Nani angesaidia kuharakisha mchakato wa Ujenzi uwanja wa ndege Mwanza, TAA au TANROADS, naomba mawazo yenu

dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
1,460
1,444
Ni kweli suala la mchakato wa ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege Mwanza limechukua muda mrefu na sasa wananchi waliahidiwa Mwezi February 2024 mkataba ungesainiwa hapahapa Mwanza. Tuliamini baada ya TAA kukabidhiwa na mkoa kasi ingeongezeka na hususani baada ya Rais kutoa bn 30 kazi ianze, na maelekezo yake ya Mwanza lakini hadi sasa kimya, TAA wanasemaje?

Wananchi tunaanza kuingiwa na wasiwasi na hii taasisi kuhusu utekelezaji wa mradi huu.Mkuu wa mkoa ametimiza wajibu wake kuwakabidhi mradi na hata kuwashirikisha NSSF,kulikoni kwa sasa,siasa ziachwe kwenye miradi muhimu kama hii, huku ni kukosa uzalendo. Pengine TANROADS wangefaa zaidi kuliko TAA ni wazito, hususani kwenye uwanja huu wa Mwanza, kulikoni!
 
Back
Top Bottom