Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,673
- 22,264
Ujenzi wa uboreshaji soko la Mbagala Zakhiem umekamilika na wafanyabiashara wa soko hilo walitegemea warejeshwe kwenye soko hilo kulingana na utaratibu waliopewa kabla ya ujenzi, kinachoendelea hivi sasa ni wamejitokeza viongozi wanaotaka kuvuruga utaratibu wa kuwarejesha wahusika ili wajigawie wao! Watu hawa hujitokeza kwenye kila miradi ya masoko inapokamilika.
Wafanyabiashara wa soko hilo kabla ya kupisha ujenzi walichukuliwa taarifa zao na kupewa namba za vizimba vipya kulingana na walivyokuwa awali, ila sasa wamejitokeza watu wanaotaka kuvuruga ahadi ya utaratibu wa awali ambao usingeleta taharuki wala vurugu na wanasababisha kuchelewa kuwarudisha wafanyabiashara walipewa namba za vizimba vipya hivyo kulikosesha mapato jiji.
Kama ulivyoweza kuwadhibiti watu hao waroho kwenye masoko ya Mwenge na la ndizi ndiyo matarajio ya wafanyabiashara wa soko la Mbagala Zakhiem.