Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Mkutano wa Mwigamba na vyombo vya habari

Kama kweli mh. Mbowe alishuhudia mwigamba akipigwa, mbowe yapaswa awaombe wanachadema na watanzania msamaha, kiongozi wa upinzani sio mtu mdogo hata kidogo, anastahili kuheshimu haki za binadamu na haki za watuhumiwa! Mimi kama mwanachadema nimesikitishwa sana na hayo yaliotokea.
 
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.

Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.

Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.

Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.

Hakuna mapya!
vp mkuu utabili wako umetimia au pepo la kijiendekeza lilikuharakisha ?
 
Uyu atakuwa msaliti,kakiri kutumia ID feki kwenye mitandao akiwa kama Mwenyekiti,ni sawa na Dr.Slaa au Mbowe atumie ID feki kuhujumu chama alafu anadai anamapenz na chama,huo ni unafki mkubwa,akiwa kama Mwenyekiti nilitegemea aje na ID original kama mwenyekit wa Arusha,je isingejulikana ingekuaje.Nimemsikia kwenye media kamtukana sana Lema..

Nadhani alikuwa na nia ovu paseee, angeyazungumza ndani kikaoni na kama aliona kwenye hadhira ndo sawa basi angekuja na Jina lake halisi as long as anazungumza mambo yenye uhakika kwa kadiri ya ufahamu wake
 
Atasema kuwa aliondolewa makao makuu kwa hila.

Atasema aliombwa kufanya kazi pale lakini mambo yakaenda ndivyo sivyo.

Atasema hakuna uhuru wa kutoa maoni. Atasema kuna ukabila na udini.

Atasema yeye ni msomi hawezi kutumika. Kisha atasema anaipenda Chadema na kambi ya upinzani na ni muumini wa mabadiliko.

Atasema anakusudia kukata rufaa. Atasema anaenda mahakamani.

Hakuna mapya!
Mpumpaf kwa wapumbaf kama mpumpaf Ben mpu.paf asiyejitambua
Wewe unapata wapi ujasiri wa kumkanusha Mwigamba kwa hayo anayoeleza na aliyotendewa.
Pumbaf tena.
 
ndio maana nilishakataa kuwa mtaji wa wanasiasa!! kwz kbs usaliti ni nini!?mm binafsi nadhani ni kutoa siri ambayo kimantiki lazima iwe true kwa wasio husika. Mwigamba hajaitwa muongo,wala mzushi bali msaliti mfano wa yuda kwa sababu ya kutoa siri(ukweli) kwa watanzania wote na sio wanachadema tu japo wengi walikua gizan kama mm. kama mTz wa kawaida mwigamba ni shujaa kwa upande wangu coz ni upande tofauti na watunza siri ambao walikusudia nisiijue. na kama chadema wanasema kanunuliwa ili atoe siri,hv kwa nafasi aliyonayo Mwigamba chadema ni ya kununuliwa kwl na ma'ccm!! je hakuna wengine watakanunuliwa!!?na je hayo matycoon ya ulaya tungewapa nchi si ingekua laana maana mwenyekit wa mkoa ananunuliwa na ccm tu!toeni vielelezo mje kujibu hoja,sio kwa vile hatuipendi ccm ndo mtugeuze geuze mpendavyo maana nishaona na nyie njaa tu zinawasumbua!!
 
Pole na huruma ziwaendee hao waandishi wa habari walokwenda kumsikiliza huku wakijua fika MFAMAJI HAISHI KUTAPATAPA
 
Mwigamba ana hoja ! CHADEMA inaendeshwa Kidikteta na Mbowe anatakiwa kung'atuka apishe damu changa willingly!

Aheri iongozwe kidikteta kuliko iongozwe na wasaliti,

Usaliti ni moja ya dhambi isiyosameheka hata mbele za Jah
 
Umenena Mkuu, ametuma vijana akina Bramo Waje kutukana watu hapa Jamvini!

Mkuu MSALANI, kitu kimoja kinachonicehekeshaga ni kuwa, tofauti na wenzako wa Team Buku 7 LF, wewe hutukanagi kabisaa, Chukua like yangu
 
Last edited by a moderator:
Kama ilivyo kazi kubwa sana kuiondoa CCM madarakani ndivyo ilivyo kazi kubwa pia kupata suluhisho la utawala wa sheria.

