Uzalendo wa Hayati Mwalimu Nyerere na Sokoine hakuna kiongozi wa kuufikia

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Wadau nawasabahi. Naomba tuambizane ukweli.

Toka vifo vya mwalimu Julius Nyerere na Edward Sokoine nchi yetu imekosa kabisa viongozi wenye uzalendo na nchi hii. Hayati Nyerere na sokoine hawakuruhusu raslimali za nchi zichezewe au ziuzwe

Hawakuruhusu fedha za umma ziibiwe na wajanja. Hawakuruhusu matajiri kushika nyadhifa ndani ya chama.

Hawakuruhusu viongozi kuwa na hisa ktk makampuni na mashirika ya umma hawakuruhusu viongozi kufanya biashara na kuwa na majumba ya kupangisha.

Ndio maana walianzisha Azimio la Arusha ili kuyasimamia na kuyadhibiti hayo yote.

Tanzania ya leo viongozi ndio wahusika wakubwa wa hayo yote.Uzalendo wa viongozi kwa nchi yao haupo.

Tumeshuhudia ufisadi mkubwa wa viongozi kwenye mali za serikali.

Tumeshuhudia viongozi kuchezea raslimali za nchi kama zao.

Tumeshuhudia viongozi wakiwa na hisa na biashara kubwa kwenye mashirika ya umma.

Hakika nchi imekosa viongozi wazalendo.

Viongozi wanaishi maisha ya raha na starehe zaidi ya wananchi wao

Viongozi wanatumia magari ya starehe na kujilipa mishahara kubwa na minono huku walimu wakiishi kwa mishahara ya kujikimu siku 15 wao na familia zao.

Tumeshuhudia wabunge wakijitetea wenyewe na kujilipa mishahara na posho nzuri huku waliowatuma kwenda bungeni wakikosa maji na dawa.

Hebu viongozì kuweni wazalendo kama hayati mwalimu nyerere na hayati sokoine ili mungu siku moja awahesabie haki mtakapofika mbinguni.

0ca13942dedc0ae4512fc89119b683a2.jpg
c41eea363bfdecfbd77754bcfb00ced8.jpg
 
Lakini matatizo mengi ya leo ni matokeo ya uongozi wa nyerere
1. Azimio la Arusha, limechelewesha sana watu, limeathiri mambo mengi sana kiuchumi
2. Kuchelewasha vyama vingi na kukubali mawazo ya watu tofauti mfano Osca kambona.

Kinacho msitiri Nyerere ni kutokuepo kwa media,
 
Back
Top Bottom