Kwa nini mtoane Roho kwa mali alizoacha baba? Ijue Sheria ya MIRATHI, WOSIA na Usimamizi wa mali zitokanazo na Mirathi

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
3,022
5,254
Binadamu wote ni lazima tupitie kifo ikiwa ndio mwisho wa maisha yetu hapa duniani. Wakati wa uhai mtu unaweza kumiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika mahali tofauti tofauti ndani au nje ya nchi ya Tanzania. Kuondoka kwako duniani kwa njia ya kifo hakufanyi mali zako zipotee kwa kuchukuliwa na watu wasiokuhusu kwa kuwa tu hakuna usimamizi au mgawanyo sahihi. Uhamaji wa umiliki wa mali kutoka kwa marehemu kwenda kwa wapendwa wake walio hai ndiyo huitwa MIRATHI. Kufanikisha uhamaji huo, Bunge la JMT liliamua kutunga Sheria za Mirathi kuongoza na kusimamia ugawaji na usimamizi wa mali za marehemu.

Naitwa Lusajo W. Mwakasege, Mwanasheria na Co-Partner wa Marm and Associates Advocates, namba yangu ya simu ni 0713-368153 (inapatikana whatsapp na telegram) na barua pepe yangu ni mwakasege@gmail.com. Tuanze somo letu:​

A: NI SHERIA ZIPI ZINAZOSIMAMIA MAMBO YA MIRATHI TANZANIA?

👉Sheria za Kimila (Customary Laws)

👉Sheria za Kiislamu ikiwa ni pamoja na Quran na Sharia

👉Sheria ya Mirathi na usimamizi wa Mirathi, Sura ya 352 pamoja na kanuni zake,

👉Sheria ya urithi (The Law of Succession Act)

👉Pamoja na Sheria ya Mirathi ya India

B: NINI KIFANYIKE BAADA YA KIFO?
  • Sajili kifo kwa msajili wa vizazi na vifo (RITA);
  • Kikao cha ukoo kifanywe na uandikwe muhtasari wa kikao hicho pamoja na mahudhurio yakiwa na saini za waliohudhuria;

  • Kikao kinafanyika kwa ajili ya:
    • Kutambua majina ya warithi wa marehemu,
    • Kutambua kama marehemu aliandika wosia (uonekane) au la kuhusiana na mali zake,
    • Kutambua mali za marehemu na mahali zilipo,
    • kutambua madeni ya marehemu anayodaiwa na anayodai,
    • Kutambua sababu za kifo cha marehemu
    • kutambua hali ya kiimani ya marehemu enzi za uhai wake;
    • kutambua hali ya ndoa ya marehemu;
    • Kutambua sheria na mahakama zitakazohusika na mirathi hiyo;
    • Kumteua msimamizi wa Mirathi ya marehemu.
Muhtasari wa kikao uoneshe yafuatayo:

  • Majina ya warithi wa marehemu,
  • kutambua hali ya ndoa ya marehemu;
  • uwepo wa wosia wa mwisho wa marehemu au la,
  • Kama kuna wosia, uoneshe yaliyomo ndani ya wosia
  • Orodha ya madeni yaliyotambuliwa ya marehemu anayodaiwa ama anayodai,
  • uteuzi wa msimamizi wa mirathi ya marehemu

C: NI KINA NANI WANAORUHUSIWA KUOMBA USAJILI WA KIFO CHA MAREHEMU?
  • Ndugu wa karibu wa marehemu waliokuwepo wakati na mahali ambapo kifo cha marehemu kilitokea au waliowahi kumtembelea akiwa katika ugonjwa siku za mwisho za uhai wake;
  • Ikiwa ndugu wa karibu hawapo, basi ndugu yoyote wa marehemu anayeishi ndani ya Wilaya kifo kilipotokea;
  • Kama ndugu hawapo, mtu yeyote aliyekuwepo mahali na wakati kifo kilipotokea, AU
  • Mmiliki wa nyumba ambapo kifo kilitokea;
  • Ikiwa mwenye nyumba hayupo, basi Mkazi yeyote wa nyumba ambayo kifo kilitokea;
  • Mtu aliyehusika na utunzaji wa mwili wa marehemu au aliyeagiza mazishi ya mwili huo (mfano, polisi au mahakama au viongozi wa mamlaka za serikali nk)
KIFO KINATAKIWA KUSAJILIWA NDANI YA MUDA UPI?
Muda ni ndani ya siku thelathini (30) kutokea tarehe ya kifo. Msajili wa vifo anaweza kuruhusu usajili ufanyike ndani ya miezi mitatu kutoka tarehe ya kifo ikiwa ataridhika na sababu za kuchelewa kusajili kifo ndani ya siku 30.

KIFO KINASAJILIWA WAPI?

Katika Ofisi za Msajili Mkuu wa vifo au katika Ofisi za Mkuu wa Wilaya kifo kilipotokea ambapo kuna wasajili wa wilaya (RITA)

JE, NI MUHIMU KUELEZA SABABU ZA KIFO?

NDIYO
. Sababu za kifo huandikwa na tabibu anayetambulika na serikali katika cheti cha sababu za kifo na cheti hicho huwasilishwa na tabibu huyo katika ofisi za msajili wa vifo wa wilaya – fomu hii inaweza kupewa kwa ndugu wa marehemu anayefuatilia usajili wa kifo.

D: JE NI MUDA GANI KISHERIA UTEUZI WA USIMAMIZI WA MIRATHI UNAWEZA KUOMBWA?

Kanuni za Sheria ya Mirathi (PAEA Rules) inaelekeza kuwa kipindi kinachoruhusiwa kuomba uteuzi wa usimamizi wa mirathi ni ndani ya muda wa miaka mitatu (3) kutoka tarehe marehemu alipofariki dunia.

Je, usimamizi wa mirathi unaweza kufanywa baada ya miaka mitatu (3) kupita?

NDIYO
, inawezekana kuomba uteuzi wa usimamizi wa mirathi nje ya muda wa miaka mitatu kwa kueleza sababu zilizofanya maombi hayo yasifanyike ndani ya muda.

👉Ni vyema kupata huduma ya wakili kukusaidia kufanya maombi ya uteuzi wa usimamizi wa mirathi yanayofanyika nje ya muda. Ikiwa utahitaji msaada kwa hili, wasiliana nasi kwa maelezo zaidi.

E: NI SEHEMU IPI NI SAHIHI KUOMBA MAOMBI YA MIRATHI?

👉Mahakama ya Mwanzo – ikiwa mirathi inaombwa kwa sheria za kimila ama za dini ya kiislamu

👉Mahakama ya Wilaya – ikiwa mirathi inaombwa kwa sheria ya mirathi

👉Mahakama Kuu ya Tanzania – ikiwa mirathi ina utata kidogo juu ya sheria ipi inayopaswa kutumika kati ya sheria ya kimila, dini ya kiislamu au sheria ya mirathi

Utumizi wa Sheria hizo ni kwa kuzingatia hali ya kiimani na kimaisha ya marehemu kabla ya kifo chake, mfano kama marehemu alikuwa ni mtu wa kuzingatia mambo ya kimila ya kabila lake, basi mirathi yake itaombwa kwa mujibu wa sheria za kimila.
 
F: JE NI NANI ANAWEZA KUWA MSIMAMIZI WA MIRATHI YA MAREHEMU?

Sheria inaelekeza kuwa mtu yeyote aliyetajwa katika Wosia halali wa Marehemu anaweza kuwa Msimamizi wa Mirathi isipokuwa kama mtu huyu ni mtoto (chini ya miaka 18) au asiye na akili timamu.

👉Si lazima mtu huyu awe ni ndugu wa marehemu au mwezi wa marehemu, hata rafiki wa marehemu anaweza kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu.

👉Mtu yeyote mwenye maslahi (interest) na mali za marehemu anaweza kuomba kuteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi ikiwa hakuna wosia ulioachwa na marehemu;

JE NI LAZIMA KUSIMAMIA MIRATHI YA MAREHEMU HATA KAMA HUPENDI?

Sheria inaelekeza kuwa si lazima mtu awe msimamizi wa mirathi ikiwa hapendi kufanya hivyo.

Hata hivyo ikiwa marehemu alimteua mtu kwa wosia halali kuwa msimamizi wa mali zake (marehemu) na mtu huyo hayuko tayari kuwa msimamizi, ni lazima mtu huyo aukane mahakamani uteuzi uliofanywa na marehemu kumchagua yeye kama msimamizi wa mirathi yake.

G: NAMNA GANI YA KUWASILISHA MAOMBI YA MIRATHI?
Uwasilishaji maombi unategemea na ngazi ya mahakama unayotakiwa kisheria kuwasilisha maombi.

👉Kwa mahakama ya Mwanzo unajaza fomu namba 1 ikiwa imeambatishwa na muhtasari wa kikao cha ukoo au familia pamoja na cheti cha kifo cha marehemu

👉Kwa mahakama ya Wilaya au Mahakama Kuu ya Tanzania unajaza fomu ya maombi (petition) ikiambatana na muhtasari wa kikao cha ukoo.

📌Unashauriwa kutumia huduma ya mawakili ili waweze kukushauri na kukusaidia kujaza kwa usahihi fomu hiyo (namba 1) au petition kulingana na mazingira ya kifo cha marehemu kwa kuwa maombi hutofautiana pale ambapo kuna wosia na ambapo haupo, ama kukiwa na wosia lakini hauonekani ama umeharibiwa au umepotea nk,

H: NI NAMNA GANI YA KUPINGA UTEUZI WA MUOMBAJI WA MIRATHI?

Uteuzi hupingwa kwa kuwasilisha pingamizi mahakamani baada ya mahakama kutoa Notisi (taarifa) ya kuwasilisha mapingamizi dhidi ya mwombaji.

Taarifa hii ya kuomba uteuzi hubandikwa katika mbao za mahakama na pia huchapwa katika gazeti lenye wasomaji wengi na linalosambazwa sehemu kubwa ya nchi (gharama za kuweka tangazo gazetini ni za mwombaji)

I: Je, NI SABABU ZIPI ZINAZOWEZA KUTUMIKA KUPINGA MAOMBI YA UTEUZI WA MWOMBAJI WA USIMAMIZI WA MIRATHI?
  • Ikiwa mwombaji sio mtu aliyeteuliwa katika wosia;
  • Ikiwa afya ya kiakili ya mwombaji haipo sawa wakati wa kuomba uteuzi;
  • Ikiwa mwombaji anaomba uteuzi kwa kutumia wosia ulioghushiwa (forged will);
  • Ikiwa mwombaji ameacha kuwaweka katika maombi yake warithi na wanufaika wa marehemu;

NINI KINAFUATA IKIWA HAKUNA PINGAMIZI?
Muombaji huthibishwa na mahakama na kuteuliwa kuwa msimamizi wa Mirathi ya Marehemu.

J: NINI UWEZO/MAMLAKA NA MAJUKUMU YA MSIMAMIZI WA MIRATHI?

  • Kushtaki kuhusiana na mali za marehemu kwa jina la marehemu; Yaani Msimamizi wa mirathi anaweza kuwafungulia kesi wadai wa marehemu au wowote wanaosumbua mali za marehemu, vilevile na yeye anaweza kushtakiwa kwa niaba ya marehemu.
  • Kufanikisha mazishi ya marehemu katika namna aliyotaka marehemu ikiwa marehemu aliacha fedha ya kufanikisha hilo;
  • Kutambua na kudai madeni ya marehemu;
  • Kuhamisha umiliki wa mali ya marehemu kwa namna yoyote ile atakayoona inafaa kama kuuza, kugawa, kukodisha nk;
👉 Ingawa busara ni kusikiliza maoni na mapendekezo ya warithi na wanufaika wa marehemu, Msimamizi wa mirathi anaweza kufanya mgao wa mali pasipo kuwashirikisha au pasipo kupokea maoni ya warithi;

Mfano, badala ya kugawa mali halisi anaweza kuiuza na kugawa fedha itakayopatikana nk

  • Kutunza na kuhifadhi mali za marehemu katika ubora (ikiwa mali hizo hazitagawiwa)
  • Majukumu mengine ni kwa mujibu wa tamaduni za kabila husika, ikiwa usimamizi wa mirathi umetolewa kwa sheria za kimila
 
JE, MSIMAMIZI WA MIRATHI ANAWEZA KUTENGULIWA?

Ndiyo
, msimamizi wa mirathi anaweza kutenguliwa na mahakama katika nafasi hiyo kwa maombi yatayofanywa na mrithi au mtu mwingine yoyote akiwa na sababu za msingi.

👉 Waone mawakili kwa msaada wa kuandaa maombi nk

K: SABABU ZIPI ZINAWEZA KUTUMIKA KUOMBA UTENGUZI WA MSIMAMIZI WA MIRATHI?

Afya ya akili – ikiwa msimamzi amekosa afya ya akili mara baada ya kuteuliwa kuwa msimamizi;

👉Kushindwa kutekeleza majukumu yake kama msimamizi – ikiwa msimamizi hatatambua na kukusanya mali za marehemu ndani ya miezi 6 basi anaweza kutenguliwa

👉Kutogawa mali za marehemu kwa warithi

👉Kufuja mali za marehemu

👉Kutumia mali za marehemu kwa maslahi yake binafsi

JE, MSIMAMIZI WA MIRATHI HULIPWA MSHAHARA AU POSHO NA WARITHI WA MAREHEMU?

Hapana, msimamizi wa mirathi halipwi mshahara bali huweza kutumia fedha au mali ya marehemu kufanikisha majukumu yake kama msimamizi wa mirathi. Mfano, anaposhtakiwa – gharama za kuendesha kesi zitatokana na mali za marehemu au kutoka katika mchango wa warithi wa marehemu.

📌Kama msimamizi wa Mirathi ni Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali (The Administrator General) basi hukata asilimia kadhaa ya fedha ya mirathi kama gharama za kutekeleza majukumu yake ya usimamizi.

L: JE, MAHAKAMA INAWEZA KUGAWA MALI?

Hapana
, kazi ya Mahakama ni kusikiliza maombi na kumteua msimamizi wa mirathi au kukataa maombi yake ikiwa yatapingwa. Inatakiwa kushia kwenye uteuzi tu na sio kugawa mali za marehemu.​
 
M: WOSIA

Nini maana ya Wosia?

Wosia ni nyaraka au maelezo ya mwisho yanayoelekeza namna ya kusimamia na kugawa mali za mtamkaji wa wosia pindi atakapokufa.

Je, kuna aina ngapi za Wosia?

Mbili
, Wosia wa mdomo na wa maandishi

Wosia wa Mdomo
Ni ule unaotolewa kwa mdomo pasipo kuandika popote. Mtamkaji anaongea jambo kuhusu mali zake na jambo hilo haliandikwi popote.

Wosia huu hotelewa wakati mtamkaji akiwa mzima wa afya au katika dakika za mwisho za uhai wake.

Hasara za wosia wa mdomo

Ni rahisi kwa wosia huu kupotoshwa;

Ni vigumu kuthibitisha uhalali wa wosia huo;

Wakati mwingine, mashuhuda wa wosia huu huwa ngumu kupatikana wakati mwombaji akiw anautoa;

Wosia wa maandishi
Ni ule unaokuwa katika mfumo wa maandishi.
👉 Unaweza kuandaliwa na mtamkaji mwenyewe au ukaandaliwa na wakili.

Faida za wosia wa mandishi:​
  • Ni rahisi kuukagua na kuona kama una kasoro;​
  • Sio rahisi kuupotosha na kubadili matakwa ya mtamkaji (mtoa wosia);​
  • Ni rahisi kutunzika;​
  • Ikiwa una kasoro, ni rahisi kupinga uhalali wake mahakamani​

Mifumo ya Wosia wa maandishi
  • Unaweza kuwa wa kuandika kwa mkono​
  • unaweza kuwa wa kuchapwa na kompyuta​
  • unaweza kuwa wa kuchwapa na kompyuta na kuandikwa na mkono​

N: Mambo ya kuzingatia kwenye wosia wa maandishi:

👉Hautakiwi kuandikwa kwa kalamu inayofutika (Penseli) – huu haukubaliki kisheria sababu ni rahisi kuchezewa

👉Chochote kitakachoandikwa baada ya saini ya mtoa wosia (mtamkaji) – hakitatambulika kisheria isipokuwa kama kutakuwa na saini tena ya mtoa wosia na mashahidi wake

Je, mtu anayeamini dini ya kiislamu anaweza kuandaa wosia?

Ndiyo
, anaweza kuandaa wosia na ukatambulika.
Isipokuwa wosia wake utagusa 1/3 tu ya mali yake kwa kuwa 2/3 ni lazima iende kwa warithi halali

Hata hivyo sio lazima kwa kuwa dini ya kiislamu tayari imekwishafanya mgawanyo wa mali katika sharia (Quran) 4:11 ambapo imeelezwa

👉Mtoto wa kiume atarithi mara mbili zaidi ya mtoto wa kike, na ikiwa watoto wa kike wapo wawili au zaidi, watarithi 2/3.

O: VIGEZO NA SIFA ZA WOSIA HALALI UNAOTAMBULIKA KISHERIA

👉Uwe umetolewa na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 21

👉Uwe na jina kamili la mtoa wosia

👉Lazima uwe na tarehe ya kutolewa wosia

👉Uwe umesainiwa na mtoa wosia mbele ya mashahidi wake (yaani wote – mtoa wosia na mashahidi wake) wasaini wosia kwa mara moja katika siku na muda sawa)

👉Lazima uwe na kauli kuwa umefuta wosia nyingine za awali zilizofanywa kwa mdomo au kwa maandishi - hii ni kuondoa mkanganyiko wa wosia upi ufuatwe kati ya huo na nyingine zilizotangulia

👉Uwe umeshuhudiwa na mtu asiyekuwa na maslahi na mali za mtoa wosia (isipokuwa mke au mume maana hawa ni lazima kushuhudia wosia wa wenza wao)

👉Uwe umeshuhudia na watu (mashahidi).​

  • Ikiwa ni wosia wa mdomo – mashahidi 4 na 2 kati yao wawe ni ndugu wa mtoa wosia​
  • Ikiwa ni wosia wa maandishi- mashahidi 2 na 1 kati yao ni lazima awe ndugu wa mtoa wosia​
  • Ikiwa ni wosia wa maandishi na mtoa wosia hajui kusoma na kuandika – mashahidi 3 pamoja na mke/mume wa mtoa wosia​

👉Mtoa wosia awe na ufahamu wa kilichotamkwa katika wosia;

👉Mtoa wosia anaweza kumteua msimamizi wa mirathi

👉Mtoa wosia anaweza kueleza hali ya afya yake ya mwili na akili wakati wa kuandaa wosia huo.

👉Uwe umebainisha mali za marehemu

👉Uwe umebainisha warithi wa mali za marehemu

👉Uwe umemteua msimamizi wa mirathi – ingawa sio lazima

P: JE, NI SABABU ZIPI ZINAWEZA KUTUMIKA KUPINGA UHALALI WA WOSIA MAHAKAMANI?

Afya ya akili ya mtoa wosa wakati wa kuandaa wosia husika

Ikiwa wosia ulipatikana kwa udanganyifu (fraud)

Ikiwa wosia ni bandia (forgery)

Ikiwa mtoa wosia hakuwa na ufahamu juu ya wosia husika

Usiwe umepatikana kwa njia ya kulazimisha (undue influence)

Ikiwa haujakidhi vigezo vya wosia mfano umeshuduiwa na watu wasiotimia idadi itakiwayo

Q: Sifa za mtoa wosia

Ni lazima awe na umri wa miaka 21 na kuendelea

Ni lazima awe mwenye afya nzuri ya akili wakati wa kutoa wosia huo

Ni kina nani wanapaswa kuwa mashahidi wa wosia?

👉Ndugu wa marehemu pamoja na watu wengine wasiokuwa warithi (mfano marafiki, majirani nk)

👉Mrithi wa mali za marehemu haruhusiwi kisheria kuwa shahidi wa wosia – isipokuwa tu kama ni Mke au Mume wa mtoa wosia (huyu ni lazima awe shahidi na pia ni mrithi wa mali za marehemu)

Katika wosia wa maandishi ni lazima mashahidi wawe ni wale wanaojua kusoma na kuandika

👉Ni lazima wawe na umri kuanzia miaka 15 na kuendelea

👉Ni lazima wawe na afya njema ya akili​
 
R: Je, Msimamizi wa mirathi hutakiwa kugawa mali kwa warithi baada ya muda gani?

Sheria ya Mirathi inamtaka msimamizi wa mirathi kugawa mali na kufaili mahakamani nyaraka ya kuonesha namna alivyozigawa mali ndani ya mwaka mmoja (1) kutoka tarehe alipoteuliwa.

Pia, Ndani ya miezi sita (6) toka kuteuliwa kwake, msimamizi anatakiwa kufaili mahakamani orodha ya mali za marehemu alizozibaini na anazokusudia kuzigawa kwa warithi​

NB: Kutokufanya hayo ni kosa la jinai na Msimamizi wa Mirathi akitiwa hatiani anaweza kuadhibiwa kwa kufungwa jela.

S: Je, Msimamizi wa Mirathi anaweza kuwa mrithi wa marehemu?

Ndiyo, msimamzi wa mirathi anaweza pia kuwa mmoja wa warithi wa mali za marehemu.
👉 Hata hivyo bado atatakiwa kugawa mali kwa haki bila kujipendelea

T: Ni mazingira yapi yanaweza kufanya mrithi wa marehemu kutolewa katika mirathi?

Ikiwa kwa makusudi hakumuuguza marehemu siku za mwisho za maisha yake;

Ikiwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa marehemu;

U: Wosia wa Pamoja (Joint Will)

Ni aina ya wosia unaoandaliwa na watu wawili (mke na mume) ukiwa na maelekezo ya umiliki wa mali baada ya mmoja wa wanadoa hao kutangulia mbele za haki.

📌Katika wosia huu, Mwanandoa mmoja akifa, umiliki wa mali zote huhamia kwa mwanandoa aliyebaki hai
📌Na mwanandoa aliyebaki anapokufa mali zote zinahamia kwa watoto wa ndoa hiyo.

👉Ni aina ya wosia ambao wanandoa hupenda kuutumia ili kulinda maslahi ya wenza wao pindi mmoja anapokufa na pia maslahi ya watoto wao pindi wote watakapokufa.

👉Wosia huu haubadilishwi wala mali zake kuguswa bila ruhusa ya wanandoa wote.

👉Hata mwanandoa mmoja akifa, mwanandoa aliyebaki hawezi kubadilisha chochote katika wosia huu.

Wosia huu unaondoa wasiwasi wa watoto kunyang'anywa mali au mali zao kufujwa mara baada ya mzazi wao mmoja kufariki dunia.

V: Wosia hutunzwa au kuhifadhiwa wapi?

Wosia ni nyaraka muhimu sana, utunzaji wake pia unahitajika uwe wa makini sana.

Wosia unaweza kutunzwa na
📌mtoa wosia mwenyewe mahali anapoamini ni salama na ambapo hapawezi kufikiwa na watu wanaoweza kuuiba, kuuharibu au kubadili (tampering) kilichoandikwa.

📌Siku hizi kuna baadhi ya benki za kibiashara wanatoa huduma ya kutunza wosia;

📌Pia Ofisi ya Usajili wa Vizazi na vifo (RITA)

📌Katika ofisi za mawakili walioandaa wosia au hata ambao hawajaandaa wosia huo;

📌Unaweza kutunzwa kwa rafiki au ndugu wa marehemu

W: MASWALI YA MARA KWA MARA

Je, nifanyeje pale ambapo ndugu hawataki kukaa kikao na kuandika muhtasari wa uteuzi wa msimamizi wa mirathi?

Sio lazima kuwe na muhtasari wa mirathi, unaweza kuomba usimamizi wa mirathi pasipo kuwa na muhtasari wa ukoo au familia.

Kama ndugu zako hawakubaliani na maombi yako watakwenda kupinga mahakamani ndiyo sababu muhtasari sio lazima.

Muhtasari sio lazima bali ni muhimu sana uwepo.

Je, nitafanyaje iwapo niliteuliwa na marehemu katika wosia kuwa msimamizi wa mirathi lakini wosia umepotea au kuharibika?

  • Kama umepotea, toa taarifa ya upotevu katika kituo cha Polisi​
  • Watafute mashahidi waliosaini wosia wakueleze tarehe ya wosia, ni nini kilichoandikwa katika wosia,​
  • Kafanye maombi ya uteuzi mahakamani​

Je, tutafanyaje ikiwa kuna familia mbili ambazo haziaminiani (ndoa ya wake wengi), msimamizi atatoka familia ipi?

Kama hakuna wosia, mnaweza kukubaliana na kuomba usimamizi wa mirathi kwa pamoja kutoka kila familia

Ikiwa mwombaji atakuwa ni wa familia moja – umekuja kujua tayari maombi yapo mahakamani – unaweza kuomba kuunganishwa nawe kama msimamizi katika maombi hayohayo

Ikiwa mnaona hali ni ngumu sana na kwamba mtakwamishana kutekeleza majukumu ya usimamizi – basi mnaweza kuomba Kabidhi Wasii Mkuu (the Administrator General) yaani Serikali ndio awe msimamizi wa mirathi.

Je, wajukuu wanastahili kurithi mali ya mtoa wosia kwa niaba ya mzazi wao aliyefariki?

