Mkurugenzi wa Rita Tunaomba uchunguzi cheti cha kifo No 100000203415(MOSHI)/ tangazo la kifo BD 0668249(Dar)Marehemu kafia dar kaishi dar +mirathi mo

Kuna mambo mengi naona kama unayaficha kwa nia ovu. Nina maswali mengi sana juu ya hili suala lako. Kama uko serious kabisa na Jambo hili na kwa hakika/dhati kabisa unahitaji msaada, uje inbox kwangu endapo kama unaogopa kuweka wazi details zote hapa Jf
Kesi za Mirathi au za migogoro ya ardhi zinazowahusu watu wa Kaskazini mara nyingi huwa zinakuwa ngumu sana ku-deal nazo, sababu ni kwamba wahusika mara nyingi huwa wanajihusisha na udanganyifu mwingi sana. Unapaswa kuwa makini sana na mwangalifu kupitiliza unapojihusisha na migogoro ya watu hawa.
 
Kama upo serious kuwasaidia Watoto wa marehemu peleka hii barua makao makuu ya Polisi Dar kitengo cha fraud, peleka barua nyingine kwa DCI.

Kisha nenda wizara ya Ardhi Dar omba kuonana na kamishna wa Ardhi, mueleze hii scenario yote na mumpe maombi ya kufunguwa CAVEATE.

Hiyo CAVEAT ikitolewa hakuna Nyumba wala Ardhi ya marehemu inayoruhusiwa kuuzwa mpaka mkae sawa.

Mwisho kaeni kikao cha familia badilisheni Msimamizi wa mirathi andaeni muhktasari pelekeni hiyo Mirathi mahakama ya juu pale Temeke Chang'ombe one stop center, kuna majaji kabisa pale.
PhD woote waliopo sisiemu wangekuwa na akili km wewe hii nchi ingekuwa mbali sana! huu ushauri wako ushamaliza kila kitu mtoa mada aufuate tu..
 
Back
Top Bottom