Mkwasi Rostam na Vodacom

Huu mkutano umejaa ubabaishaji mwingi sana. Sidhani kama kuna wahusika wengi hapa nchini, hata katika ngazi ya mawaziri, wanaoelewa kwa undani dhima ya huu mkutano. Nadhani wao wanaona kama kijiwe kingine cha kupigia blah blah.
Mpaka sasa hivi sijaona mikakati yoyote ya kitaifa ya ku-tap potentials ambazo tumekuwa tukiambiwa kijuujuu kuwa zinakuja along side huu mkutano
 
Naomba umwulize Carl Masters kwa nini yeye na Andrew Young na Goodworks International wamehusishwa na ufisadi huko Nigeria na ni mafanikio gani na ajira ngapi walio-create huko Nigeria, baada ya kufanya Sullivan Summit huko Lagos mara 2? Na usikubali akwambie eti alimpeleka Bill Clinton Lagos because Bill na Andy Young ni washikaji na business partners, na huyo Condi Rice naye asikutajie, kupeleka hao wazito si biashara ni blahblah.
Mbane vizuri pia kuhusu uhusiano wao na makampuni ya Coca Cola, na ya mafuta ambao ni clients of Goodworks (Young na Masters wote ni directors) na pia ni wadhamini wa Sullivan foundation. Pia mwulize how is it that mke wake Carl ndiye president wa Sullivan Foundation (Joy Masters)?
Jamani huu ni usanii mkubwa sana. Mnafahamu ya kuwa ITV kwa mfano walilipa hundred of thousand of USD kununua right to transmit the Summit? They are charging fees for hosting the summit! Na wametoa eti 700,000 USD via foundation for HIV/AIDS etc. Hela gani hiyo? Ni aibu tupu! Alafu magazeti wanawapamba utafikiri wanafanya cha maana.
mi naomba kuona guest list, ni wawekezaji gani wakubwa watakaohudhuria na ni wakuu gani wa serikali watakaohudhuria zaidi ya Museveni, Kagame (if they have the time)?Kazi unayo Paparazzi!
 
Pia mwulize how is it that mke wake Carl ndiye president wa Sullivan Foundation (Joy Masters)?

Mke wa Carl Masters......ni binti wa marehemu Leon H Sullivan mwenyewe....hence the name Sullivan Foundation.....Leon H. Sullivan Summit.....kwahiyo anasababu ya kuwa President, Chairman...or whatelse she might be kwenye hizo organisation zao!
 
utashangaa viongozi wa tanzania kushabikia mambo!
kikwete alienda Japan, hajapata hata kumaliza mkutano uzuri kakimbilia zake tanzania ati akawe mfunguzi wa mkutano wa sullivan. ukimuuliza akupe mchanganuo hizo zjira kutoka kwenye mkutano huu zitapatikana vipi.......peupeee!
 
Unajua huu mkutano ni wa kitapeli tu umepambwa kifisadi fisadi angalieni eti ITV ndio wanahaki ya kuunyesha LIVE mkutano huo jamani hii nimesikia kama ni shughuli inayo husu UTAIFA kwa hiyo itafika kipindi hata maadhimisho ya MUUNGANO vyombo vya habari vitakuwa vinajipa haki miliki kuonyesha kama ilivyo fanya ITV lazima kuna harufu ya kifisadi hapo kwa hiyo TBC1,Star TV na nyinginezo hazina haki kuonyesha mkutano huo mpaka wapate kibali toka kwa ITV duh hii sasa kali.
Angalia kwenye mawasiliano VODA nao wanadai wanafadhili mawasiliano kule wanadai huduma zao ni nafuu kuliko mitandao mingine.....Hivi kuna mtandao gani wenye gharama nafuu hapa TZ kama TIGO ambao umewawezesha walalhoi kuwasiliana kwa longa longa pamoja na etreme kwa gharama chee na huo wa VODA ni moja ya mitandao yenye gharama za juu sana kuliko TIGO,ZANTEL lakini kumbukeni mashareholders ni mafisadi wenyewe wanawakamua sana waTZ wasio jua gharama halisi za mawasiliano.
Je nn tutapata kama wazawa katika mkutano huu?
Je tutegemee kuachiwa mashimo kwenye ardhi yetu kwa mikataba ya miaka 99?
Naona vyombo vya mafisadi vinautangaza sana mkutano huu.
Tusubili machungu tu hapa nyumbani.
 
