Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Mkuu wa nchi ambae ndio ndio custodian wa mali za taifa la watanzania kudai kuwa hawezi kufokea mtumishi wa umma ni kushangaza umma wa watanzania.
Kwamba watumishi wa umma wakiharibu atawabembeleza?
Nimekaa na wazee wengi waliofanya kazi na hayati Julius Nyerere wanasema wazi kuwa Mwalimu alikuwa mkali sana.
Ilitokea akikuita kwake Msasani au Ikulu ilikuwa lazima upate wasiwasi na woga mkuu.
Wengine aliwaita kuwapongeza lakini hawakuamini walichoitiwa wapo pia aliowafokea hadharani au hata kifichoni.
Kwamba mkuu wa nchi unafanya kazi kwa kuonea aibu wateule wako? Kwamba utakuwa unawabembeleza?
Mbona hii sio sawa? Mkuu wa kaya lazima uwe mkali ili nidhamu ipatikane kuanzia juu mpaka chini.
Hatusemi ufokee watu kama watoto wako. Bali uwe na maamuzi na maelekezo yenye kuonyesha kuwa kuna kiongozi mwenye mamlaka aisiyetaka mzaha na anataka watu wafanye kazi.
Mfano, tulitegemea umkaripie January Makamba maana mradi wa JNHP unaweweseka kama vile hauna manufaa kwa wanaCcM wenzake.