Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, kwanini usijiuzulu?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Lango la kuingia nchini linapokosa mtu makini lawama na kudumaa Kwa huduma lazima kuwepo; Kwa kipindi kifupi toka kuzinduliwa Kwa terminal 3 madhaifu yafuatayo yapo wazi na Kila msafiri makini anayaona.

1. TV zinazoonyesha ratiba ya safari terminal 2 zimeondolewa, hivyo hakuna sehemu unapata huduma yakutambua ndege Yako inaondoka saa ngapi au mpendwa wako anaingia saa ngapi.

2. Spika za matangazo hazifanyi kazi au matangazo ayatolewi Kwa mujibu wa sheria na taratibu kama viwanja vingi vya Kimataifa vinavyopaswa kufanya kazi.

3. Kukosekana Kwa matangazo na kuondolewa Kwa tv za matangazo kumepelekea wasafiri wengi kukataliwa kusafiri Kwa kuambiwa geti zimefungwa na wanapolalamika mbona walikuwa uwanjani awapewi msaada.

4. Hakuna mtu anayesimamia huduma za precision na air Tanzania, watoa huduma wapo too slow lakini pia wanarundikana kaunta wakipiga stori huku wateja wapo Kwenye foleni.

5. Nimesafiri mara kadhaa mwaka huu kila ukiingia uwanjani usipokutana na abiria wanalalamikia huduma za air Tanzania utakutana na lawama kwenye ndege. Inaonekana wapo baadhi ya wafanyakazi wa air Tanzania wanatoza wasafiri fedha kinyume na tiketi zao,au wapo wahudumu wanakataa kuwahudumia wateja Ili wawalipishe tiketi upya na wapewe commission na shirika au wapo watu wanaoshindwa kuwajibika kutoa taarifa SAHIHI Kwa wateja nk naamini Kuna uzembe

6. Hakuna siku nimewahi kusafiri na air Tanzania nikaona wahudumu wao wakitafuta wateja ambao walifanya booking wakalipia lakini awajacheck in; ukienda viwanja vyote vikubwa lazima uone wahudumu wa mashirika ya ndege wakitembea Hadi nje ya uwanja kutafuta abiria ambao awajacheck in . Hapa Kwetu utadhani tuna laana; muhudumu kuangalia system na kutoka kutafuta abiria kabla yakufunga kaunta hakuna na hapa Nadhani ndipo Dili linapofanyika. It's like wapo tayari ndege iende na watu wawili lakini waache abiria au wawakatishe tickets twice.

Haya na mengine mengi yanakufanya ujiulize msimamizi wa Uwanja huu yupo serious? Anafanya ukaguzi-? Wageni kutoka nje hasa wanaokwenda kwenye utalii kaskazini wanalalamikia hizi huduma zetu sijui anasikia? Spika inacost shilingi ngapi? Mtoa matangazo Kwanini asiwajibishwe? Huyo aliyetoa screen anasubiri Nini ofisini? Air Tanzania Kwanini wahujumu shirika Kwa huduma mbovu wasiwajibishwe? Don't you have standards? Wageni wanaposikia makelele uwanjani mnajisikiaje? It's shame mjue? But why everyday mnarudia same mistakes? Je, hakuna CCTV camera zakuonyesha ubovu wa watoa huduma?

Naamini terminal 3 Haina Muda nayo itakufa Kwa sababu mentality ni zile zile; mkurugenzi Toka ofisini angalia miundombinu ya uwanja inavyohudumiwa lakini pia angalia watoa huduma sidhani kama wanakutakia mema.

Contrary basi tutaanza kuamini mnamhujumu mama Kwa Sasa yule Mzee amkumfanyia haya; mnataka air Tanzania ipewe jina baya ikose abiria Jambo ambalo Lina tija Kwenu ila halina tija Kwa Taifa.

Roho wa Mungu akuongoze uwekeze Kwa watoa taarifa wanaokuambia nini kinafanyika hapo uwanjani kwako; Hali si shwari.
 
Consistency kwa mwafrika ni msamiati mgeni sana, hushangai mwendokasi tu mpk leo tiketi zinachanwa badala ya scanners kukagua.

Mfano rahisi; kama ulikulia pahala choo ni kwenda vichakani, mara nyingi yale maisha utajikuta unaendelea nayo hata kama si 100%
 
Anaitwa nani huyu mkurugenzi....
Shughuli iliyopo pale ndio maana nchi nyingi ziliamua kusitisha safari za Tanzania wanaamua kwenda Kenya
Huduma mbovu.

Wafanyakazi wengiiii unashindwa kujua swala la security lipo vipi
Mkurugenzi pengine hata Nairobi tu hajawahi kufika.

Sehemu kama hizi wapeni kazi waliopata exposure kidogo

Huduma kwa wateja ni mbovu kila mahali sijui shida ni nini?
 
Lango la kuingia nchini linapokosa mtu makini lawama na kudumaa Kwa huduma lazima kuwepo; Kwa kipindi...
Nasema hivi, Sijiuzulu Ng'o.

Hivi wewe katika vitengo vyote vya mamlaka za Serikali umeona hichi changu tu? Binti mbona una nongwa sana wewe?

Niambie ni mamlaka gani iliyoko chini ya Serikali hii ambayo wewe unaona kila kitu kiko perfect mpaka uje uiseme hii ya kwangu? Yaan ushaenda Bandari, TRA, TBS, Ewura, Latra, Sumatra, Tanesco, Dawasco au ATCL, Mifuko ya Jamii, etc ukaona utendaji wao mpaka uje useme eti nijiuzulu?