Mwisho wa yote nitauliza yafuatayo kwa mpigo .Je maada mkutano Tanzania itakuwa imepata faida gani ? Wangapi wana enda Mbugani kutuachia pesa kidogo ama ZNZ ? Ule ujio wa Bush ume create ajira ngapi na kama bado lini faida za Bush kuwa Tanzania ambazo tulitangaziwa kwa lazima zitaanza kuonekana ?

Faida ya kwanza nadhani itawa kwa wenye Mahotel na nyumba za kulala wageni ambao wamepandisha bei za huduma wanazotoa kwa hadi asilimia 150!

Kwa faida nyengine na job creation hapo bado nna maswali magumu...hayajibiki. Tobo katika uchumi na mengine yatafahamika mara baada ya mkutano kumalizika!
 
Vodacom Overview Shareholders
Vodacom Group 65%
Caspian Ltd 19%.....Rostam Aziz
Planetel Communication 16%...Noni

Lowasa ni Super Dealer....tu kupitia Kampuni yake Alphatel...
 
utashangaa viongozi wa tanzania kushabikia mambo!
kikwete alienda Japan, hajapata hata kumaliza mkutano uzuri kakimbilia zake tanzania ati akawe mfunguzi wa mkutano wa sullivan. ukimuuliza akupe mchanganuo hizo zjira kutoka kwenye mkutano huu zitapatikana vipi.......peupeee!

JK BILA KUKUTANA NA ROSTAM NA HAO MATAPELI WENGINE,KWENYE HUO MKUTANO WA MATAPELI ATAPATA WAPI NGAWIRA YA KUHONGA WADANGANYIKA WAMCHAGUE KWA 90% 2010?
 
KUna jambo moja ambalo tumelikosea sana wakati tunashupalia Uadilifu wa Sullivan na ujio wa mkutano huu. Ni opportunity ya kujitangaza kibiashara na kujiingizia kipato.

Hivi, kama tungechanga vijisenti, tukamtuma Halisi au Invisible wakaweka IT Kiosk yenye network babkubwa na ku-charge dola kadhaa kwa saa ka matumizi ya Computer na huduma, je tungejipatia vijisenti vingapi?

Je kama tungeweka mkakati wa kibiashara kwa kutafuta wawekezaji na kuingia nao ubia kungekuwa na ubaya gani?

Hivi kama tungeungana na kutafuta Travel Agent mmoja au vendors wa kutoa huduma na tukatoa best services, je tungejitangaza namna gani na kujiingizia mapato?

Just a thought after the fact, realizing what a missed opportunity simply because I was too critical of everything and saw everything from Ufisadi perspective and not business opportunity.
 
Rev.

am starting to think you are a genius!
 
Rev. Kishoka,
Haya ndio mawazo mkuu sio habari za kudadisi kila kitu wakati watu wanakwenda mbele sisi tunakanyaga moto kwenda mbele huku guu jingine limedata kwenye brakes!
 
Unajua huu mkutano ni wa kitapeli tu umepambwa kifisadi fisadi angalieni eti ITV ndio wanahaki ya kuunyesha LIVE mkutano huo jamani hii nimesikia kama ni shughuli inayo husu UTAIFA kwa hiyo itafika kipindi hata maadhimisho ya MUUNGANO vyombo vya habari vitakuwa vinajipa haki miliki kuonyesha kama ilivyo fanya ITV lazima kuna harufu ya kifisadi hapo kwa hiyo TBC1,Star TV na nyinginezo hazina haki kuonyesha mkutano huo mpaka wapate kibali toka kwa ITV duh hii sasa kali.
Angalia kwenye mawasiliano VODA nao wanadai wanafadhili mawasiliano kule wanadai huduma zao ni nafuu kuliko mitandao mingine.....Hivi kuna mtandao gani wenye gharama nafuu hapa TZ kama TIGO ambao umewawezesha walalhoi kuwasiliana kwa longa longa pamoja na etreme kwa gharama chee na huo wa VODA ni moja ya mitandao yenye gharama za juu sana kuliko TIGO,ZANTEL lakini kumbukeni mashareholders ni mafisadi wenyewe wanawakamua sana waTZ wasio jua gharama halisi za mawasiliano.
Je nn tutapata kama wazawa katika mkutano huu?
Je tutegemee kuachiwa mashimo kwenye ardhi yetu kwa mikataba ya miaka 99?
Naona vyombo vya mafisadi vinautangaza sana mkutano huu.
Tusubili machungu tu hapa nyumbani.

Fidel unafahamu ya kuwa Vodacom na ITV wamelipa hundreds of thousand of USD kupata haki ya kuwa exclusive providers kule? Hii ni biashara si utaifa or whatever, let TBC1 pay 200,000 USD kama Mengi alivyolipa watapata haki ya kutransmit. Katika hilo nasema it is ok.
 
Mke wa Carl Masters......ni binti wa marehemu Leon H Sullivan mwenyewe....hence the name Sullivan Foundation.....Leon H. Sullivan Summit.....kwahiyo anasababu ya kuwa President, Chairman...or whatelse she might be kwenye hizo organisation zao!

Kigoma, asante kwa maelezo! I think then in this cse we rephrase the question: How come Joy Sullivan Masters' husband is on the board and is a prominent member and organizer of the Foundation? Kwa mfano Cindy McCain ana foundation lakini John McCain is not on the foundation board. This is important especially since Carl Masters ana kesi kule Nigeria na hata Marekani people are seeking to indict him as Economic hitman aliyewaibia sana waafrika!
 
Kama mlivyosema wengi hapo juu. Mkutano umekuwa ukipambwa sana na vyombo vya habari vya ndani na nje. Lakini hatuelezwi kwa kina kwamba watanzania watafaidika vipi na huo mkutano. Tunachoona sasa hivi (labda ndio faida zenyewe) ni mahoteli kujaa wageni na watu wenye magari kupata tenda ya kukodishwa kwa kiwango cha Tshs 150,000/- kwa siku. Labda wageni wachache watatembelea mbuga zetu pia. Je, hizi ndio faida za Sullivan Summit?
 
MiMi naomba tu orodha ya wageni hao ili tuweze kujua wanakujakwenye huu mkutano kufanya chochote cha maana! Ni vituko tu, wameleta watalii matajiri siyo wawekezaji.
Hii ni ze comedy kweli!
 
naomba na mimi kuuliza niliwahi kuambiwa nikiwa nje ya tz, kuwa shareholder wakubwa wa vodacom ni lowasa na rostam azizi, na eti rostam yeye ana hisa nyingi kupitia caspian construction na bwana lowasa sijui alphatel, na hata ile bilioni moja waliotoa vodacom kama msaada wakati wa ile njaa ya kuundwana loasa zilitoka kama geresha!
tupashane, kama hili kampuni ni la kifisadi tuanze nalo

Ni kweli Rostam kupitia kampuni yake ya Caspian anamiliki kama 20% ya hisa za Vodacom Tanzania na Planatel Communication inamiliki 15% ya hisa. Hao ndio watanzania pekee wenye hisa Vodacom. Japokuwa hizo 15 za Planatel ni kiina macho (Peter Noni) ndio mmiliki wake kuna wakubwa wengi zaidi wanamiliki hizo hisa yule ni kama kivuli cha kuwafunika wakubwa.

Kuhusu Lowasa yeye anamiliki Alphatel ambayo ni wakalu mkuu wa Vodacom, Alphatel haina share yoyote Vodacom ni wakala tuu.
 
Kenya waligomea hata vyakula kwenye supermarket when they felt kwamba pesa zao zilienda kwa Kibaki na zikatumika kuwanyima haki yao .Tanzania Rostam Aziz kila kukicha ana wezi mpya lakini iko kimya na support anapewa .Sisis tuna lalamika lakini bado tunatumia huduma za simu za Vodacoma ambazo yeye ni mmoja wa share holders .Kama tuna uchungu kweli na huyu ambaye analindwa na CCM na serikali yake , tuhamie sote kwenye tigo ama zantel ama Celtel .Hii itakuwa njia nyingine ya sisi kuonyesha kwamba tumechoka kuibiwa na kuzidi kukamuliwa kila mara .Mimi nimesha hama na huhu unakaribia mwaka tangia nimejua kwamba Rostam anatumaliza bado na vodacom yumo .Mie natumia Zantel sasa na Celtel .Je wewe unangoja nini ?Tuambiane tuachana nao hawa .Wanatuona wajinga katika maamuzi yao je waendelee kutuona wajinga hata katika pesa zetu wenyewe za kutumia katika simu ?
 
Back
Top Bottom