Hakuna ubishi hata kidogo kwamba Mwigamba amefanya kosa la kiufundi, lakini wakati huo huo inashangaza sana kwamba ndani ya kikao kile kulikuwa na wabunge watunga sheria wetu akiwemo Mwenyekiti wa taifa wa chadema wakishuhudia na kuchekelea vitendo vya kihuni vya vijana wa chadema wakiongozwa na Lema (Mbunge) kumshambulia kiongozi mwenzao ndani ya kikao ili hali kulikuwa na nafasi ya kuyamaliza haya ndani ya kikao bila kuleta vurugu na bila kuleta attention ya media isiyo ya lazima. Busara ya Mbowe iko wapi?

Hawa ndiyo watakuwa mawaziri wetu huko baadaye, wavunjifu wa utawala bora, watu wanashabikia eti kwa sababu lengo ni kuindoa CCM madarakani basi tusiwaguse hawa wafalme.

Tunaweza kweli tukaiondoa ccm madarakani, but guess what next!!!! Sitaki kuwa mtabiri, lakini viongozi wetu wasipojirekebisha, ikiwa ni pamoja na yale ambayo Maskini mkulima kayainisha kule, itakuwa ni kilio na kusaga meno mfano wa wale waliomuondoa Gadaffi madarakani wakitegekea maisha bora zaidi kumbe ni shida bora zaidi.

Wabunge wetu mmeonyesha udhaifu mkubwa sana na Mungu Mkubwa hayakutokea madhara makubwa zaidi.

Wale washabiki bendera fuata upepo, badilikeni, jaribu kuwa objective kidogo. Kama mnaunga mkono Mwigamba kushambuliwa vile, nawaomba pia muunge mkono polisi wanapowashambulia nyie, maana yote yanahusu utawala wa sheria na utawala bora.

Isiwe tu kwa mwenzio kutamu kwako mhhhhhh.
 

[TD="bgcolor: #ffffff"]MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha ambaye amesimamishwa uongozi kwa tuhuma za usaliti, Samson Mwigamba, amesema kuwa hakupigana na Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, kama ilivyodaiwa na baadhi ya magazeti.
Mwigamba alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa kuelezea kile kilichojiri mwishoni mwa wiki hadi akapigwa na baadhi ya wajumbe wa kikao, wakimtuhumu kwamba aliandika taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa Jamii Forums akizungumzia masuala ya uongozi ndani ya chama.
Mwigamba alisema kuwa hata wakati akivutana na walinzi wa chama Mbowe hakuwa ndani ya chumba cha mkutano, hivyo akadai kuwa anashangazwa na wale waliosambaza taarifa hizo kwamba alipigana na kiongozi huyo ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni.

