Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,673
- 22,264
Mkuu wa mkoa umeonekana kwenye TBC 1 saa mbili usiku ukitoa shutuma kuwa wafanyabiashara wamefoji majina! Pamoja na udogo wao kimadaraka shutuma hizo si za kweli.
Mkuu wa mkoa kabla ya soko la awali kubomolewa wafanyabiashara waliokuwepo manispaa ya Temeke iliwapiga picha kila mmoja kwenye fremu yake na kumpa namba, hizo namba wafanyabiashara wanazo na ndiyo ushahidi wao dhidi ya madai yako, nenda Mbagala Zakhiem kaoneshe majina ya waliofoji na wao watakuonesha namba walizopewa na manispaa, pia manispaa wanazo picha za wafanyabiashara husika.
Mkuu wa mkoa hapa kinachohitajika ni kueleza hao wafanyabiashara waliopewa kipaumbele cha kupata fremu za mwanzo wametoka wapi wakati hawakuwepo kwenye soko la awali.
Nenda Zakhiem ili wananchi wajenge imani kwenu katika ugawaji wa keki ya taifa.