HAPANA
, mirathi hutolewa kwa watu walio hai – aliyekufa hawezi kupewa mirathi. Wajukuu wanaweza kupewa urithi moja kwa moja na marehemu ikiwa kulikuwa na wosia na kama hakukuwa na wosia wanaweza kuomba kama ndugu baki wa marehemu (mazingira yanatofautiana tofautiana – wengine huenda walilelewa na marehemu, wengine huenda walimuuguza nk)

Je, kuna tofauti gani ya kufa huku umeacha wosia na kufa bila kuacha wosia?

Kukiwa na wosia

  • Mirathi hupatikana kwa urahisi kwa sababu mtoa wosia anakuwa ameelekeza kila kitu pamoja na mgawanyo wa mali zake​
  • Warithi wa marehemu wanakuwa wamejulikana​
  • Mali na madeni ya marehemu zinakuwa zimejulikana​

Kukiwa hakuna wosia
  • Ni rahisi kuibuka kwa mvurugano wa warithi kugombea mali za marehemu​
  • Ni rahisi kwa mali za marehemu kusahaulika na kupotea​
  • Ni rahisi kuibuka kwa madeni yasiyoeleweka​

Uombaji wa mirathi pia hutofautiana ikiwa kuna wosia na usipokuwepo.

X: HITIMISHO

Kwa sababu kifo ni kitu pekee cha uhakika kwa mwanadamu, ni muhimu kujiandaa nacho kwa kuweka mambo vizuri kupitia wosia.

👉Wosia ndio njia pekee inayopendekezwa kisheria na iliyo rahisi ya kugawa mali zako kwa wapendwa wako waliobaki hai baada ya wewe kufariki dunia; Tunapendekeza kila mtu awe na wosia aliouandaa kwa kuzingatia vigezo vyote vya kisheria ukionesha majina ya warithi wa mali zake pamoja na mali wanazorithishwa.

👉Masuala ya Mirathi ni ya kisheria – ni vyema kutumia huduma ya wanasheria ili kuandaliwa wosia wenye sifa zinazotakiwa na pia kuepusha mapingamizi ya kisheria kuhusu utekelezaji wa wosia huo.​
 
swali: cheti cha kifo cha hospitali kishria kimekaaje, kinakubalika mahakamani?
 
swali: cheti cha kifo cha hospitali kishria kimekaaje, kinakubalika mahakamani?
Cheti cha kifo ni cha serikali, yaani ni kama cheti cha ndoa vile. Kama hapo hospitali kimetolewa na wakala wa RITA basi kitatambulika tu mahakamani na kwingineko. Siku hizi baadhi ya hospitali kuna ofisi za RITA hapohapo, kwa hiyo vyeti vinavyotoka ni vya serikali na sio vya hospitali ingawa vinatolewa hospitalini.
 
Asante kwa wito
Ila nijuacho mirathi ni vita na mara nyingi hii vita huwa haiishi vizuri.
Ukiwa hai weka mambo yako sawa kwenye maandishi maana hata wale ambao walimtenga marehemu na kumfanya marehemu kuwaondoa kwenye urithi wa mali zake dakika za mwisho kutokana na matendo yao kwa marehemu pindi akiwa hai, watajitokeza mstari wa mbele as if hakuna kilichotokea.
 
Ni kweli kabisa, mirathi ni vita. Kwenye somo hili nimetoa wito watu wapende kuandika WOSIA unaokidhi matakwa ya kisheria ili kupunguza hiyo vita au misuguano baina ya wanandugu.
 
Ahsante sana sajo kwa elimu pana juu ya mambo ya mirathi .Haya yakikupata unaelewa umuhimu wa Elimu kama hii.
 
Asante kwa wito
Ila nijuacho mirathi ni vita na mara nyingi hii vita huwa haiishi vizuri.
Ukiwa hai weka mambo yako sawa kwenye maandishi maana hata wale ambao walimtenga marehemu na kumfanya marehemu kuwaondoa kwenye urithi wa mali zake dakika za mwisho kutokana na matendo yao kwa marehemu pindi akiwa hai, watajitokeza mstari wa mbele as if hakuna kilichotokea.
Mbaya sana... Huwa nachukia Sana Vita ya aina hii.... Ee Mwenyezi Mungu tuepushe nayo.
 
Kwasie waislamu tumeusiwa wakati wa kulala tulale na wosia wetu,tena mtume kasema ukilala weka chini ya mto upande wako wa kulia
 
Back
Top Bottom