its a nice move ila watanzania walio wengi ni wagumu wa kubadilika as a result wanakufa na kamba shingoni.
Cha msingi apa ni kuolozesha biashara zote zilizo chini ya Mafisadi na kunza kuzisusia as soon as possible.
Ila sasa TICKS ya karamagi itakuwaje?
 
Kuna maswali kadhaa,
-Je shares za Caspian T LTD(zilinunuliwa kwa hela za kifisadi)
-Ilikuwaje Shares za Caspian kuongezeka wakati za Planetel zikapungua na Shivacom kuondolewa?
-Hizi kampuni nyingine zina nafuu? najua Celtel wamenunuliwa na Zein/Zain, Tigo from my understanding wako owned na Mic T LTD na Ultimate Security(ambayo inamilikiwa na muungwana mmoja ambaye naye ametajwa kwenye some of the dubious deals)
 
Superb! I like you, always sounding like a concerned TISS associate!

Asha
 
Mimi naunga mkono hoja ya Lunyungu kwa 100%. Hapa ninayo vocha ya Voda niliyonayo na inapesa zangu zilizobaki kama 16,000 baada ya kuweka Sh.20,000 jana asubuhi. Zikiisha bye bye voda hakuna atakayenipata huko tena. Nitabaki na line zangu za Tigo, TTCL na Celtel. Hata hivyo nimeshaanza kuishtuka celtel kama kamputni ya kifisadi baada ya MCI kudhurumu TTCL hivyo nafuatilia nikithibitisha naitema pia.
Pia nilishaacha kusoma magazeti ya Rai, Mtanzania na yale ya michezo maana nayo kwa kuyanunua namnufaisha RA. Nitasoma Raia mwema na Mwana halisi.
Asante Lunyungu hoja ina mantiki wasioelewa hawataelewa hata ukiwaelewesha vipi. Hii itaangusha uchumi wa RA iweje isiweje.
Naunga hoja
 
Mkuu Lunyungu nadhani uliangalie swala lako kiuchumi zaidi:::

Maoni yangu ni haya:::

1) Vodacom gharama zao ziko juu mno kulinganisha na Celtel, Zantel na Tigo. Swali kwa nini watu bado wako Vodacom???

2)Ingawaje hili ni suala la kisiasa lakini unaweza kuliweka kwa upande wa kumsaidia mwananchi na kusema unataka gharama za simu zishuke, kwa hiyo unawashauri wananchi waboycott Voda kwenye angle ya kiuchumi (ie savings) ili competition iongezeke na bei za simu zishuke.

Sasa watetezi wa Voda watuambie, kuna kosa gani kuwaelimisha wananchi kuwa waende kwenye gharama nafuu?? Si ndio PSA yenyewe au???
 
Ilianza mwaka 2000 ambapo tayari huyu Bwana alikuwa tayari ameshafilisi viwanda vyetu vya ngozi, tayari alishategeneza himaya yake ya kisiasa ndani ya CCM na kuitumia kuhakikisha kampuni yake ya Caspian inapata kandarasi serikali. Na kampuni hii ndio yenye mahisa humo vodacom. Lakini alikuwa pia na makampuni mengine pembeni yaliyokwiba fedha za mfuko wa Japan. Na pia lile kampuni lake lingine lililojibebea fedha za import support. Halafu akaendeleza mtaji wake miaka ya 2002-2006 kwa kutumia mafedha mengine ya BOT. Huyu ndiye Kagoda ninayemfahamu! Sasa ni bilionere, hata mkimchanganya vodacom, mkono wake upo kila mahali. Upo TICS, msuse kuingiza makontena. Upo habari corporation, msuse kusoma rai na mtanzania. Upo Mwananchi, nako pia msuse. Lakini upo pia ndani ya CCM, hisa zake huko ni nyingi zaidi. Mkitaka kumkomoa basi mjitoe kwenye Chama Cha Mafisadi(CCM),atabaki tu na vile vitega uchumi vyake vilivyopo Oman, Iran, Maritius etc. Hivi ile tenda ya kujenga kiwanja cha ndege alishakamilisha?

Asha

Nadhani huu ndo mzizi mkubwaa kuliko yote, huu ukikatwa naamini RA atanyauka tu!

Wito:
Kwa hao ndugu na jamaa tunao washawishi watupe line za voda, hiyo iambatane na kutupa/rejesha kadi + tisheti + kanga + fulana+ Kofia + mashati vya kijani, hiyo move ikifanyika tena kwa makusudi vikitupwa hivyo vivazi mbele ya ofisi za chama, kadi kweye mashimo ya taka, naamini hapo hiyo ngao aliyowekewa huyo fisadi ya kutoguswa kwa vile anawakodishia helokopita ya kampeini itapasuka na tuta weza mfikisha mbele ya sheria.

Otherwise hata hii ya kuanza na Voda si haba!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom