Mufindi Kusini Wamzawadia Rais Samia Ng'ombe

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MUFINDI KUSINI WAMZAWADIA RAIS SAMIA NG'OMBE

“Zawadi hizi; Ng'ombe Wawili, Mmoja kwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwingine kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo zimetolewa na Wana-Mufindi Kusini na mimi ninazikabidhi kwa niaba ya kuwawakilisha wananchi wa Mufindi Kusini, kadhalika wamenituma niwasilishe salamu nyingi kwa Rais Samia na pongezi kwa kazi kubwa na nzuri zenye msingi wa kujenga na kuboresha taifa bora" - Mhe. David Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la JMT kwa niaba ya Wananchi Mei 28, 2023 amekabidhi zawadi ya Ng’ombe wawili kama ishara ya shukrani kwa Rais kwa kazi kubwa na nyingi alizoweza kuzifanya na kuzitekeleza katika nchi kwa ujumla hususan katika jimbo la Mufindi Kusini kwenye Sekta mbalimbali kama vile Elimu, Umeme, Afya, Barabara, na Maji.

FxRywSLXwAMqutn.jpg
FxRyvf6WIAAV6d_.jpg
FxRywwjXsAERMBe.jpg
 
CCM bado hamjaacha siasa za kizee. Mnaigiza kuleta ng'ombe ili kuhadaa umma kuwa mnakubalika sana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom