Mkoa gani ni mzuri kuishi?

Mkoa gani ni mzuri kuishi?

ule mkoa anotokea Wapigwe tu tumechoka... Ni pazuri sana naskia. Pia watu wa mkoa huo ni wakarimu kama alivyo Wapigwe tu
 
Ila ki ukweli tarime isingekuwa mapanga, ni wilaya ambayo maisha yake ni very simple, vyakula bei rahisi, madukani vitu bei rahisi, shida ni kugechana tu
it's true tarime is the best place to live in tz kama cyo kugecha na kutema kunakofanywa na akina mura
 
Kwani hauna kwenu? nenda kajenge na kuishi mkoani kwenu, kisha kapafanye sehemu pazuri pa kuishi; na sio kufuata mikoa ya watu ambayo wenyewe washapafanya pazuri kuishi. usikimbie kwenu!
 
Karibu NYANYEMBE EMPIRE,NYAMWEZI LAND a.k.a MBOKA MANYEMA almaarufu kama TABORA. Laki moja unatumia miezi miwili kwa matumizi ya nyumbani.

Mkuu, Tabora nyoka wamepungua siku hizi? Nakumbuka Cheyo A, kulikuwa kuna nyoka wana speed ya ajabu.
 
Shukraan, Nimebahatika kutembea mikoa kadhaa lakini kwa bahati ndogo tu siku wahi kufika Singhida ispokuwa kupitiliza !! Lakini nimeshaweka note na schdl. za kutemblea mustakabalin....Kabla ya Maji hayo kutoweka au kukauka maana naona Yamepungua vibaya sana. Tuombe mungu atuongezee mvua.kila la kheiri.

Halafu nadhani hili litakua ni tatizo la sehemu kadhaa ndani ya Tanzania, vyanzo vya maji vinapungua mno na kukauka. Nadhani tumelegalega kwenye kuhifadhi mazingira. Nilishangaa hata Moshi baadhi ya ile mifereji iliyokua ikititirisha maji mashambani imekauka. Ingawa ni mabadiliko ya hali ya hewa lakini inabidi tupambane kadri tuwezavyo.
 

Attachments

  • Photo0061.jpg
    Photo0061.jpg
    43.9 KB · Views: 169
Eh cjui huyu mtu aende wapi bce kila mtu anamuita aende mkoa aliopo..sasa ckia wewe nenda namtumbo nackia kila kitu kule ni kama bure vile..!!
 
Karibu Mbeya, tupo juu karibu na mbingu, Unapenda kula chakula gani? Mchele, Mbeya ndo nyumbani kwao. Chips, viazi mviringo bombaa vinatoka Mbeya. unataka ndizi? Tukuyu ndo Mungu alishusha migomba, Ugali? Mbozi - Mbeya Mahindi ndo yanakotoka. Unataka kulima zao gani? Cocoa? njoo Kyela, kahawa? njoo Mbozi, Ufuta? njoo chunya kwa Mh. Mulugo. Alizeti? nenda Ileje na Momba, Parachichi? nenda Rungwe, Chai? nenda rungwe, chikichi? Nenda Kyela. Unataka madini?? Dhahabu? nenda Cjunya ya Mh. Mwambalaswa na Mbozi kwa Mh. Zambi. mkaa wa mawe? nenda kiwira, mafuta na gesi? neza ziwa nyasa na ziwa Rukwa. Unataka kutembea wapi? Mbugani? nenda Ruaha maana siku hizi inaanzia Mbeya, au nenda Kitulo ukaone miujiza ya Mungu. Mapumziko?? nenda fukwe za ziwa nyasa, hakuna kama hiyo hapa Tanzania. Unataka nini tena bongo hiiii? Karibu Mbeya jiji la maziwa na asali.
 
Back
Top Bottom