Mkoa gani ni mzuri kuishi?

Mkoa gani ni mzuri kuishi?

FaizaFoxy, hebu tuonane PM, nahitaji kiwanja cha kujenga nyumba hapo singida


Singida kuna Maziwa (mabwawa) ya asili makubwa mawili yako kila kando ya mji (mji uko kati), moja linaitwa Singidani na moja linaitwa Kindai. Pazuri sana kwa mwenye kuelewa.
 
FaizaFoxy, hebu tuonane PM, nahitaji kiwanja cha kujenga nyumba hapo singida
ram, mie sipo Singida sitoweza kukusaidia kwa hilo.

Nakushauri wasiliana amma na Mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji, au na Mkuu wa Mkoa, Dr. Parseko Kone, ni watu wenye kupenda sana maendeleo na wasikivu sana nna uhakika watakusaidia sana.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Dar pazuri mji msafi, hakuna foleni, hali ya hewa nzuri, Ardhi ya kilimo yenye rutuba n.k yaani dar panafaa sana
 
Uzuri wa mkoa ni pamoja na gharama za maisha kuwa chini nakushauri nenda Mbeya hasa wilaya ya Rungwe,kyela,ileje,mbeya vijijini na mjini basi,kule kwa akina Shonza yule Yuda Iskarioti usifike.
 
Ok, nikajua uko singida, manake umeufagilia kweli mkoa wa singida


ram, mie sipo Singida sitoweza kukusaidia kwa hilo.

Nakushauri wasiliana amma na Mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji, au na Mkuu wa Mkoa, Dr. Parseko Kone, ni watu wenye kupenda sana maendeleo na wasikivu sana nna uhakika watakusaidia sana.
 
Yakheee nenda Tanga Raha, hao wote wanakudanganya tu. Ulishawahi kusikia mkoa wa Tanga kuna njaa?

Mvua mara mbili, matunda yote unayoyajua wewe utapata Tanga, mazao karibu yote yanakubali ardhi ya Tanga. Hao mademu waliosema wengine huku wapo wa kumwaga na maji ya hiliki na mdalasini utawekewa bafuni na ukitaka kubebwa mgongoni pia utabebwa.

Kule twala samaki wa maji chumvi unachoma na kula bila kuweka chumvi sio wengine wanakula perege hata nyama hawana.

Wilaya za Handeni na Lushoto ziko mkoa gani? Au unajua Tanga mjinj tu?
 
Kwani mikoa ipo Bara tuu?wadau Znz nako hakuna mikoa ?
 
Ok, karibu sana kwetu singida mamii

Ahsante sana, nnapajuwa vizuri sana, mume wangu yuko kwenye mradi fulani huko na mimi huwa nakuja mara kwa mara. Kwenu kuzuri na nnadhani ntahamia huko panapo uhai na majaaliwa, nimependa sana nipate nyumba karibu ya Kindai.
 
Back
Top Bottom