Wewe mwanaume, umejifunza nini juu ya kifo cha Mr Ibu, msanii wa Nigeria?

Tafakari_nami

JF-Expert Member
Nov 4, 2016
779
1,517
Habari ya muda huu wana jamvi. Bila kupoteza muda basi naomba niende moja kwa moja kwenye mada.

Wengi wetu nina amini tuna mfahamu msanii aitwaye Mr Ibu kutoka nchini Nigeria, ameigiza filamu za vichekesho kama zile za akina Aki na Ukwa ma nyinginezo.

Huyu msanii kwa sasa ni Marehemu, Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani maana amepitia magumu mnoo kabla ya kifo chake na ukizingatia watu waliompitisha katika njia ya mateso kabla la umauti wake ni watu wa familia yake kabisa kwa maana ya wake zake na watoto.

Hivi ninauliza kuna haja ya KUOA kweli miaka hii kama watu tumekosa utu kiasi hiki kisa tuu uchu wa mali.
Wanaume nina uliza kuna haja ya kuoa, kuishi na mke kama mambo yenyewe ndiyo hivi, je wewe kama mwanaume umejifunza nini kutokana maswaiba aliyopitia huyu mwenzetu, wanawake mna roho mbaya shetani akasome.

Tuone maswaiba yenyewe aliyopitia Mr Ibu

1. Mke wake wa kwanza aliachana na jamaa, yaani alimpiga chini jamaa na kuchukua fedha zote walizochuma pamoja na zilizokuwa kwenye akiba.

2. Mke wa pili alimtuhumu jamaa kulala na binti yake, mara akaanza kuugua sana hasa ugonjwa wa kisukari baadaye akaanza kupatwa na tatizo la kuganda kwa damu, na mishipa ya damu ya miguuni ikaanza kufa kitu ambacho kili pelekea yeye kukatwa miguu, kumbuka hapa hakuwa na fedha za matibabu yeye kama yeye, ilibidi wasanii wa Nigeria wajichange ili apate fedha za kupatiwa matibabu hospitalini.

3. Binti yake alitumia pesa zilizo changwa kwa ajili ya matibabu ya baba yake Katika mambo yake binafsi.
Ina sikitisha sana hili hata mtoto hakujali afya ya baba yake.

Alafu kuna kijana anakuja oa huyu binti huko mbeleni, yaani mwanaume una oa mwanamke ambaye kipindi alipokiwa binti aliwahi kula hela za matibabu ya baba yake bila huruma wala kujali, hakika Mwanaume omba sana Mwenyezi Mungu akuongoze kabla ya kupata mke wako wa ndoa la sivyo ndoa inaweza ikawa ndiyo tiketi ya kujifungulia lango la kwenda kuzimu ukiwa hapa hapa duniani.

4. Mke wake img'ang'aniza na kumuomba sana Marehemu yaani Mr Ibu amnunulie iphone 15 wakati huo marehemu yupo kitandani ana umwa huku akijipigania uhai wake. Huyu ni mke au ni shetani aliyevaa ngozi ya binadamu. Dah!

5. Aliuza mali zake karibu zote ili apate matibabu ua miguu yake ila ikashindikana ikabidi waikate tuu, hapa weka au jumlisha na fedha alizokuwa ana changiwa na wasamaria wema na wasanii wenzake ila bado ikabidi Marehemu akatwe miguu, na wakati huo mke wake ana taka apewe iphone15.

Hizi simu za iphone zina laana kwakweli, kuna wengine wanauza mpaka figo ili tuj apate hela ya iphone. Mhhh!

6. Pamoja na kupambana kote kule ila Marehemu amefariki akiwa ameachwa bila Mke, yaani amekimbiwa na wake zake wote, bila Mali maana aliuza karibu zote, Pesa wala hakuwa na miguu maana ilibidi waikate tuu kule hospitalini.

Sasa tuangalie kilicho tokea mara baada ya kifo cha Marehemu.

Binti yake muda mchache mara baada ya kifo cha Baba yake, aliamua kuchukua account ya Tiktok ya Marehemu baba yake ambayo ipo verified, akabadili jina la account ya baba yake ya tiktok na kuandika jina lake likasomeka ka LADY JASMINE na wakati huo huo amefuta picha na videos zote za Marehemu Baba yake kwenye account hiyo.

Kwa haya tuu, je wewe MWANAUME kiumbe ambaye ume amriwa kula kwa jasho uende ukatafute kwa shida wakati wote wa mvua na jua bila kujali muda ili tuu uje ulishe familia, mke na watoto, tena wala huna kinyongo unaweza walisha miaka na miaka bila shida yoyote alafu mwisho wa siku siku zako za mwisho duniani uma ishia aibu ma fedheha kubwa kiasi hiki.