Aliwataja wale aliodai walimpiga kuwa ni Katibu wa Bavicha Wilaya ya Arusha, Noel OLovaroya, walinzi wa chama pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, kwamba alijaribu bila mafanikio kumpiga na kitofali ambapo alikikwepa kwa kujiangusha chini na kujigonga kisogoni.
“Wakati vurugu zikianza Mbowe hakuwa ukumbini, nilimuona akija Lema na Olevaroya, ambapo Lema alishikwa kabla hajanifikia huku Olevaroya akiruka juu ya meza na kuja kunipiga ngumi, mimi kwa kujitetea ilibidi nimpige ngumi kabla hatujaamuliwa,” alisema.
Mwigamba alimtuhumu Lema kuwa amekuwa akimtishia kumuua kwa kipindi kirefu, ambapo siku ya tukio alirudia kauli hiyo kabla hajaenda kuchukua kitofali na kujaribu kumpiga nacho ambapo alikikwepa.
Alisema kuwa tayari alishatoa taarifa polisi na kupewa kumbukumbu: AR/RB/1759/2013 aliyoifungua Februari 12, mwaka huu, baada ya kuwa anapokea vitisho vya kuuawa kutoka kwa Lema kupitia simu yake ya kiganjani.
Kuhusu kusimamishwa uongozi, Mwigamba alisema kuwa ametii licha ya kuwa kikao kilichomsimamisha hakina mamlaka kisheria, huku akiweka wazi kuwa hayuko tayari kukihama chama hicho, kwani bado anaamini ndicho chenye uwezo wa kuleta mabadiliko nchini.
Hata hivyo, tuhuma za Mwigamba zilikanushwa na Katibu wa CHADEMA wa mkoa, Amani Golugwa, akisema ni uongo dhidi ya Lema, kwani kwenye taarifa yake aliyowasilisha juzi kwenye kikao cha uongozi wa kanda alimsifu mbunge huyo kwamba ameongoza harakati mbalimbali za ujenzi wa chama kwa mafanikio makubwa, zikiwamo kampeni za ushindi wa kata nne zilizofanya uchaguzi mdogo hivi karibuni.
“Kwa kipindi chote ambacho amekuwa hayuko kazini Lema amekuwa akimsaidia hata kukamilisha ujenzi wa nyumba yake maeneo ya Sokon 1, hata anavyokwenda kwenye kesi zake Dar es Salaam ni Lema amekuwa akimsaidia gharama.
“Hicho alichokizungumza kwenye mkutano wake juu ya malalamiko ndiyo anatudhihirishia kuwa amekuwa nyoka na mnafiki ndani ya kundi letu,” alifafanua katibu huyo huku akisema hakuna malalamiko yoyote juu ya suala hilo ndani ya chama.
Golugwa aliongeza kuwa baada ya kupitia kompyuta ya Mwigamba wamebaini mambo mengi machafu na ya hatari kwa mustakabali wa chama ambayo yanawagusa watu wengi.
Hata hivyo hakutaka kuingia kwa undani wala kuyafafanua akisema yatakisaidia chama katika uchunguzi wake zaidi, na kwamba tayari kikao cha Baraza la mkoa kimeshakaa na kimemwandikia Mwigamba barua ya ajieleze ni kwa nini asivuliwe uongozi ikiwa ni sehemu ya mchakato wa kulifikisha suala hilo mbele ya kikao cha Kamati Kuu ya Taif

[TD="bgcolor: #ffffff"]
• CHADEMA yadai kompyuta yake ina siri zitakazogusa wengi

na Grace Macha, Arusha


[/TD]
[TD="width: 200, bgcolor: #FFFFFF, align: center"][/TD]
[/TD]

CHANZO TANZANIA DAIMA.
 
Silaha kubwa ni kujihami,safi kabisa ulivyompiga ngumi huyo mgema ulimbo.
Nalog off
 
CDM ni mwiba mkali sana kwa CCM! Kila mbinu zinatumika ili kuisambaratisha CDM kama Ukanda, ukabila, Udini, Ugaidi, Ufisadi, mabomu na B7 Lumumba Project! Tayari mbinu hizi zimeshagota na zimeshindikana vibaya sana, kwani CDM ndio kwanza inashamiri!! Sasa wanapiga mayowe ya kutaka Demokrasia ndani ya CDM. Mbinu hii nayo itashindikana pia!!
 
Kila aina ya mbinu chafu za magamba zinagundulika mapema. Nyoka wanagongwa vichwa kitambo! Chadema inaendelea kutakasika mapema asubuhi wakati CCM inaendelea kuwa najisi hadi jioni!!!
 
Kwa hapa cdm tulipofika, hakuna msaliti aliye salama! Wajiandae.
 
Jamaa alipigwa sana na vijana wa Chadema.

Mkuu Ritz
Hii habari imeacha hoi yaani hiki chama hakifanani na jina lake yaani jina lako kama sio Masawe; Tarimo; Lema au Lyimo uanachama wapo mashakani; hivi kama jina langu ni Mwita Maranya au Mohamedi Mtoi kweli nakubalika kwenye chama hiki? Mkuu hiki chama kingetafuta jingine maana demokrasia hakuna ni ubabe mtupu; maendeleo hakuna hata kimeshindwa kujenga pamoja na kupokea ruzuku ya mabilioni hiki chama afadhali kijiite MEKU Brotherhood tujue moja!
 
Back
Top Bottom