Na nikijiuzulu nikakosa mshahara nitakula Nini? Utanisaidia kulisha na kusomesha Watoto wangu? Nijiuzulu ili nikose posho na marupurupu ya vikao na Safari mbalimbali ambazo zingine najitungia mimi Mwenyewe?

We unavyoniambia nijiuzulu utanipa wewe VX ya kutembelea? Unaona wivu sana navyoweka kishoka nikiwa naendeshwa kurudisha au kuchukuliwa nyumbani ee? Au utanipa wewe Allowance ya Nyumba ingawa naishi kwangu?

Wewe nani umemuona wa Level ya Mkurugenzi amejiuzulu kwa tumakosa tudogo tudogo kama hutu mpaka uje uniambie Mimi pia nifanye hivyo? Na nikijiuzulu nani ataniita Boss? Au unadhani sipendi sifa za kuitwa Boss? Unadhan sipendi kunyenyekewa?

Unajua hata nimehangaika vipi kupata hichi cheo mpaka uje useme kirahisi tu kua eti nijiuzulu? Usitake nitoe siri zingine za ndani mpaka leo unaniona niko hapa, lakin nakuapia kwa sababu ulizozitoa mimi kujiuzulu hiyo sahau.

Mambo ya hizi taasisi zetu hayaendi kiholela kama unavyodhani. Lazima ufanyike upembuzi yakinifu, iitishwe tenda, apatikane mzabuni, afanyiwe vetting kupitia vikao mbalimbali ambavyo vitahitaji gharama mbalimbali kama vile posho ya kikao, refreshments, ukumbi, etc, ipatikane bajeti ya huo ukarabati n.k. Hivi vyote vinahitaji muda na fedha ili tufanye kwa umakini zaidi.

Sio unakurupuka tu eti nijiuzulu.
 
Mkurugenzi kazi yake kujifungia ofisini na kusubiri ripoti ziletwe asaini... Hana muda wa kwenda kwenye ground.

Asuhuhi kwake ni muda wa kusoma magazeti. Ikifika saanne breakfast heavy baada ya hapo soga na wageni.

Saa saba lunch na kukimbia huku na kule nje ya uwanja kwenye dili binafsi na mikutano isiyo na faida
 
Consistency kwa mwafrika ni msamiati mgeni sana, hushangai mwendokasi tu mpk leo tiketi zinachanwa badala ya scanners kukagua...
Ndio huwaambiaga watu siku zote. Unategemea nini kumchukua mmoja wa dada zetu anayetoka kijijini kwenye nyumba zetu za udongo ukuta na sakafu, unampeleka course ya housekeeping ya miezi 3 halafu unampa kazi ya usafi kwenye hoteli ya 3-5 stars.

Kwake yeye vumbi na mchanga sio uchafu bali ni part ya jengo.
 
Lango la kuingia nchini linapokosa mtu makini lawama na kudumaa Kwa...
Mkuu 'Bea', Umesomeka.

Lakiiiniiii, naomba siku nyingine utuwekee ofisi nyingine yoyote ya serikali ambayo umeingia na kuhudumiwa vizuri.

Tunaomba utupe mrejesho wa furaha yako hapa ili nasi tuungane nawe kusifu mafanikio ya ofisi hiyo.

Usibeze wala kudharau, hili ni ombi maalum kwako. Wengi tutafurahi sana kujua kumbe kuna sehemu serikalini wanakofanya kazi nzuri kwa kujituma, wakizingatia kuipeleka nchi hii hatua kadhaa mbele.
 
Mamlaka za ndege Tanzania zipo far better compared to others in Africa, hasa Africa ya Kati.

Sisi tupo vizuri na tunaboresha kila siku. Mkae kwa kutulia
 
Karibu kila kitengo nchi hii kinaongozwa na makada wa CCM ambao upeo wao uko chini sana. Usitegee matokeo chanya.
Huku ni kuhamisha magoli, sioni mantiki ya uingizaji wa ccm hapa kwenye mada ya msingi kama hii. Mtoa mada ameeleza kwa ufasaha kabisa. Watanzania tuna shida vichwani mwetu sio bure.
 
Wale Wahudumu wa Terminal 2 wana njaa hatari,wanaomba hadi kero,mtu unaenda kuchagua seat unakutana na malalamiko sijala sina nauli leo Sister ,mara Mama yangu Mgonjwa siku nyingine Michango ya Harusi yani kero tupu!Nilijaribu kuvaa uso wa nyani labda wataniogopa wapi,hii kero ya Wafanyakazi kuwa ombaomba ni janga lingine kubwa.
 
Mkuu 'Bea', Umesomeka.

Lakiiiniiii, naomba siku nyingine utuwekee ofisi nyingine yoyote ya serikali ambayo umeingia na kuhudumiwa vizuri.
Tunaomba utupe mrejesho wa furaha yako hapa ili nasi tuungane nawe kusifu mafanikio ya ofisi hiyo.

Usibeze wala kudharau, hili ni ombi maalum kwako. Wengi tutafurahi sana kujua kumbe kuna sehemu serikalini wanakofanya kazi nzuri kwa kujituma, wakizingatia kuipeleka nchi hii hatua kadhaa mbele.
Halafu maofisi yote yanafungwa camera, sijui wanaona ni za mapambo?
 
Back
Top Bottom