Mkuu wa Wilaya ya Same aagiza Shule ya Msingi Kigulunde ifungwe kutokana na kutishia usalama wa watumiaji

Same.jpg

Same2.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni ameagiza kufungwa kwa Shule ya Msingi Kigulunde, iliyopo katika Kata ya Mtii, Tarafa ya Gonja kutokana na kutishia usalama na uhai wa wanafunzi pamoja na walimu wao.

Shule hiyo iliyojengwa mwaka 1975, licha ya kukabiliwa na uchakavu wa majengo yake, imejengwa kwenye mkondo wa maji.

Hofu hiyo inatokana na historia mbaya ya shule hiyo ambapo mwaka 2011, ilizingirwa na mafuriko ya maji, yaliyokuwa yakitiririka kutoka safu za milima ya Upare, na hivyo kusabisha uharibifu wa miundombinu yake ya madarasa.

Amri ya kuifunga shule hiyo ambayo ina jumla ya wanafunzi 49 na walimu wawili, imetolewa, Desemba 5, 2023 wakatiDC huyo alipoitembelea shule hiyo akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo.

"Nimeagiza shule hii ifungwe, nimeitembelea na iko kwenye mkondo wa maji, na mwaka 2011 iliwahi kukumbwa na mafuriko na wataalam wangu wa udhibiti ubora wamenithibitishia kwamba pale hapafai na walishatoa huo ushauri kwa mamlaka husika kwamba hiyo shule ifungwe," amesema DC Kasilda.

Pia soma - Muonekano wa Shule ya Msingi Kugulunde, miundombinu yake ni hatari kwa Wanafunzi na Walimu

- Kilimanjaro: Serikali yasema inasubiri Wananchi watenge eneo ili ujenzi wa Shule ya Kigulunde uanze
 
Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729

FB_IMG_17018049790764977.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kufunga mara moja Shule ya Msingi Kigulunde baada ya kubaini eneo ilikojengwa shule hiyo ni mkondo wa maji na tayari majengo yake yana nyufa hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.

Shule hiyo yenye wanafunzi 49 na walimu wawili iliwahi kukumbwa na mafuriko mwaka 2011 na baadhi ya majengo kusombwa na maji ambapo kipindi hicho iliamuliwa wanafunzi kupelekwa shule jirani ya Msingi Mtii.

Katika ziara yake mkuu huyo wa wilaya aliye ambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ameagiza shule hiyo kufungwa na wanafunzi kupelekwa shule iliyo jirani, Shule ya Msingi Mtii kuendelea na masomo wakati hatua myingine zikiendelea ikiwemo uwezekano wa kujenga shule mpya eneo rafiki litakalo kuwa salama.

Viongozi wa Kijiji hicho wamebainisha kuwa eneo la shule lina ukubwa wa Hekari Saba na mkuu huyo wa wilaya akashauri endapo wakazi wa eneo hilo wanauhitaji wa shule kushirikiana na wataalam wa Halmashauri kupata eneo linalofaa na kuanza msaragambo kujitolea michango na nguvukazi kujenga maboma Kisha kuwezesha urahisi kwa serikali kumalizia kama inavyofanyika kwenye maeneo mengine.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
 
Yaani hapo kiujumla kawaambia wananchi wajenge shule nyingine!
 
Kwa mazingira haya bado tunatarajia mwl. Kuipenda kazi yake.
Huyu DC naye ndo anajua Kuna shule ya namna hii kwenye eneo lake.
 
Mkuu wa Wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kufunga mara moja Shule ya Msingi Kigulunde baada ya kubaini eneo ilikojengwa shule hiyo ni mkondo wa maji na tayari majengo yake yana nyufa hali inayohatarisha usalama wa wanafunzi na walimu.

Shule hiyo yenye wanafunzi 49 na walimu wawili iliwahi kukumbwa na mafuriko mwaka 2011 na baadhi ya majengo kusombwa na maji ambapo kipindi hicho iliamuliwa wanafunzi kupelekwa shule jirani ya Msingi Mtii.

Katika ziara yake mkuu huyo wa wilaya aliye ambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ameagiza shule hiyo kufungwa na wanafunzi kupelekwa shule iliyo jirani, Shule ya Msingi Mtii kuendelea na masomo wakati hatua myingine zikiendelea ikiwemo uwezekano wa kujenga shule mpya eneo rafiki litakalo kuwa salama.

Viongozi wa Kijiji hicho wamebainisha kuwa eneo la shule lina ukubwa wa Hekari Saba na mkuu huyo wa wilaya akashauri endapo wakazi wa eneo hilo wanauhitaji wa shule kushirikiana na wataalam wa Halmashauri kupata eneo linalofaa na kuanza msaragambo kujitolea michango na nguvukazi kujenga maboma Kisha kuwezesha urahisi kwa serikali kumalizia kama inavyofanyika kwenye maeneo mengine.

Sent from my TECNO CF7 using JamiiForums mobile app
Magufuli njoo umkamate huyu aliyepiga picha hii.
 
Halafu, hapo unakuta DC na msafara wake wana MaV8 yakutosha, RC analakwake nk, eneo lina Mbunge, Diwani nk... toka 1975 shule ipo hapo eti leo ndio tunasema ni hatari.

Kujenga tu madarasa kama 7, nyumba standard za walimu kama 10 ni kazi nguumu sana hapo..
Hivi DC atashindwa kufanya fund raise hata 20m ya kujenga madarasa mawili?
 
EE ni kwa matajiri,shule IPO mkondo WA Maji ndio maana haijaendelezwa wanataka kujenga eneo jingine
Tangu lini wapare wa Same wakawa matajiri?
Mvua na ardhi yao ni chanzo cha umasikini, bora Usangi mara 100
 
Back
Top Bottom