Dah! Ina uma na ina sikitisha mnoo. Wale wote aliyokuwa ana walea na kuwalisha bure leo hii ndiyo wame mtelekeza na kumfanyia unyama mkunwa kiasi hiki.

WANAUME TUISHI SANA KWA AKILI DUNIA YA SASA, HATA KAMA NI KUJITOA BASI TUJITOE KWA AKILI ILE DHANA YA KUSEMA MWANAUME TUMEUMBWA MATESO KUHANGAIKA NI KWELI SIJAKATAA ILA TUTUMIE AKILI SANA HASA KIPINDI HIKI BADO TUKIWA NA NGUVU ZA KUTAFUTA.
 
Mind you, huyo unayemuita binti yake sio mwanaye wa kumzaa bali ni mtoto wa Kuchukua Mitaani/ Vituo vya Yatima ambaye IBU alimlea tangu mdogo.

Hawa watoto tunachukua Vituo vya Yatima wengine wamelaaniwa by nature, ni vema kufuatilia historia ya wazazi wa mtoto kabla hujaokoteza SHUMILETA.
Rip Mr Ibbu
 
Duh aisee, mpaka nimehisi kulia
 
Ila wazee wa kataa ndoa wanajizolea point kila siku.
Kuna vitu vinaumiza sana wanadoa tunapitia.
Hichi chama kiangaliwe kwa jicho la 3, kuna kitu cha maana sana kwenye hichi chama japo hicho kitu kimejificha, huwezi jua umuhimu wake mpaka uingie kwenye ndoa, una kuja shtuka kumekucha, mara eeh tugawane mali mara ame kimbia na mali. Ndoa za sasa hivi ni kuviziana tuu
 
Mind you, huyo unayemuita binti yake sio mwanaye wa kumzaa bali ni mtoto wa Kuchukua Mitaani/ Vituo vya Yatima ambaye IBU alimlea tangu mdogo.

Hawa watoto tunachukua Vituo vya Yatima wengine wamelaaniwa by nature, ni vema kufuatilia historia ya wazazi wa mtoto kabla hujaokoteza SHUMILETA.
Rip Mr Ibbu
Kabisa. Mkuu ali waasili hao watoto na bado waka mfanyia hayo. Ila KARMA is real na haina huruma kabisa
 
Mind you, huyo unayemuita binti yake sio mwanaye wa kumzaa bali ni mtoto wa Kuchukua Mitaani/ Vituo vya Yatima ambaye IBU alimlea tangu mdogo.

Hawa watoto tunachukua Vituo vya Yatima wengine wamelaaniwa by nature, ni vema kufuatilia historia ya wazazi wa mtoto kabla hujaokoteza SHUMILETA.
Rip Mr Ibbu
Naskia ana watoto wakike wawili mmoja wa kuzaa na mwingine ndo wa kuadopt sasa cjui yupi ndo yupi
 
Mind you, huyo unayemuita binti yake sio mwanaye wa kumzaa bali ni mtoto wa Kuchukua Mitaani/ Vituo vya Yatima ambaye IBU alimlea tangu mdogo.

Hawa watoto tunachukua Vituo vya Yatima wengine wamelaaniwa by nature, ni vema kufuatilia historia ya wazazi wa mtoto kabla hujaokoteza SHUMILETA.
Rip Mr Ibbu
Sijui hiyo jamaa wala unaowaongelea, ila wakati nasoma, wazo lilijijenga kuwa ni malezi mabaya ya wahusika ndio yanapelekea yote haya. Hata hao wanawake wameokotwa mtaani tu akawafanya wake zake kama huyo mtoto. Unakosa aje utu kiasi hiki?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Kwamba ni hatua ya kuacha ulimwengu huu na kuendelea hatua ingine kama tulivozaliwa tukawepo na tutachimoka siku mwili taposhindwa mapambano ya kuendelea kubaki duniani
 
Mind you, huyo unayemuita binti yake sio mwanaye wa kumzaa bali ni mtoto wa Kuchukua Mitaani/ Vituo vya Yatima ambaye IBU alimlea tangu mdogo.

Hawa watoto tunachukua Vituo vya Yatima wengine wamelaaniwa by nature, ni vema kufuatilia historia ya wazazi wa mtoto kabla hujaokoteza SHUMILETA.
Rip Mr Ibbu
Duh
 
Back
Top Bottom