Resilience
JF-Expert Member
- Jan 4, 2023
- 877
- 4,106
Mshauri wa kisheria wa serikali ni mwanasheria Mkuu wa serikali. Ilipotokea kifo cha Hayati Magufuli alipaswa kutoa dira ya kikatiba na kisheria. Alipaswa kusimamia uandaaji wa tangazo la kifo kwenye vyombo vya habari kujielekeza katika vifungu vya sheria vya kutangaza kifo, maambolezo na kuapishwa Rais Mpya.
Kwa maelezo ya CDF ni kwamba huyu AG hakutekeleza wajibu wake au labda akishirikishwa. Kuachwa kwake nyuma ni kwa sababu ofisi hii imekuwa ya kisiasa kuliko ya kitaaluma. Angekuwa strong enough angeitwa at first place .
Mapungufu ya ofisi ya AG hata sasa yanaonekana wazi. Sikiliza tangazo la kifo cha JPM kama utasikia ikitamkwa kifungu cha katiba, fuatilia mchakato mzima wa mazishi hakuna tangazo lililozingatia mwongozo wa sheria na katiba.
Tuachane na hayo, tusome barua za uteuzi na utenguzi tuone kama kuna maneno
..Mhe. Rais wa JMT kwa mamlaka aliyopewa chini ya Ibaraa ya katiba au kwa mujibu wa kifungu ...cha sheria........ameteu au amevunja au ametengua uteuzi wa...
Nenda kwenye mashirika na taasisi nyingine nchni maaafisa habari hakuna Sehemu wanatoa tamko lao kwa kutaja sheria wala kanuni maana yake hakuna mwongozo wa AG kuwataka wazingatie sheria.
Nchi za wenzetu mfano Kenya kila tangazo la serikali lazima liwe na reference na backup ya sheria iliyohusika. Kwetu tunashindwa nini kuziweka sheria zetu kwenye practice? Mazoea ujenga kawaida.
Kwa kutotaka kuzingatia sheria ndiyo maana Jaji Mkuu ameongezewa muda kimya kimya na hakuna official report to public na hata mahitaji ya sheria kwamba inatakiwa kutangazwa kwenye GN limepuuzwa.
Let us operate professionally, fani ya sheria nchni kuweni na wivu na fani yeni. Wafanyeni watu wasome sheria serikalini kwa kufanya yafuatayo
1. Kila tangazo la serikali linalotolewa kwa mujibu wa sheria au katiba basi liwe na kifungu husika. Hii itawafanya wanaotoa taarifa kwa umma kusoma na kujieleimisha kuhusu matakwa ya sheria
2. Majibizano na maamuzi yote ndani ya serikali yaandikwe yakiwa na backup ya kifungu cha sheria.
3. Auditors wanapofanya ukaguzi wajiridhishe na maamuzi yaliyofanywa kama yalijielekeza kwenye citations za sheria husika au maamuzi yanatolewa kwa stori tu.
4. Viongozi wa kisiasa wanapotekeleza maelekezo yao lazima wazingatie sheria na waseme sheria iliyoguswa.
Sekta binafsi hawana sheria ila wana kanuni na miongozo ambayo usipoizingatia umefikuzwa kazi. Hii inasaidia kazi inayofanywa na bunge ya kutunga sheria iwe na tija. Kama tunatunga sheria na hakuna anayeona zina kazi gani?
Kila siku tunashindwa kesi za kimataifa kwa sababu watumishi wa umma na wanasiasa wazingatie sheria wanapooshauri serikali. Hii yote ni kwa sababu watu wamegoma kusoma na kuziishi instrument zao za kazi.
PGO ilipaswa kuifungua macho ofisi ya AG kwamba yanayofanywa serikalini ni mazoea na siyo sheria.